Kwa Hili WCB mmechemsha

Sele Mkonje

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
643
845
Aje washkaji zangu wa nguvu!?

Kuna jambo sijalipenda hata #Kidogo na sina budi niliweke wazi. wiki iliyopita Kampuni ya WCB iliingia kwenye headliness baada ya msanii wake Diamond platnumz kuzuia uzinduzi wa Singo yake aliyowashirikisha Psquare ili kuruhusu msanii chipukizi wa WCB Harmonize kuachia singo yake mpya iitwayo matatizo.

Kiukweli ilikuwa ni jambo zuri sana kwa mondi kuonesha support kwa vijana wake lakini nimeshangazwa na kitendo cha WCB tena kumruhusu Mondi kuachia ngoma yake mpya huku ngoma ya Harmonize bado ipo "Yamoto" bado hata aijaanza kupoa. Hii itasababisha Watu kusahau singo mpya ya Harmo na kuipa nafasi kubwa zaidi singo ya mondi kutamba. Kibiashara kwa WCB ni faida kubwa sana bt kwa Msanii Harmonize ni unyonyaji.

Napenda kuwashauri WCB wawe na mpango maalum wa kuachia ngoma. Tujifunze kwa wenzetu wamarekani inapotokea msanii mmoja yupo kwenye Chat basi wasanii wengine humpa gap ili wasije wakafunikwa. WCB ni chama kubwa na natumaini hili mtalifanyia kazi.

Nawasilisha
 
Kwani harmonize na Diamond ni msanii mmoja mpaka nyimbo zote mbili zisitoke kwa pamoja?
Kwani wanashare fan base moja hadi idhaniwe kuwa mashabiki wataacha kusikiliza nyimbo ya harmonize na kuamia kusikiliza nyimbo ya diamond?
 
Hoja dhaifu sana.

Muziki ni promotion wanauwezo wa kupromote nyimbo zote zika kaa kwenye chart
kwa maana nyingine unajaribu kusema hata wengine wasitoe nyimbo mpaka ya harmonize amalize?

Pamoja na harmonize kutoa nyimbo mbona kuna nyimbo nyingine na zote zina pata air time? Swala kubwa hapa ni uzuri na ubunifu kwenye nyimbo watanzania hawana shida kuwa na hit song hata mia na zote wanazichagua na wana sikiliza.

Kama ni nafasi Diamond kawaachia nafasi kubwa tuu... Kama nyimbo zao nzuri zitabamba tuu na isitoshe wao ndio wameteka media zote nchini na wana mamanager wenye uwezo wa kupromote nyimbo zao sio shida.
 
#Aje washkaji zangu wa nguvu.!?
Kuna jambo sijalipenda hata #Kidogo na sina budi niliweke wazi. wiki iliyopita Kampuni ya WCB iliingia kwenye headliness baada ya msanii wake Diamond platnumz kuzuia uzinduzi wa Singo yake aliyowashirikisha Psquare ili kuruhusu msanii chipukizi wa WcB harmonize kuachia singo yake mpya iitwayo matatizo.
Kiukweli ilikuwa ni jambo zuri sana kwa mondi kuonesha support kwa vijana wake lakini nimeshangazwa na kitendo cha WCB tena kumruhusu Mondi kuachia ngoma yake mpya huku ngoma ya Harmonize bado ipo "Yamoto" bado hata aijaanza kupoa. Hii itasababisha Watu kusahau singo mpya ya Harmo na kuipa nafasi kubwa zaidi singo ya mondi kutamba. Kibiashara kwa WCB ni faida kubwa sana bt kwa Msanii Harmonize ni unyonyaji. Napenda kuwashauri WCB wawe na mpango maalum wa kuachia ngoma. Tujifunze kwa wenzetu wamarekani inapotokea msanii mmoja yupo kwenye Chat basi wasanii wengine humpa gap ili wasije wakafunikwa. WCB ni chama kubwa na natumaini hili mtalifanyia kazi.
Nawasilisha kwa hisani ya # McKonjeTv on instagram @mckonje

Kweli tunatofautiana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom