Kwa hili la Taasisi ya Moyo, Kikwete anastahili pongezi

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
NI dhahiri kwamba, maradhi ya moyo ambayo ni tishio duniani, yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa kati ya mwaka 1990 hadi 2013 kumekuwa na ongezeko la vifo vinavyotokana na maradhi ya moyo kwa asilimia 41, kutoka watu milioni 12.3 hadi milioni 17.3 ambao hufariki kwa maradhi hayo. Kwa Tanzania, inaelezwa wagonjwa wa maradhi ya moyo wamekuwa wanaongezeka kwa asilimia 26 kwa mwaka.

Nimeanza kwa maelezo hayo nikilenga kumuunga mkono Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kwa kupigania afya za Watanzania kwa kuomba fedha kutoka Serikali ya China mwaka 2007, ili kuweza kujenga Taasisi ya Upasuaji Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambayo tayari imeshaanza kufanya kazi.

Kikwete, baada ya kuona Watanzania wengi wanasumbuliwa na tatizo la moyo, ambalo liliwapasa kwenda kutibiwa nje ya nchi, alithubutu kuomba msaada huo ili kuokoa maisha ya wananchi wake. Ni ukweli usiopingika kuwa maradhi ya moyo yameanza kuwa tatizo kubwa hapa nchini, hivyo hakuna budi kuchukua hatua thabiti ili kukabiliana nayo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, mwaka 2014 watoto wapatao milioni 1.7 walizaliwa, kati ya hao asilimia 0.8 waliokuwa na tatizo la moyo ni sawa na watoto 13,600. Wengine walizaliwa na tundu kwenye moyo, mishipa ya moyo kukaa vibaya pamoja na valvu kubana.

Kutokana na hali hiyo kuwepo, ndipo Rais Kikwete alilazimika kuomba kusaidia kujengewa kituo hicho alipokuwa katika ziara yake ya kikazi nchini China mwaka 2007. Katika ziara hiyo, Kikwete alizungumza na Rais Hu Jintao aliyeridhia kutoa Sh bilioni 16.6 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo, na Serikali ya Tanzania kutoa Sh milioni 10 kwa ajili ya kununua vifaa vingi muhimu.

Lengo kuu lilikuwa ni kupunguza kupeleka wagonjwa nchini India kwa matibabu. Hivi sasa Watanzania tunajivunia kutibiwa magonjwa ya moyo hapa hapa nchini.

Kwa mafanikio haya, tuna kila sababu ya kumshukuru Rais mstaafu Kikwete kwa jitihada na upendo wa dhati kwa wananchi wa Tanzania. Taasisi hii imeleta faraja kubwa kwa Watanzania kwa sababu siku za nyuma wagonjwa 440 walipelekwa India, kati ya hao, 220 walikuwa ni wagonjwa wa moyo.

Kwa idadi hiyo kupelekwa India, ni dhahiri kuwa wagonjwa wengi walibaki nchini wakitaabika na kuteseka kwa maumivu ikiwemo kutoweza kupumua vizuri, kuhema haraka haraka, miguu kuvimba na wengi kupoteza maisha yao mapema kutokana na kuchelewa kupata huduma stahiki.

Lakini uwepo wa taasisi ya JKCI, unatoa fursa kwa Watanzania wote kutibiwa katika taasisi hiyo ya moyo hapa nchini. Binafsi, nimeguswa na ninathubutu kusema `Asante Jakaya Kikwete’ kwa uthubutu na utu dhidi ya Watanzania wenzako kwani kwa kujua mazingira magumu yanayowakabili wagonjwa wa moyo, ulipigana kiume na kuhakikisha unawaachia zawadi ya taasisi ya moyo kabla ya kungatuka madarakani mwishoni mwa mwaka jana.

Hongera Kikwete kwa kuokoa maisha ya Watanzania hapa nchini, kwani kama sio kuona mbali kuhusu ugonjwa wa moyo, Watanzania wangeendelea kuteseka hata kupoteza maisha. Ninawasihi Watanzania wenzangu, kila mmoja amuunge mkono Kikwete katika kuokoa maisha ya raia wa taifa hili, angalau kwa kushiriki katika hatua yoyote muhimu ya kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji mbalimbali.

Aidha, tuiunge mkono taasisi ya JKCI, uongozi wake na watumishi wote ili izidi kushamiri na hivyo kutimiza ndoto za Rais mstaafu Kikwete na Watanzania kwa ujumla kuhakikisha tiba ya moyo inapatikana kwa uhakika nchini
 
Swadakta.

Si hilo la moyo tu, Kikwete kafanya maajabu katika kila nyanja. Hakuna sehemu yoyote utayogusia ambayo Kikwete hajaifanya kwa ubora zaidi kuliko rais yeyote wa kabla yake.

Kikwete tutamkumbuka daima kwa mema mengi aliyoyafanya katika awamu yake na kama hiyo haitoshi basi Kikwete mpaka hivi sasa yupo busy kutengeneza mema kwa Tanzania na dunia kwa ujumla.

Tutakukumbuka sana na tutakuenzi daima kaka Kikwete.
 
mmh...kweli nimeamini kwa sasa mnazunguka mikoani kumkataa the coming chairman Uncle JPM...
 
Swadakta.

Si hilo la moyo tu, Kikwete kafanya maajabu katika kila nyanja. Hakuna sehemu yoyote utayogusia ambayo Kikwete hajaifanya kwa ubora zaidi kuliko rais yeyote wa kabla yake.

Kikwete tutamkumbuka daima kwa mema mengi aliyoyafanya katika awamu yake na kama hiyo haitoshi basi Kikwete mpaka hivi sasa yupo busy kutengeneza mema kwa Tanzania na dunia kwa ujumla.

Tutakukumbuka sana na tutakuenzi daima kaka Kikwete.
Kweli kabisa. Tutamkumbuka kwa yote aliyoyafanya... na yale ambayo hakufanya ila yalimpasa kuyafanya..

Na yale ambayo aliyafanya.. ila haikumpasa kuyafanya.
 
Ningeshangaa kama uzi huu ungepita bila kupiga vigeregere
 
Swadakta.

Si hilo la moyo tu, Kikwete kafanya maajabu katika kila nyanja. Hakuna sehemu yoyote utayogusia ambayo Kikwete hajaifanya kwa ubora zaidi kuliko rais yeyote wa kabla yake.

Kikwete tutamkumbuka daima kwa mema mengi aliyoyafanya katika awamu yake na kama hiyo haitoshi basi Kikwete mpaka hivi sasa yupo busy kutengeneza mema kwa Tanzania na dunia kwa ujumla.

Tutakukumbuka sana na tutakuenzi daima kaka Kikwete.
Ni kweli kabisa , Hakuna asiye na mazuri na Mabaya:
Ili kuepuka Ushabiki hapa tuna sema yafuatayo
(1)Kikwete ana mabaya na mazuri
(2)Magufuli ana mabaya na mazuri
(3)Mkapa ana mabaya na mazuri
(4)CCM ina mabaya na mazuri
(5)Ukawa ina mabaya na mazuri

Tatizo la watu ni kuwa washabiki na labuda na wewe ni mmoja wapo
 
Swadakta.

Si hilo la moyo tu, Kikwete kafanya maajabu katika kila nyanja. Hakuna sehemu yoyote utayogusia ambayo Kikwete hajaifanya kwa ubora zaidi kuliko rais yeyote wa kabla yake.

Kikwete tutamkumbuka daima kwa mema mengi aliyoyafanya katika awamu yake na kama hiyo haitoshi basi Kikwete mpaka hivi sasa yupo busy kutengeneza mema kwa Tanzania na dunia kwa ujumla.

Tutakukumbuka sana na tutakuenzi daima kaka Kikwete.
mimi simpendi JK lakini kwa swala hili nampongeza kwa moyo wote,ameacha legacy kubwa sana.
 
Chadema wanamuita jamaa Fisadi,magufuli analialia kuhusu serikali ya JK...ccm wanamuita Lowassa Fisadi....lakini hawa wote kuna mahali wamefanya kazi.
Hongera JK ....yapo mengi uliyafanya japo lichama unaloliongoza lilizidi wizi...
hata ukimchukua mwendwazimu kutoka mirembe na awe rais miaka kumi lazima atakuwa na kitu cha kuonyesha. kiongozi hata awe mbovu vipi, hawezi kosa cha kuonyesha. tunawapima viongozi kama wamefikia malengo waliyojiwekea na ikiwa wametimiza matarajio ya wananchi.
 
Tuwekee mafanikio ya viongozi wote wa kabla ya Kikwete ili tulinganishe na ya Kikwete tuone ni nani mwendawazimu zaidi.

Ukishindwa kuweka vya kulinganisha basi ujuwe wewe si mwendawazimu bali ni punguani tu unaehororoja na kubwabwaja bila mpango.
 
mimi simpendi JK lakini kwa swala hili nampongeza kwa moyo wote,ameacha legacy kubwa sana.

Hapo hapo Muhimbili ukienda utakuta pamebadilika sana wakati wa Kikwete. Hakuna sehemu haijaboreshwa, kuanzia emergency mpaka vitengo vya kinywa na meno, ni vya kisasa kabisa kwa viwango vyetu.

Bila kusahau chuo kikuu cha tiba, Mloganzila. Ambacho kikimalizika kitakuwa ni chuo kikubwa cha tiba Afrika Mashariki na ya kati kama si Afrika nzima.
 
Kweli kabisa. Tutamkumbuka kwa yote aliyoyafanya... na yale ambayo hakufanya ila yalimpasa kuyafanya..

Na yale ambayo aliyafanya.. ila haikumpasa kuyafanya.

Wacha porojo, mleta mada kaainisha hiyo hospitali ya moyo.

Wewe unakuja kuhororoja na kubwabwaja na ngonjera za eti kafanya, hakufanya. Sijui umesoma shule ipi?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Swadakta.

Si hilo la moyo tu, Kikwete kafanya maajabu katika kila nyanja. Hakuna sehemu yoyote utayogusia ambayo Kikwete hajaifanya kwa ubora zaidi kuliko rais yeyote wa kabla yake.

Kikwete tutamkumbuka daima kwa mema mengi aliyoyafanya katika awamu yake na kama hiyo haitoshi basi Kikwete mpaka hivi sasa yupo busy kutengeneza mema kwa Tanzania na dunia kwa ujumla.

Tutakukumbuka sana na tutakuenzi daima kaka Kikwete.
Naona kagusa kwenyewe.
 
Mi pia nampongeza kwa dhati kwa hilo. Ila alinisikitisha tu kutoingilia kati deni la the late Dr Masau na NHC pale leaders alipokua anatibu kwa operesheni kama zile wanazopelekwa wagonjwa India kutibiwa. Kila mtu anadaiwa ila ni kiasi cha kukaa na kuangalia unajipangaje kulipa.
 
Mtamkumbuka sana maana mmepigwa panga sasa njaa kali sana. Njaa kali sana!! Pumzi itakata soon!!
Swadakta.

Si hilo la moyo tu, Kikwete kafanya maajabu katika kila nyanja. Hakuna sehemu yoyote utayogusia ambayo Kikwete hajaifanya kwa ubora zaidi kuliko rais yeyote wa kabla yake.

Kikwete tutamkumbuka daima kwa mema mengi aliyoyafanya katika awamu yake na kama hiyo haitoshi basi Kikwete mpaka hivi sasa yupo busy kutengeneza mema kwa Tanzania na dunia kwa ujumla.

Tutakukumbuka sana na tutakuenzi daima kaka Kikwete.
 
Swadakta.

Si hilo la moyo tu, Kikwete kafanya maajabu katika kila nyanja. Hakuna sehemu yoyote utayogusia ambayo Kikwete hajaifanya kwa ubora zaidi kuliko rais yeyote wa kabla yake.

Kikwete tutamkumbuka daima kwa mema mengi aliyoyafanya katika awamu yake na kama hiyo haitoshi basi Kikwete mpaka hivi sasa yupo busy kutengeneza mema kwa Tanzania na dunia kwa ujumla.

Tutakukumbuka sana na tutakuenzi daima kaka Kikwete.
Ni kweli yapo mambo mengi mazuri ambayo kikwete ameifanyia nchi hii lakini kusema kila nyanja amefanya kwa ubora kuliko rais yeyote aliyetangulia ni kutia chumvi kupita kiasi.
 
Back
Top Bottom