Kwa hili, nampongeza sana Rais Samia

Kwa hili, nampongeza sana Rais Samia

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
10,959
Reaction score
13,426
Hamjamboni wanangu wana jamvi? Ni muda mrefu watanzania wamekuwa wakisikia viongozi wao wakienda ughaibuni bila kujua walioandamana nao.

Haya mambo ya kuficha waliokuwa au wanaoandamana na viongozi kwenye ziara za nje hasa rais yalianza wakati wa Jakaya Kikwete aliyependa kuzurura huku akijaza watu wasio na sifa wala kuhitajika kwenye msafara wake. ili kufanikisha matumizi haya ya hovyo ya kodi za wananchi maskini wa Tanzania, Kikwete alikuwa akifanya orodha ya waliokuwa wakiandamana naye siri kubwa.

Kuna kipindi alituhumiwa kujaza wana familia yake hata wakwe zake kwenye ziara zake za mara kwa mara. Kitendo cha rais Samia kutoa orodha ya wale atakaoandamana nao kwenda kwenye uapishaji rais HH wa Zambia ni uwazi unaopaswa kupongezwa, kuhimizwa na kuungwa mkono. Kwa vile Rais husafiri kwa kodi zetu, ni vizuri tuwe tunaambiwa wanaoandamana naye.

Kwa hili, hakika na toka moyoni, nampongeza mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. Keep it up and keep it in on.

1629746615293.png
 
Tozo zinaliwa na CCM. Hao wana Sisiemu wanalipwa kwa tozo za maskini wa Tanzania.

Mungu ibariki Afrika, walaani viongozi wake. Warejeshee uhuru wananchi wake.
 
Wana CCM kazi yenu kupongeza tuu
Hata nyie wanaupinzani kazi yenu ni kupinga tu! Si ndio? Utakula ulikopeleka mboga…
 
Back
Top Bottom