Kwa Hili, Sitta Simwelewi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Hili, Sitta Simwelewi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Aug 1, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Aug 1, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wakati wa kumaliza Mkutano wa 20 wa Bunge Wabunge walimlalamikia aliyekuwa Spika wa Bunge hilo Samwel Sitta, kuwa TAKUKURU inawafuatilia majimboni wakati wanatoa misaada ili kutimiza ahadi zao. Baada ya kutaka ufafanuzi toka kwa AG kuwa vijana wa Hoseah waachwe kufanya kazi zao, Sitta aliongeza kusema kuwa misaada ya kutolewa usiku inatia mashaka! Muda si muda mkewe Sitta alidakwa na TAKUKURU usiku guest akiwa na simu kadhaa mpya zikiwa kwenye maboksi yake, fedha taslim zaidi ya 1m/- na bahasha nyingi za kuwekea "vijisenti" hivyo! Hata kama hujaenda shule, akili za kawaida zitakuambia mazingira hayo yanaashiria nini! Cha kushangaza ni pale Sitta anapothibitisha ule usemi "mkuki kwa nguruwe..." kwa kusema eti hataacha "mambo haya yaishe hivi hivi" akiwa na maana kuwa ata-deal na maofisa wa TAKUKURU waliomdaka mkewe! Mimi simwelewi huyu "mpambanaji" wa ufisadi anapokuwa na double standard! Au "upambanaji" wake ulikuwa kuhusu Richmond peke? Au tuseme kuwa vita ya ufisadi inapambanwa "kibinafsi?"
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Huwezi kuyajua maumivu hadi yamekufika! Na pia aliyeshiba hajui maana ya njaa hadi ikimtembelea.

  Hata hivyo siungi mkono huu upuuzi wa TAKUKURU kwa sababu siamini kama kweli wako kazini. Wanatuzuga na kuwavunjia heshima baadhi ya watu. Kwani nani hajatoa zawadi kwenye hizi kampeni zao?
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  MANENO YA SITTA YALIKUWA HAYA

  "Ndugu zangu wabunge kama Mwanasheria alivyotoa ufafanuzi, kwa hiyo nawaambia ndugu zangu kwa nini utoe zawadi usiku wa manane, mbona hii kitu ni rasihi tu we itisha mkutano wako na alika na waandishi wa habari kisha toa zawadi yako"

  sasa hapo anapotetea Bw Sitta sijuhi ni nini? yaleyale ya usiku wa manane ndio hayohayo yametokea kwa mkewe, nadhani swali zuri kwake angemuuliza mkewe alikuwa anafanya nini guest house akiwa na watu wengine pamoja na hizo 1m na simu saba mpya?
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  Mtaanzisha thread ngapi za habari hiyohiyo moja? hebu mods ipeleke hii kunakostahiki.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  All politicians are stupids....
   
 6. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ikiwa Sitta na Mkewe si wafanyabiashara ya bahasha, wala si wanafanyakazi wa posta, wala hapakua na ajenda yeyote muhimu ya vikao kufanyikia chumbani (gesti),

  Na ikiwa Sitta na Mkewe si wafanyabisahara wa simu, wala hawana Shirika lolote lilsilo la kiserikali (NGO) la kutoa huduma kwa wanachini,

  Na Ikiwa Mama Maggie Sitta alikamatwa faragha akiwa na wapambe wa CCM na sio wanachi wa kawaida kwa maana ya wapiga kura wake tu.

  Na Ikiwa hata baada ya kukamatwa, mtuhumiwa amekwisha zungumza kukanusha maelezo kuhusu kukamatwa kwake,

  iweje Samuel aonekane kuwa tena kama msemaji wa Mkewe??, Yeye Samuel alikuwepo eneo la tukio?. Ikiwa yeye ni mtu wa viwango, kwa nini asiache sheria ichukue mkondo wake badala yake asimame kutangaza mapambano kana kwamba mkewe ni pekee aliyehusishwa na tuhuma hizo za rushwa? Wapo wagombea wangapi ambao wamekamatwa na TAKUKURU na hakuna kelele kama hizo za Sitta?.

  Napata shaka na hawa wakuu wetu. Kama ni jambo lililomtia fedheha, aache sheria imshuhulikie mkewe ili baada ya muda ukweli ubainike!.

   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Aug 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu,
  Ni vizuri mkipata uhakika wa habari hii kuliko kuokoteza yanayoandikwa wa vibaraka wa RA. Ikumbukwe tu kwamba Lowassa na RA wako mbioni kuingiza vijana wao ktk uchaguzi wa CCM kumpiku JK ili kuwawezesha kulishika Bunge kama CCM itashinda. Na kikubwa zaidi ni kuhakikisha Mh. Sitta harudi ktk kiti cha Uspika ili wamweke mtu wao tayari kwa kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo tayari harakati za kumsafisha Lowassa zimeanza na anagombea tena Ubunge.

  Na mwisho ifahamike tu kwamba TAKUKURU wanaifanya kazi yao kwa kulinda maslahi ya Lowassa kwani wako chama moja na Hosea, na ndio maana niliuliza kwa nini Takukuru chombo cha dora kinasimamia uchaguzi wa chama kinyume cha majukumu ya chombo hiki kama tulivyofahamishwa awali.

  Upinzani wangu mkubwa na CCM hautokani na JK mwenyewe isipokuwa baada ya kufahamu kwamba kundi la Mkapa kina Mramba na Yona wameunganisha nguvu na kundi la Lowassa/ Rostam kuhakikisha wanachukua bunge na kujiandaa kuchukua tena nchi ifikapo mwaka2015..

  Hivyo wakuu zangu tuwe macho na makini kwa kila move wanayoifanya dhidi yao wenyewe au vyama vya upinzani kwa sababu mustakabali wa nchi yetu unategemea nyie Watanzania wapiga kura mnaelewa kitu gani kinaendelea nyuma ya pazia la sivyo mtauza nchi yenu kwa kura zenu wenyewe pasipo kujitambua.
   
 8. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  Kaka umenena nimeongea sana humu ndani ila watu wanapumbazwa na maneno ya wanasiasa uchwara siku zoote! Huyu mama ninamfahamu si msafi kama mumewe (ambaye simjui vizuri) na kwa tukio hili inadhihirisha kuna untouchables within CCM na hata Sitta mwenyewe si msafi! Angetakiwa akae kimya atafute lawyer then mambo yasuluhishwe mbele ya sheria sio ku-influence mambo through media kama hivi! Hapo ndo nilipochoka! Na ikumbukwe huyu bwana ni majuzi tu alimwaga matrekta ya mikono huko kwake watu wakauliza inakuwaje mpk sasa hayo ndo yanatendeka akadai eti kutimiza ahadi!
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni usanii tu mkubwa, none of them is serious about this!
   
 10. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  nenda zako wewe tena ukome kuita watu ati vibaraka wa EL na RA hapa ndani kuna wanasheria so uache kuua hoja kwa visingizio eti vya wafuasi wa RA na EL wametumwa! wao (EL na RA) wana rushwa zao pia lakini haimaanishi kama RA na EL hawakamatwi basi na Magreth Sitta asikamatwe!
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Aug 1, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Na wewe sikuelewi kama nisivyomwelewa Samwel Sitta!
   
 12. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu umenena, ila nadhani kama vita yenyewe ndio iko hivyo basi elewa kuwa hata kama watashinda kura za maoni bado hao wanaoandaliwa wanaweza pia wasipitishwe na kamati kuu..! (tafadhali rejea ile process ya kumpata mgombea wa ubunge wa CCM).
   
 13. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Je haiwezekani kwamba hizo simu 7 alikuwa anataka kuwapa wapambe wake hili kuweza kuwasilia nao kirahisi wakati huu wa kuchagua wawakilishi wa chama?

  Je haiwezekani hio millioni moja ikawa ni ya gharama za chakula na malazi kwa wapambe wake wakati huu wa kuchagua wawakilishi?


  Sio kwamba naunga mkono rushwa wakuu naipinga sana tatizo kinachonishangaza ni kwamba wengi wanao kamatwa hakuna ushahidi wa kutoa bali tunaambiwa walikuwa wanataka kutoa.kwanini wasi subiriwe mpaka watoe? au ni njama tu zinatumika kuwachafua watu fulani wakati vigogo wenyewe wa rushwa wanaogopewa?
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Aug 1, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010 hata kuwalipa wapambe (ambao pia ni wapiga kura) ni kitendo kilichokatazwa! Haina tofauti na takrima!
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Aug 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu hakuwa na haja ya kwenda huko koote badala ya kujadili hoja iliyopo hapa. Nilichoandika ni ujumbe kwa mtazamo wangu ambao naweza kuutetea ikiwa swali lako litahusiana na maandishi yangu.

  Ebu tujiulize ikiwa habari hii inasema mama Sitta amekamatwa nyumba ya wageni ( Guesthouse) akiwa na kiasi cha millioni moja na simu saba hii kweli inaonyesha kuhusika kwake na takrima au takrima ni wakati mhusika anapokamatwa akitoa vitu hivyo kwa wapiga kura.

  Halafu nambie ni kiasi gani cha fedha kimewekwa mkama sheria ya mgombea kutembea nazo kama gharama ya matumizi yake na wapambe wake pindi anapojinadi jimboni kwake. huwezi kuondoa gharama za chakula namalazi kwa wapambe ati ni takrima hali kazi hiyo lazima iwe na gharama zake.

  Hizo simu saba wagombea wote wanazo zaidi ya hapo kwa kuwasiliana na wapambe wao wanaowanadi ktk kata mbalimbali. Sidhani kama kuna mtu anaweza kumpigia debe kiongozi yeyote ktk uchaguzi huu asihitaji simu za mawasiliano baina yake na makundi ya watu wake wanaotembelea sehemu mbalimbali.

  Jamani millioni moja na simu saba kweli unaweza kuziweka katika hesabu ya takrima au rushwa hali kila mgombea ana kiasi sawa au zaidi ya hicho?.. Kama ni uvunjaji wa sheria, wewe nambie kuna tofauti gani kati ya kuwa na fedha hizo nyumbani kwako au kuwa nazo Guesthouse?..

  Halafu iweje kweli mke wa Sitta, waziri mzima ndiye awe mtu wakuzungumziwa kukamatwa kwake pasipo ushahidi unaojitokeza wazi. Kwa mfano umezungumzia Spika Sitta ktk ugawaji wa matrekta hali ukisahau kwamba serikali imeingiza matrekta kibao na kuyagawa ktk majimbo kulingana na mpango mzima wa Kilimo kwanza, sasa ikiwa wewe una mashaka nautoaji wa Matrekta haya ungeuliza chama cha CCM kwa nini wamefanya haya karibu na Uchaguzi mkuu na wasifikirie kabla au miaka miwili iliyopita!.

  Iweje swala la maendeleo ya taifa kwa sera za CCM zichukuliwe kama ni sifa ya mbunge au hata Takrima hali vifaa hivi vimepelekwa mikoa yote nchini na isihofiwe kwa wabunge wengine waliofikisha pia matrekta majimboni kwao..

  Mkuu wangu sikusema wewe na waandishi wengine hapa JF ni mamluki wa RA na EL isipokuwa nimewaomba mtafute ukweli kwanza kabla ya kudandia treni kwa nyuma pasipo kujua limebeba mzigo gani..
  Ni hayo tu mkuu wangu wala sina maana mbaya isipokjuwa ni kuwatahadhalisha wananchi wapate kuelewa kinachoendelea.
   
 16. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  nenda zako wewe simu zilikuwa mpya ndani ya nylon na hazina chipcard kusema zinatumika na alikutwa guest house usiku na wala hakukutwa na wanafamilia ila makada wa CCM! uende ukalale mzee hizo dalili zote ni harufu ya kifisadi na kwa taarifa yako hawezi kutembea na millioni tano maana anajua TAKURURU wako nyuma kwa hiyo ni mjanja na hizo bahasha lukuki unasemaje?
   
 17. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu sheria inataka uweke wazi utagharamia vipi kampeni yako (malazi ya wapambe, malipo ya posho zao nk..), kwanza wapambe wenyewe wanaoruhusiwa ni wachache. Kama tuhuma ni za kweli, sasa hayo mamilioni yote yalikuwa yanini pia kumbuka alinaswa usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura za maoni!!, kwanini hakuwapa wapambe wake hizo simu na pesa mapema?, na hizo bahasha zilikuwa ngapi??? (i guess zaidi ya namba ya wapambe!!!)..
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Aug 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Swala sii mpya au zimetumika, takrima ni unapokamatwa unatoa hongo kwa wapiga kura. Utalala wewe kwanza maanake Bongo tayari usiku mmelala hali sisi ndio kwanza tunapata chakula cha mchana.

  Kuhusu bahasha lukuki umeambia zina kitu gani na zinakwenda wapi. Kuwa na bahasha lukuki lini imekuwa kuvunja sheria.. Mkuu wangu huwezi kumkamata mtu kwa kukisia ni jambazi simply because umekwenda kwake na kukuta visu kibao jikoni.
   
 19. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Tulitegemea mambo kama hayo yatamtokea Sitta, tena hili dogo. Yetu macho. Kuendesha bunge kwa viwango vile mafisadi hawakuachi ng'ooo! Rushwa hukamatwa kwenye eneo la tukio, sio popote tu. Ati una kitu chako mtu akuhisi unaenda kukitoa rushwa...mmh!
  Sitta na familia yake wategemee vitimbi vya kutosha kwenye uchaguzi huu...CCM ina wenyewe bwana!....sio unatuletea mambo ya haki hapa.....wenye ndio mafisadi...huwezi timuaaa.....Sitta umesikia?
   
 20. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #20
  Aug 2, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Hawa watu wazima hovyo,wao ndio waliokuwa msitari wa mbili kupiga vigelegele na kushangilia pale Raisi aliposaini ile sheria pale magogoni ,sasa nimeamini ya Mh Sophia Simba aliposema CCM hakuna msafi wote ni wachafu kupindukia na hao ndio viongozi wetu watoa rushwa ,nchi inayoongozwa na genge la viongozi watoa rushwa haliwezi hata siku MOJA likawaletea maendeleo wananchi wake kwani wako after Mijitumbo yao AIBU KWAO NA VIZAZI VYAO
   
Loading...