Ndalilo
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 3,674
- 8,313
Salaam Waungwana,
Mwanaume unamtongoza binti,kwa utashi,akili,utimamu,utahayari na uelewa wake anakukubali na kuanza mahusiano ya kimapenzi na wewe. Wote mnakuwa na furaha na mahusiano yenu na mnapanga mipango mingi ya kimaisha pamoja na kapeana ahadi za kuishi pamoja kwa ndoa. Lakini katikati ya furaha ya mapenzi unagundua mwenzio ametongozwa na ameridhia kuwa na mwingine zaidi yako. Kama alivyokukubali wewe ndivyo alivyomkubali na huyo mwingine na kwakujua kuwa ukijua hutoafiki,anakuficha.
Kwa hili, kuna sababu ya wewe kuchukia,kuwa mkali au kuanzisha bifu na mwanaume mwenzako au kumchukia mwanamke huyo? Akiomba msamaha ili muendelee, utamsamehe? Tena pengine akwambie alipitiwa na shetani,je usingegundua angekuwa anapitiwa na malaika?
Nini cha kufanya kwenye hali kama hii?