Erick zeph Stanley
JF-Expert Member
- Apr 25, 2013
- 647
- 72
Ni siku ya ijumaa serikali kupitia wizara husika ilamua kutoa orodha ya watumishi halali waliohakikiwa na majina Yao kubandikwa katika halmashauri za wilaya wanazofanyia kazi lakini jambo la ajabu ambalo limenifanya niandike uzi huu ni baada ya kupita katika halmashauri ya wilaya moja na kukuta wafanyakazi kibao(zaidi ya 150) wakiwa wamekushanyika nje ya ofisi za halmashauri na nilipojaribu kuwadadisi ndipo waliponieleza kinagaubaga kuwa wapo pale kufuatilia hatma Ya majina Yao kutojumuishwa katika orodha ya wafanyakazi halali ilhali katika orodha ya wafanyakazi wenye vyeti feki majina Yao hayakujumuishwa pia licha ya kwamba vyeti vyao vilihakikiwa .
Hii inadhihirisha madudu yanayofanywa na serikali kupitia wizara yenye dhamana kwani kitendo hicho kinaonesha kuwa serikali kupitia watu waliopewa dhamana hiyo imeshindwa kuonesha umakini katika swala nyeti kama hilo mpaka kutoa orodha inayoivua nguo serikali kwani inaonekana zoezi hili limefanywa na watu wasio makini.
Nipende kuishauri serikali kupitia wizara husika Itoe UFAFANUZI kuhusu jambo hili mapema iwezekanavyo na hatua sitahiki zichukuliwe na kama Kuna uzembe sehemu ulifanyika basi waliohusika na uzembe huo wawajibishwe.
Mwisho wa Kuwasilisha.