endesha
JF-Expert Member
- Dec 9, 2015
- 1,190
- 1,644
Rais John Magufuli amepata heshima ya pekee kualikwa na waziri mkuu wa Uingereza katika mkutano utakaofanyika kuzungumzia mikakati ya mapambano ya rushwa ikiwa ni nchi mbili tu zimepata fursa hiyo kwa bara la Africa ikiwemo pia Nigeria.
Lakini Rais wetu amedai sasahivi amebanwa na majukumu kwahiyo atawakilishwa na Waziri mkuu mh. Kassim Majaliwa
Chanzo: Cloudz Tv
Lakini Rais wetu amedai sasahivi amebanwa na majukumu kwahiyo atawakilishwa na Waziri mkuu mh. Kassim Majaliwa
Chanzo: Cloudz Tv
Kwa sababu yoyote ile lazima tubaki na maswali kadhaa. Kwa nini rais wetu akache fursa ya kukutana taifa kubwa na mfadhili wetu aende kukutana na Mseveni ambaye tangu amechaguliwa amekutana naye mara kadhaa kwenye vikao vya EAC.
Watanzania tunakumbuka alivyokataa kwenda Davos na kumtuma makamu wa rais, tunajua pia kwamba Uingereza amewakilishwa na waziri mkuu. Swali ni je, sherehe za kuapishwa Mseveni na kikao cha kikazi na Cameron ni kipi muhimu?
Hii ilikuwa fursa pia ya kwenda kujaribu kuiosha nchi yetu machoni kwa wafadhili kwa sababu kikao hicho kilikuwa cha kujadili suala la ufisadi. Rais wa Naigeria hata kabla ya kwenda London ameshamtumia ujumbe Cameroon kwamba anataka Uingereza irudishe fedha za mafisadi wa nchi yake walizoficha Uingereza. Magufuli amepoteza fursa hiyo kweli?