Kwa hili la panga pangua viongozi Rais Samia atapoteza mvuto kwa Chama na kwa Wananchi

Msifikiri makonda aliposema viongozi wengi ni wanafiki aliropoka tu alimaanisha sana
Mimi niwambia 2025 ccm itakuwana mgombea mwigine kabisa mpaka sasa washauri wanampoteza kisomi wengi watz imani imepungua kwa 95%
Ngoja twaweza waingie kazini mwone
 
Naunga mkono hoja, ila tusimlaumu Maza, sio yeye, yeye anakoseshwa tuu.

Phttps://www.jamiiforums.com/threads/rais-samia-sio-malaika-ni-binadamu-anaweza-kukosea-tusimlaumu-kumshutumu-na-kumponda-kwa-makosa-ya-kukoseshwa-tumvumilie-tumpe-muda.1883239/
P
Inaonekana nyumbani kwako unawalaumu watoto kwa maamuzi yako mabovu.
 
Nakubaliana na wewe P lkn kuna tatizo mahala. Haiwezekani kufanya teuzi kwa majaribio(sumu haionjwi).

kuna kundi fulani linalompotosha kwa manufaa yao.
Lipo ni kundi la wahafidhina wanamuingiza maza chaka, Maza akiisha jaa kwenye 18 yao, 2025 watamtosa!.
P
 
Mama anafanya kazi nzuri sana, na iliyotukuka.

wanainchi wanafurahia matunda ya matokeo ya mipango yake madhubuti sana, katika kuyafikia malengo ya serikali kwa wanainchi, lakini pia kufikia ndoto na matarajio ya wanainchi kwa serikali yao sikivu 🐒
Idd Amini alipokuwa anapanda ndege kukimbilia Libya,

Alitoa vitisho ambavyo wanajeshi wetu wangesikia wote wangekimbiana.

Nakuelewa unachokimaanisha, unaamua kufa na tai shingoni.
 
Nimuda wake na Katiba inamruhusu kufanya hivyo, na washauri wake wamekubaliana, anaona inamsaidia kwenye uongozi wake, mwacheni apambanie muda wake kuongoza nchi si jambo dogo. Si dhani kama ni dhamira yake kufanya mabadiliko kila mara, changamoto inayoonekana hapa ni aina ya watu wanaomzunguka ni tofauti na matarajio yake.
 
Ndio ukweli wenyewe. Mobutu alikuwa akifanya hivyo hivyo.

Unavunja msingi wa civil service unaotegemea merit na utendaji. Unabomoa confidence ya watumishi hata wakiwa bora na makini sana. Kila mmoja wao anaishi na hofu ya kutoswa nje ya ajira wakati wowote. Wote wanajua maslahi yao yako mkononi mwako na utendaji wao si lolote wala chochote. Unawaaminisha wananchi kuwa unafanya hivyo kwa maslahi ya taifa.

Nilishangaa sana JPM alipoanza kufanya hivyo. Hasa pale alipovunja management za serikali za mitaa na kuteua vijana wasio na experience wengi toka UVCCM kuwa wakurugenzi wa halmashauri. Nikakumbuka mambo ya Mobutu na washauri wake.

Sasa kaka, kweli unaona chini ya Uongozi wake kuna anae ogopa!? Huoni wanaotoswa baada ya miezi wana rudi tena, mbaya wanaotoswa ni kwa kashfa lakini wanarudi tena mfano Chongola.

Sidhani kama Mobutu ni mfano mzuri wa mfumo huu, hili linalofanyika liko mbali kabisa na unayo sema.. sioni vikifanana.. maana hao wanaobadilishwa badilishwa hamna kitu wanafanya wanapo toka.. Mfano Mhede au huyo Kindambwa, wamesha kaa nafasi ngapi!?
 
Nimuda wake na Katiba inamruhusu kufanya hivyo, na washauri wake wamekubaliana, anaona inamsaidia kwenye uongozi wake, mwacheni apambanie muda wake kuongoza nchi si jambo dogo. Si dhani kama ni dhamira yake kufanya mabadiliko kila mara, changamoto inayoonekana hapa ni aina ya watu wanaomzunguka ni tofauti na matarajio yake.

Ina maana tutawalaumu walio mzunguka, yeye hana fikra zake?! Hana utashi na fikra zake za kuona kipi ni kibaya kipi ni kizuri! Akiwa kama Rais hana nafasi ya kukataa lililo baya!?
 
Idd Amini alipokuwa anapanda ndege kukimbilia Libya,

Alitoa vitisho ambavyo wanajeshi wetu wangesikia wote wangekimbiana.

Nakuelewa unachokimaanisha, unaamua kufa na tai shingoni.
Hakuna, cha sijui nani alifanya nini, wap na tai...
Kazi lazima ifanyike...🐒

ukweli usemwe bila mbambamba, Comrade Dr SSH ni mahiri na ni madhubut mno katika uongozi wa nchi. hayupo na hakuna wa kumtisha wala kumuyumbisha kwa namna yoyote ile.

waTanzania kwa umoja na kwa maelfu na mamilioni yao, wanamuunga mkono, wanampenda, wanamfurahia nae bila hiana anawapa tabasamu na anawafurahisha kwenye maji,elimu,afya, kilimo, biashara n.k🐒

na uteuzi huu unalenga kuwafurahisha wanainchi zaidi 🐒
 
Lipo ni kundi la wahafidhina wanamuingiza maza chaka, Maza akiisha jaa kwenye 18 yao, 2025 watamtosa!.
P
Sasa kwanini asitafute historia ya hao Wahafidhina kabla ya kufanya teuzi??? Mimi ningemshauri aachane na Uchawa kwani ndiyo unaochangia haya yote.

Hebu fikiria alipomteua Makonda kuwa Mwenezi wa CCM Chawa walimpongeza na kumsifia. Amemtoza kwenye Uenezi Chawa wale wale wamerudi tena kumsifia kwa kumtoza.
 
katika utamaduni wa kujitathimini, kujisahihisha na kuziba mipasuko na kudhibiti nyufa, kurekebisha kasoro na dosari za kiutendaji kwenye chama na serikali.

Chama Cha Mapinduzi chini ya kiongozi madhubuti, shupavu na mahiri sana wa waTanzania, Comrade Dr.Samia Suluhu Hassani, kimeendelea kuimarika na kuaminika zaidi kwa wanainchi, na zaidi sana ccm imeendelea kupendwa sana na kuvutia mamilioni ya wanainchi wapinzani, kuungana na DR.SSH katika kuwaongoza waTanzania, na kuwaletea wanainchi maendeleo ya kiuchumi kijamii na kisiasa kwa usawa na haki, bila kijali rangi ya mtu, dini ya mtu au mrengo wa kisiasa wa mtu.

viva comrade DR.SSH viva...

Kidumu Chama Tawala na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi....
Umempaka mafuta mazuri kwa mgongo wa chupa!
 
Hakuna, cha sijui nani alifanya nini, wap na tai...
Kazi lazima ifanyike...

ukweli usemwe bila mbambamba, Comrade Dr SSH ni mahiri na ni madhubut mno katika uongozi wa nchi. hayupo na hakuna wa kumtisha wala kumuyumbisha kwa namna yoyote ile.

waTanzania kwa umoja na kwa maelfu na mamilioni yao, wanamuunga mkono, wanampenda, wanamfurahia nae bila hiana anawapa tabasamu na anawafurahisha kwenye maji,elimu,afya, kilimo, biashara n.k

na uteuzi huu unalenga kuwafurahisha wanainchi zaidi

Daah wewe jamaa uko vizuri sana.
 
Umempaka mafuta mazuri kwa mgongo wa chupa!
hakuna chupa yoyote hapa wala mgongo wake 🐒

na huu ni mwanzo na haya anayofanya hivi sasa ni kwa uchache tu, japo mengi ni bayana na yanaonekana mchana kweupe 🐒

bila kumuonea mtu haya wala aibu, tutawaeleza waTanzania kinagaubaga mambo muhimu ambayo CCM chini ya Dr.SSH wanafanya kwa maslahi mapana ya waTanzania 🐒

ili hatimae wale wa porojo na stori za sijui nini, nao wakataliwe hadharini kwenye sanduku la kura, Lakini kidemokrasia 🐒
 
hakuna chupa yoyote hapa wala mgongo wake

na huu ni mwanzo na haya anayofanya hivi sasa ni kwa uchache tu, japo mengi ni bayana na yanaonekana mchana kweupe

bila kumuonea mtu haya wala aibu, tutawaeleza waTanzania kinagaubaga mambo muhimu ambayo CCM chini ya Dr.SSH wanafanya kwa maslahi mapana ya waTanzania

ili hatimae wale wa porojo na stori za sijui nini, nao wakataliwe hadharini kwenye sanduku la kura, Lakini kidemokrasia

Unavyo ongea ni unanikumbusha kitabu kimoja cha Lelo Mmasi.. cha Mimi na Rais namna wapambe walivyokua wanamsifia Rais Costa wa Stanza… unajua kusifia ila unasifia kwenye hamna… unasema ukweli wa uongo.
 
Toka Rais Samia ameingia madarakani amekuwa na mwendo wa panga pangua nyingi kutoka kwenye Chama hadi kwenye serikali yake, Panga pangua zake amekua akizifanya kwa mantiki ya kufanya maboresho na utendaji kazi lakini hakuna kinacho badilika.

Panga pangua zake nyingine hata masaa 24 hazichukui na sio tu mwaka, hii inaleta tafsiri ya kuwa hana imani na anao wateua, au hashauriwi vizuri au hana misimamo.

Kwenye Chama, Kashabadilisha makatibu wenezi 3, Makatibu wakuu wawili, Na ukiangalia baadhi yake ni zinalalamikiwa au zinatoka kwa aibu na maadili mabovu, na bado anao watengua baadae au hapo hapo anaenda kuwapa nafasi zingine tena kwenye utumishi wa umma, hii inatafsiri gani? Kwenye uongozi wake hakuna uwajibikaji?!? Hawachukuliwi hatua.

Nfani ya Chama Mwenyekiti ataenda kupoteza mvuto na ushawishi, na panga pangua hizi zinaenda kuharibu Chama na kukigawa na kukifanya kionekane cha kawaida zaidi mbele ya macho ya wanachama na wananchi.

Panga pangua Serikalini na vyombo vya ulinzi (Tiss) na mabosi wa mashirika, ambao humo humo mtu anashindwa hapa anapelekwa huku, mara ana shushwa hapa mara ana pandishwa hapa.

Maamuzi ya kuchukua hatua kwa mama ni kubadilishia watu vitengo na sio kuwa wajibisha kwa makosa au maovu wanayofanya, nafasi za teuzi zimekua hazina hadhi tena, zinapoteza mvuto na hii itaenda mpaka juu kwa anae teua ambae ni yeye.

Sitali kuamini washauri wake ndio wanamshauri hivi, Au tuseme wanamshauri kwani yeye hana utashi wa kujiamulia, kwa level yake ya uraisi haoni kama vitu haviendi, hao teuzi zake zina shida, hana njia mbadala au hatua au maamuzi mengine katika kuikuza nchi hii.

Tunaenda kwenye uchaguzi, Chama chake kina poteza ushawishi kwasababu ya yeye anapoteza ushawishi na mvuto kwa wananchi na chama chake.

Hii inaenda kuharibu nchi, Amiri Jeshi mkuu hana misimamo hana maamuzi yaliosimama.. hii ni hatari kwa nchi.
Kama jpm mliimwita mshamba huyu tumwiteje sasa maan serikali tu ameshindwa kuunda kwa miaka 3 kipi anakiweza kwa sasa
 
Unavyo ongea ni unanikumbusha kitabu kimoja cha Lelo Mmasi.. cha Mimi na Rais namna wapambe walivyokua wanamsifia Rais Costa wa Stanza… unajua kusifia ila unasifia kwenye hamna… unasema ukweli wa uongo.
kama ambavyo Rais asivyobabaika na wakisoaji wake na wale wanamuhujumu kwa makundi...

mimi pia sina mbambamba yeyote na mwenye maoni au mtazamo tofauti na ukweli huu bayana sana, kuhusu jitihada za Rais, comrade SSH katika kuchochea maendeleo kwa kufanya mabadiliko ya uongozi maeneo na sekta mbalimbali humu nchini...

Riwaya, hadidhi na simulizi zibaki tu kama kitu cha kuliwaza au kukupa matumaini au burudani kwako na kwa wengine waonao zipenda,
Acha wengine tusonge kwa style hii 🐒
 
Ccm ilipoteza mvuto toka uchaguzi wa 2010, nguvu ya Dola ndio imebaki mbeleko pekee ya wao kutangazwa washindi kwa shuruti. Kwahiyo si kweli kuwa ccm ipoteza mvuto kutokana na hizi teuzi za rais, Bali ilishapoteza mvuto muda mrefu.
Nakubaliana na wewe sanaa kwenye hili...hawa inabidi watolewe kwa mtu.....
 
Sasa kaka, kweli unaona chini ya Uongozi wake kuna anae ogopa!? Huoni wanaotoswa baada ya miezi wana rudi tena, mbaya wanaotoswa ni kwa kashfa lakini wanarudi tena mfano Chongola.

Sidhani kama Mobutu ni mfano mzuri wa mfumo huu, hili linalofanyika liko mbali kabisa na unayo sema.. sioni vikifanana.. maana hao wanaobadilishwa badilishwa hamna kitu wanafanya wanapo toka.. Mfano Mhede au huyo Kindambwa, wamesha kaa nafasi ngapi!?
Katika mchezo huu wanaotoswa kabisa wapo lakini wachache sana. Lengo kuu la teua, tengua, hamisha ni kuwaaminisha wananchi kuwa Rais anafanya kazi kudhibiti watendaji wake.

Wananchi huamini kuwa utendaji mbovu husababishwa na watendaji. Wrong. Hawa hawana uwezo wa kupitisha maamuzi makubwa - katika nchi hii.
 
Mimi nauliza wanapata saa ngapi muda wa kutumikia wizara zao au nafas zao leohuku kesho kule
 
Back
Top Bottom