Kwa hili, mama umenikosea huruma Mimi mwanao.

Kwa hili, mama umenikosea huruma Mimi mwanao.

Huu ni unaa,
unayajua maumivu ya kuanza upya?
Then jamaa kasema mama anavyo vyanzo vingine kwanini amchukulie kijana wake kila kitu?

Washwahili wanasema "mzazi hamuui mtoto,ila mtoto ndiye humuua mzazi"(funzo,mzazi anatakiwa ajinyime kwa ajili ya mustakabali mzuri wa mtoto wake na siyo kinyume chake!

Kijana;mimi niseme tu "hawa ndo aina ya wazazi na ndugu zetu wa kimaskini/kiafrika tulionao.Usikate tamaa.

Embu angalia hiyo kodi ni kubwa mno,kwanini usiingie kwenye mishe mingine zisizohitaji makodi rukuki kihivyo.Yaani kwa kodi na pango ya hapo unapotaka kuendelea napo ni kubwa kuliko mtaji,jiulize hiyo kodi ukizungusha hata kwa mwaka itakuwa imerudi na faidi juu??
Pia kumbuka ktk kipindi chote utakuwa ukihitaji kula na kuvaa,je haya yote yatawezekana kwa kutegemea biashara hii??

Kuna mdau kasema kama utafanya hiyo,basi ichanganye na mambo mengine ili kuongeza faida.

Kwakuwa tayari uposehemu rasmi na leseni nadhani unazo basi zitumie kuombea mkopo mdogo(kulingana na mahitaji) kisha weka bidhaa mbalimbali zitakazo kuletea faida mapema.
Mkuu nikweli ulicho kisema kuanza upya sio rahisi na sio Kila anae anza upya hufanikiwa kusimama.

Ushauri wako nauchukua ila pia advantage ya pale nikua tayari ofisi inawateja, ntaongea na mzee nimshirikishe juu ya Kodi zinazo nikabili ili anisaidie anapo weza.

Kinacho niumiza ni Kodi tu zilizopo mbele yangu. Pale ofisini mkuu nikiingia kwa sku Nawezaje toka na 15000 Kama sku ikiwa nzuri ila ikiwa mbaya napata at sh 5000 tu ambayo kwa mkoa niliopo inatosha kula kwa sku.
 
Maisha huwa yanaacha kukuumiza pale tu yanapomaliza kukufunza, uzembe ni wako
Uzembe upi nilifanya mkuu.? Umesoma thread yangu ya awali ili upate mkasa mzima.?
 
Mkuu

Pole sana kwa mkasa uliokupata.

Kwanza kubali umeshuka kimapato na amini kuwa,Wewe ni sababu kubwa ya hali uliyonayo.

Kabla ya kuhamishia mpira kwa mtu au hali yeyote,Amini Kuna sehemu ulikosea au umekosea hata unapitia kipindi ulichonacho hivi Sasa.

Wanadam tunatofautiana , Hivyo siku nyingine jifunze kuzungumza hisia zako na yule ambae unadhani anapaswa kujua.

Usiamini yale uliyonayo kichwani na unatamani yatokee Kila mmoja anayajua na atafata vile nafsi yako inavotamani.

Lakini pia jifunze kutoa kwa kadiri ya uwezo,Mzazi ni nguzo muhimu Kwenye maisha.Ila huduma kwake iendane na uwezo ulionao.

Bado hujachelewa,Jifunze kuwa na vipaumbele siku zote katika maamuzi unayofanya.

Chagua,Unataka kurekebisha hisia zako juu ya MAMA,Au kuachana na mawazo juu yake na kutafuta mbinu za kukusaidia kuinuka kiuchumi?

Sisi tutaishia tu kuandika,Ila uzito wa unayopitia ,pasi na shaka weye ndo waujua.

Una nafasi ya kusimama tena mkuu.

Moyo ukiwa na maumivu hautoona mazuri kwa mwingine kwa sababu huwezi toa kitu usichonacho,Mfano huwezi penda kama huoni upendo ndani yako.

Niko tayari kusaidia kwa kutenga muda kuona namna gani utakabiliana na hali unayopitia.

Karibu muda wowote.
Asante sana mkuu kwa ujumbe huu, nakutafuta PM.
 
Kiukweli nimekosa namna, nimekosa jinsi ya kumzuia, wakati namkabidhi nilizuia hisia asigundue Kama sjapendezwa na hili, na ni mama angu sa nitafanyaje.?
Hapo ndipo ulipokosea... pole sana...
 
Dah! Nilitoka nikaenda mikoa ya mbali sana, nilikaa miezi 8 mpaka kurudi mkoa nilio kuwepo. Maana yake nilimuachia dhamana nikiamini ni mama anauchungu na ataipambania ofisi yangu.

Kilicho niumiza ni kiasi alicho chukua wakati anayafahamu yaliyopo mbele yangu.

Pesa haina cha mzazi elewa Hilo.
 
Maisha yenyewe magumu hivi ..kwanini usimuambie yaliyoko moyoni...angalia usijekupata sonona......
 
Una uhakika unanizidi akili wewe? Au kutungaga mariwaya yako marefu yale unajiona unaakili sana sio?

Acha akili za kitoto.

Ninyi ndio Wale wa ooh! Utamkumbuka mama sijui blah blah! Mwenzako anazungumzia pesa na maisha yake wewe unaleta Stori za kitoto Kama mtu asiyekomaa.

Kuhusu kukuzidi akili Hilo achana nalo, ninachokisema hapa ni Akili za kitoto ulizoonyesha.
 
samahani niliandika maneno makali kidogo, kama umeyasoma naomba unisamehe.

Biashara na ndugu hasa sisi waAfrica huwa ni changamoto sana.
Umeshaijua tabia ya mama, sivizuri kuendeleza malumbano naye bali pambane kiume uone unajinasuaje.

Mama, Baba zetu wametuzaa lakinj huwa nao wanakoseaga, cha muhimu kuwa makiji na makosa yao yasikuyumbishe kwenye maisha yao.
 
Acha akili za kitoto.

Ninyi ndio Wale wa ooh! Utamkumbuka mama sijui blah blah! Mwenzako anazungumzia pesa na maisha yake wewe unaleta Stori za kitoto Kama mtu asiyekomaa.

Kuhusu kukuzidi akili Hilo achana nalo, ninachokisema hapa ni Akili za kitoto ulizoonyesha.
Achana na mimi wewe
 
Acha akili za kitoto.

Ninyi ndio Wale wa ooh! Utamkumbuka mama sijui blah blah! Mwenzako anazungumzia pesa na maisha yake wewe unaleta Stori za kitoto Kama mtu asiyekomaa.

Kuhusu kukuzidi akili Hilo achana nalo, ninachokisema hapa ni Akili za kitoto ulizoonyesha.
Kaka watu hivi huwa siwajibu....hana majukumu huyu
 
Kaka watu hivi huwa siwajibu....hana majukumu huyu

Hivi mtu mwenye mke na watoto na majukumu kibao huo muda wa kukumbuka wazazi wake waliokwisha Kufa anaupata wapi?

Labda anazungumzia Vijana wa Chio au wanamuziki wasiokuwa na familia hivyo hawaoni wapi pa kupeleka pesa zao.

Ukishalea vitoto Kwa kuvidekeza haya ndio madhara yake.
 
Back
Top Bottom