Kwa hili la panga pangua viongozi Rais Samia atapoteza mvuto kwa Chama na kwa Wananchi

Mimi naona hili nalo linachangia hata kuna kipindi aliwahi kuongea, ukinizingua Zuhura anatoa mkeka! Kama sifa vile. Sasa point ambayo mleta mada anayo kwanini wale wanaotenguliwa wanapewa tena nafasi? Mfano Waziri Kindamba na Edwin Mhede. Kama Mhede alishindwa DART anaweza kwenye Unaibu Katibu Mkuu? Kama Makonda ameshindwa Ukuu wa Mkoa wa Dar na uenezi wa Chama ataweza Ukuu wa Mkoa wa Arusha!!?

Au hizi nafasi watu wanapeana tu!?
Tumechagua kuwa kizazi na kilq kitu Cha hovyo, kiswahili, weledi tumetupa pembeni
 
Toka Rais Samia ameingia madarakani amekuwa na mwendo wa panga pangua nyingi kutoka kwenye Chama hadi kwenye serikali yake, Panga pangua zake amekua akizifanya kwa mantiki ya kufanya maboresho na utendaji kazi lakini hakuna kinacho badilika.

Panga pangua zake nyingine hata masaa 24 hazichukui na sio tu mwaka, hii inaleta tafsiri ya kuwa hana imani na anao wateua, au hashauriwi vizuri au hana misimamo.

Kwenye Chama, Kashabadilisha makatibu wenezi 3, Makatibu wakuu wawili, Na ukiangalia baadhi yake ni zinalalamikiwa au zinatoka kwa aibu na maadili mabovu, na bado anao watengua baadae au hapo hapo anaenda kuwapa nafasi zingine tena kwenye utumishi wa umma, hii inatafsiri gani? Kwenye uongozi wake hakuna uwajibikaji?!? Hawachukuliwi hatua.

Nfani ya Chama Mwenyekiti ataenda kupoteza mvuto na ushawishi, na panga pangua hizi zinaenda kuharibu Chama na kukigawa na kukifanya kionekane cha kawaida zaidi mbele ya macho ya wanachama na wananchi.

Panga pangua Serikalini na vyombo vya ulinzi (Tiss) na mabosi wa mashirika, ambao humo humo mtu anashindwa hapa anapelekwa huku, mara ana shushwa hapa mara ana pandishwa hapa.

Maamuzi ya kuchukua hatua kwa mama ni kubadilishia watu vitengo na sio kuwa wajibisha kwa makosa au maovu wanayofanya, nafasi za teuzi zimekua hazina hadhi tena, zinapoteza mvuto na hii itaenda mpaka juu kwa anae teua ambae ni yeye.

Sitali kuamini washauri wake ndio wanamshauri hivi, Au tuseme wanamshauri kwani yeye hana utashi wa kujiamulia, kwa level yake ya uraisi haoni kama vitu haviendi, hao teuzi zake zina shida, hana njia mbadala au hatua au maamuzi mengine katika kuikuza nchi hii.

Tunaenda kwenye uchaguzi, Chama chake kina poteza ushawishi kwasababu ya yeye anapoteza ushawishi na mvuto kwa wananchi na chama chake.

Hii inaenda kuharibu nchi, Amiri Jeshi mkuu hana misimamo hana maamuzi yaliosimama.. hii ni hatari kwa nchi.
Lakuvunda Halina ubani, ccm ya leo hata akija maraika katikati yao naye bado watamtoboa tobowa kisha watamtaftia sababu na wamfukuze iri tu andiko lao litimie la kila mbuzi naale kwa urefu wa kamba yake

Andiko hilo ndio limehalalisha rushwa wizi fitina husuda na nihatari pia kwa viongozi wazalendo,

leo tunashangaa anguko la makonda
Lakini lipo anguko kuu linakuja hata mnaosherekea leo anguko la makonda wakati huo mtalia pia
 
Toka Rais Samia ameingia madarakani amekuwa na mwendo wa panga pangua nyingi kutoka kwenye Chama hadi kwenye serikali yake, Panga pangua zake amekua akizifanya kwa mantiki ya kufanya maboresho na utendaji kazi lakini hakuna kinacho badilika.

Panga pangua zake nyingine hata masaa 24 hazichukui na sio tu mwaka, hii inaleta tafsiri ya kuwa hana imani na anao wateua, au hashauriwi vizuri au hana misimamo.

Kwenye Chama, Kashabadilisha makatibu wenezi 3, Makatibu wakuu wawili, Na ukiangalia baadhi yake ni zinalalamikiwa au zinatoka kwa aibu na maadili mabovu, na bado anao watengua baadae au hapo hapo anaenda kuwapa nafasi zingine tena kwenye utumishi wa umma, hii inatafsiri gani? Kwenye uongozi wake hakuna uwajibikaji?!? Hawachukuliwi hatua.

Nfani ya Chama Mwenyekiti ataenda kupoteza mvuto na ushawishi, na panga pangua hizi zinaenda kuharibu Chama na kukigawa na kukifanya kionekane cha kawaida zaidi mbele ya macho ya wanachama na wananchi.

Panga pangua Serikalini na vyombo vya ulinzi (Tiss) na mabosi wa mashirika, ambao humo humo mtu anashindwa hapa anapelekwa huku, mara ana shushwa hapa mara ana pandishwa hapa.

Maamuzi ya kuchukua hatua kwa mama ni kubadilishia watu vitengo na sio kuwa wajibisha kwa makosa au maovu wanayofanya, nafasi za teuzi zimekua hazina hadhi tena, zinapoteza mvuto na hii itaenda mpaka juu kwa anae teua ambae ni yeye.

Sitali kuamini washauri wake ndio wanamshauri hivi, Au tuseme wanamshauri kwani yeye hana utashi wa kujiamulia, kwa level yake ya uraisi haoni kama vitu haviendi, hao teuzi zake zina shida, hana njia mbadala au hatua au maamuzi mengine katika kuikuza nchi hii.

Tunaenda kwenye uchaguzi, Chama chake kina poteza ushawishi kwasababu ya yeye anapoteza ushawishi na mvuto kwa wananchi na chama chake.

Hii inaenda kuharibu nchi, Amiri Jeshi mkuu hana misimamo hana maamuzi yaliosimama.. hii ni hatari kwa nchi.
Yeye mwenyewe hajitambui
Umbea na uvivu tu
 
Back
Top Bottom