KWA HILI LA MV NYERERE ATUTAWAELEWA.

KWA HILI LA MV NYERERE ATUTAWAELEWA.

Kivuko cha Mv.Nyerere kilichozama huko Mwanza jana kinadaiwa kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 100 tu lakini kilizidisha karibu mara nne ya uwezo wake. Kuna "mazwazwa" wameanza kukwepesha lawama kwa serikali na kuanza kuwabebesha mzigo wafanyakazi wa kivuko hicho eti ni kwanini waliruhusu abiria kuzidi.!

Kuna mambo matano ambayo "mazwazwa" hao wanayakwepa ama makusudi au kwa udogo wa akili zao.

#Mosi; Kama abiria walizidi, serikali haiwezi kukwepa lawama. Mamlaka za usimamizi wa safari za majini zilikua wapi? SUMATRA na watu wa bandari waliruhusuje abiria kuzidi kiwango? Na kwa hali inavyoonesha hii si mara ya kwanza kwa kivuko hiki kuzidisha abiria. It seems ni jambo la kawaida. TPA wapo, SUMATRA wapo, Polisi wapo, wote wanaangalia tu. Baada ya maafa ndipo kila mmoja anajaribu kujitoa kwenye lawama.

Kwa vyovyote serikali kupitia mamlaka zake inapaswa kuwajibika. Nilitegemea RPC Mwanza, Mkuu wa kikosi cha zimamoto na uokoaji, Mkuu wa bandari ya Ukara, Meneja wa SUMATRA Mwanza, RC Mongela, DC Ukerewe, Waziri wa uchukuzi wawe wameshajiuzulu kama sehemu ya kuonesha uwajibikaji. Lakini zimebaki porojo za kutupiana lawama tu. At the end dereva wa kivuko hicho na wafanyakazi wale wa ngazi za chini ndio watatolewa mhanga, ili kufunika kombe. What a shame?

#Pili; Pamoja na abiria kujaa lakini kivuko cha Mv.Nyerere kilikua kimeshachakaa sana. Kwa miaka mingi kimekuwa kikilalamikiwa kutokana na uchakavu wake. Na kabla hakijazama, kimewahi kusababisha dhoruba kadhaa kikiwa majini. Mwaka 2016 kilizima katikati ya ziwa na kuanza kwenda mrama (bila uelekeo). Mafundi waliokuwepo kwenye kivuko hicho wakasaidiana kufanya matengenezo kikatengemaa na safari ikaendelea. Hata hivyo hii haikua mara ya kwanza kwa kivuko hicho kuzima katikati ya maji. Imewahi kutokea mara kadhaa na kuripotiwa, lakini nani anayejali?

Mbunge wa Ukerewe Mhe.Joseph Mkundi amewahi kulalamikia mara kadhaa uchakavu wa kivuko hicho na kuomba kifanyiwe marekebisho makubwa au kinunuliwe kingine lakini serikali haikumsikiliza (labda kwa kuwa ni kutoka upinzani). Leo serikali inataka kuondolewa kwenye lawama hizi. How?

#Tatu; Huduma ya uokoaji bado ni ya kiwango cha chini sana. Kivuko kimezama just mita 100 kabla ya kutia nanga, lakini watu wameshindwa kuokolewa. Tangu maafa ya Mv.Bukoba yatokee miaka 22 iliyopita Serikali haijajifunza, wala haijajiandaa kukabiliana na majanga kama haya? Hakuna boti za uokozi, hakuna wazamiaji, hakuna teknolojia ya kisasa za uokoaji, lakini mbaya zaidi hakuna hata taa. Ni aibu na inatia kinyaa. Nchi yenye uhuru miaka karibu 60 inakosa taa za kumulika just mita 100 majini?

Jana serikali ilisimamisha zoezi la uokoaji baada ya kukosa taa. Yani ni kama vile iliruhusu manusura waliokuwa wamesalia ziwani hadi majira ya jioni wafe kwa sababu hakukua na taa za kwenda kuwafuata. Waokoaji wakaruhusiwa kwenda kulala majumbani kwao, huku manusura wakihangaika peke yao ziwani bila msaada wowote na wengine wakipoteza maisha.

Leo serikali imekuja kuokota maiti za watu walewale iliowatelekeza jana kwa kuogopa giza. Halafu kuna watu wanasema ajali ni mipango ya Mungu. Hivi hata kutelekeza manusura ziwani kwa kukosa taa ni mipango ya Mungu? Hivi kukosa hata vikosi vya uokoaji ni mipango ya Mungu? Hivi kukosa vifaa vya kisasa vya uokoaji kama boti na Helcopter ni mipango ya Mungu? Hebu kuweni serious kidogo.!

#Nne; Kwa mujibu wa taarifa ya bunge, kivuko hiki kilikua kinahudumia watu 50,000 wakazi wa Bugolora na Ukara. Uwezo wake ni kubeba tani 25 tu sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja. Lakini mara zote kimekuwa kikizidisha uzito kutokana na demand kubwa ya wasafiri. Hata jana kilipozama kinadaiwa kilikua na abiria karibu 400 na magunia 100 ya mahindi, yani karibu mara 4 ya uwezo wake.

Kichekesho ni kwamba eti serikali inashangaa ilikuaje kivuko hicho kikazidisha watu kiasi hicho. Yani watu 50,000 wanahitaji huduma ya usafiri then mnawapelekea kivuko cha watu 100 halafu mnashangaa kimezidishaje abiria? Kwani hili linahitaji degree ya uchumi kujua demand ilizidi supply?

Mahitaji yanapokua makubwa kuliko huduma lazima mtoa huduma azidiwe. Hili eneo lilikua linahitaji vivuko angalau viwili vyenye uwezo wa kubeba abiria 800 kila kimoja. Lakini mmewapelekea kivuko cha kubeba watu 100 tu halafu mnashangaa kwanini kimezidisha abiria. Hivi mko serious?

#Tano; Yamekuwepo madai ya muda mrefu kuwa serikali inatumia pesa kwenye mambo yasiyo na tija na kuacha mambo ya msingi yanayogusa maisha ya wananchi. Kuna madai ya kushawishi wabunge na madiwani kuhamia CCM katika kile walichokiita "kuunga mkono juhudi" za serikali.

Taarifa ya Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) inaeleza kuwa gharama za kurudia uchaguzi jimbo moja ni Bilioni 1, na udiwani kata moja ni Milioni 30 hadi 45. Hadi sasa kuna wabunge watano waliojiuzulu kuunga mkono juhudi (Kinondoni, Siha, Monduli, Ukonga na Liwale). Hizi ni Bilioni 5 zimepotea kurudia uchaguzi. Na kuna kata zaidi ya 100 zimerudia uchaguzi baada ya madiwani wao kuunga mkono juhudi. Hizi ni bilioni tatu na nusu.

Jumla ya pesa ambazo serikali imetumia kurudia uchaguzi kwa kigezo cha madiwani na wabunge "kuunga mkono juhudi" ni karibu bilioni 9 hadi sasa. Hizi ni zile zilizotolewa moja kwa moja na NEC kwa ajili ya kuchapisha karatasi za kura na kuwalipa wasimamizi wa uchaguzi. Bado hazijajumuishwa gharama za vyama vya Siasa kufanya kampeni.

Bilioni 9 zilizochezewa na NEC kwenye chaguzi za marudio, zingetosha kabisa kununua kivuko kikubwa na cha kisasa kama hiki cha Mv.Kazi (pichani). Hiki kina uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 200 kwa wakati mmoja. Kilinunuliwa kwa shilingi Bilioni 7.5 za kitanzania.

Yani bilioni 9 zilizochezewa kwenye uchaguzi na kuwarudishia ubunge watu walewale waliojiuzulu, zingetosha kununua kivuko kikubwa kama hiki cha Mv.Kazi kikapelekwa Ukara. Kingesaidia kubeba watu wengi zaidi na kuepusha maafa yaliyotokea. Lakini kwa kuwa kupanga ni kuchagua, tuliona watu kuunga mkono juhudi ni jambo la muhimu zaidi kuliko "kusave" maisha ya ndugu zetu wa Ukara na maeneo mengine ya nchi.

Ni kama vile maisha ya watanzania sio muhimu sana kama kuchezea pesa kwenye "zugazuga ya demokrasia" iitwayo marudio ya uchaguzi. Bado tuna safari ndefu sana.!

Tusiweke u-much know sana kwenye hili suala. Hapa Dar kwenyewe Serikali ilitaka kuzuia daladala kusimamisha abiria, uliona ilivyokuwa? Hadi saa 6 usiku watu walikuwa bado wako vituoni hakuna magari huku wengi wakitembea, hivyo wajaruhusu watu kusimama.
Kanda ya Ziwa kuna tatizo kubwa sana la usafiri wa majini ambapo boti nyingi hujaza sana abiria kuliko kawaida.
Ukitaka kuielewa vyema utamaduni wa Kanda ya Ziwa, NASA changamoto za kusongamana kwa abiria, nenda siku za:
  • Mnada (gulio).
  • Kwenda gizani (kutega dagaa).
  • Mtegeruko (kutoka gizani/kutega dagaa).
Hicho ni kipindi ambacho boti, mitumbwi na magari hulalamika sana barabarani kutokana na uhitaji mkubwa wa abiria.
 
Mungu awapunguzie adhabu ya kaburi marehemu wote waliopoteza uhai wao katika janga hili ....... Kwa kweli yaliyotokea yanaumiza sana mioyo ya watanzania hasahasa wale waliopoteza ndugu zao katika ajali kama hizi zilizowahi kutokea hapo nyuma katika MV SPICE, MV BUKOBA na nyinginezo zilizowahi kutokea ambazo ziligharimu maisha ya Watanzania wengi na kusababisha maumivu makali yasiyoweza kutibika kwa kitu chochote kile isipokua faraja ya yeye aliyetuumba. Yaliyotokea yanatufunza mengi sana sisi tulionyuma yao katika masuala mbalimbali hasa serikali iliyoko madarakani toka uhuru maana ni upuuzi wa kiwango cha juu kudharau na kupuuza maoni ya watu mbalimbali juu ya uboreshaji wa huduma zinatumiwa na jamii ya watanzania walio wengi,,serikali imekua kimya katika haya ya msingi na imekuwa bize kushupalia mambo ya kipuuzi hasa chaguzi za marudio ambazo zinagharimu pesa nyingi mabilioni kwa mabilioni ila roho chache za wapiga kura wao hawazijali sababu wao wanaishi kwenye majumba yaliyo na bima, watoto wao wanasoma ulaya, wake zao hawajui tabu za kufata maji kilometa ishirini, ukiwaambia tabu za mama wajawazito hawazijui sababu wao wanajifungulia uingereza, wanasafiria V8 na dreamliner, wanakokaa wao dar wanajijengea fly over ila kwa kina sisi wanyonge vivuko vibovu......MUDA WAO NA MWISHO WA YOTE UTAFIKA TU....NA TUTAONANA PARADISO


MUNGU WAREHEMU MAREHEMU WOTE WALIOPOTEZA UHAI

WAPE NGUVU WALE WOTE WALIOACHWA NA MAREHEMU WAKIWAMO WATOTO WADOGO WALIOACHWA NA WAZAZI WAO

MUNGU USITUSAHAULISHE HILI ILI TUPIGE KELELE KUWAKUMBUSHA WATUBORESHEE JAPO HATA HAYA KWA KUTUMIA KIDOGO WANACHOTUIBIA

MAISHA YETU NI MAGUMU TUNAKOMAA KUJITAFTIA LAKINI TUONEENI HURUMA MTUKUMBUKE KWENYE MADARAJA, VIVUKO NA BARABARA .....
 
Mkuu wa Zimamoto ajiuzuru kwa lipi, Mkuu wa mkoa nae, RPC? Iwapo mfumo tu wenyewe kwa kikosi cha uokoaji jiji la Mwanza hapo zamani ulikuwa ni wa kutegemea vifaa kutoka Tampere Finland, na gari karibu zote za kikosi zilitoka kama msaada leo tunaomba ajiuzuru kwa makosa ya watu wa ngazi ya juu ambao ndio walikuwa na uwezo wa kupitisha maamuzi ya ununuzi wa kivuko cha kisasa...!
Tukiacha ya Ukerewe, hapo Busisi kwenda Kigongo Ferry kuna vivuko viwili ni disaster, kile kidogo na kile MV Sengerema (kama sijakosea) mara nyingi hivi vivuko viwili vimekuwa vikizimika katikati ya maji na kupoteza uelekeo mara kwa mara...! Hapo napo tunasubiri kukamata watu na kuwafunga...!! Nafikiri serikali ione sasa ni wakati muafaka wa kuimarisha kikosi hiki, kwa kutoa mafunzo yanayoendana na mahitaji pamoja na vifaa vya kisasa kulingana na kila mkoa(geographical location) lakini sana leo kikosi cha Zimamoto kimegeuka kitengo cha wakusanya mapato kwenye halmashauri, sijui ni mapato ya moto wanaita(kwenye uokoaji utaishia kupata excuse tu)
 
Back
Top Bottom