Kwa hili sipati picha... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili sipati picha...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kuku dume, May 6, 2012.

 1. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimehadithiwa soon kwamba babu alikuwa miongoni mwa watu waliochanga vijisenti vyao walivyokuwa navyo ili kumsafirisha Mwalimu kwenda Uingereza kwa Malkia kudai uhuru wa Tanganyika. Nakumbuka kuna bibi mmoja wa miaka 150 huko Hai alimwambia kikwete mwaka 2006 aendelee kukazana kudai uhuru wa Tanganyika. Yaani hakujua kwamba Kikwete ni raisi wa nne. Niliposikia kauli ya bibi huyo nikadhani kasahau. Baadaye ndiyo nikatambua kwamba mzee huyo hakuijua Tanzania Bara kwa kuwa hakushirikishwa katika Muungano; Muungano ambao ulifanikishwa na viongozi waliokuwa na NIA(zao). Sipati picha kama babu angefufuka alafu aambiwe hakuna Tanganyika. Labda angechizika.

  Sipati picha kama angetokea yule aliyetunga wimbo wa taifa Tanganyika huru.

  Naumia sana pale ninapomkumbuka yule aliye design bendera ya Tanganyika. Zaidi ya yote roho yangu inazimia nikimkumbuka yule aliyekazana kuipandisha bendera ya Tanganyika katika kilele cha mlima mrefu wa Afrika.

  Najisikia mwenye uchungu pale gadhabu ya watawala itakapoliangukia lile ziwa la Magharibi lenye lile jina ambalo eti 'halitamkiki'. Wajaleo Waendaleo nasikia kwamba ni mkoa chochezi; eti unakumbushia jina lisilotamkika.
   
 2. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapi mdahalo wa katiba mpya nikatapike maana adhabu yenyewe imepunguzwa hadi miaka mitatu. Nitafungwa lakini nitatoka nikiwa shujaa wa Repablic of Tanganyika
   
Loading...