Kwa hili SUMATRA mnatia aibu

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
Leo jioni hii katika kipindi cha dira ya dunia cha BBC kulikuwa na mjadala kuhusu kuzama kwa meli MV Skagit hapa Tanzania wakati ikitoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar. Walioalikwa ni Said Kubenea, Deo Filikunjombe, Mwakilishi toka Sumatra na Mkurugenzi toka wizara ya mawasiliano Zanzibar.

Kwa masikitiko makubwa kwa mujibu wa muongoza mjadala ambaye ni mtangazaji wa BBC SUMATRA hawakutoa ushirikiano na amewalaum sana.

Katika mjadala huo Bwana Kubenea ameeleza matatizo yaliyopo katika usafiri wa majini hapa Tanzania pamoja na uzembe mkubwa unaofanya na mamlaka husika. Matokeo ya utafiti waliofunya kwa mujibu wa kubenea yako kwenye gazeti la mwanahalisi.

Mheshimiwa Filikunjombe kamlaumu naibu spika kwa kitendo chake cha kukataa kujadiliwa kwa ajali hii bungeni na kailaumu serikali kwa kushindwa kuwa na vyombo vya uokozi mpaka meli inazama katikati ya ikulu ya magogoni na ikulu ya Unguja. Kampongeza sana waziri wa mawasiliano wa Zanzibar na chama cha CUF kuonyesha kujali pamoja na kuwa meli hiyo ilikuwa inatokea Dar ambapo Mwakyembe na CCM ndo walitakiwa kuwajibika. Mwisho kawalaumu watanzania kuwaweka madarakani viongozi wasiokuwa na uwezo wa kuwasaidia.

My take: Upo umuhimu wa SUMATRA na wizara ya mawasiliano Bara kuwajibika.
 
Sumatra Wametumia styre ya Mr Dhaifu ya kukwepa Midaharo kama wakati ule wa Uchaguzi.... Fikiria Watajibu nini wenyewe wapo kwa ajili ya kuongeza % kwenye kila tiketi so hata kama meli inauwezo mdogo kwao ni sawa tu kwani % zao zinakuwa nyingi wanaawana tu... hii Bongo bwana itumie ipasavyo kesho sio yako
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom