Kwa hili La BoT, Usalama wa Taifa Ni Makini

Kwa hili La BoT, Usalama wa Taifa Ni Makini

Miaka yote usalama wa WaPo vizur sana na jambo lolote wanaona na kufikisha sehem husika sema wenye mamlaka ya kuwajibisha NDIOwalikua soft in action ukiangalia yote ambayo jpm anafanya now ni uozo wa awamuzilizopita hawakuwa na usaili wa kuwajibishana ni kulindana tu huyu anajitaidi ingawa bado anatumia sana media zetu kuaminisha umma kwa lengo la kuokoa chama sio kuwapigania wananch kuna mikataba mungu ikulu ipo kimya bado anaangaika na wapishi bank kuu weka wazi mikataba ya madini wawekezaji na vitaru vya uwindaji mkataba wa kusafirisha gass maana kinachofanywa ni kucreate mind set kwa wananchi tu

Umeeleza vema kabisa, kumbuka Makamba naye alisha tujuza awamu iliyopita ilifumbia macho kwa hiyo suala halikuwa usalama wa taifa bali regime.
 
Inawezekana na computer wameshamnyang'anya tayari hawezi kureply..
Ni mwaka wa pili sasa situmii computer..simu yangu inafanya kazi zote mpaka powerpoint naandaa kwa simu!
 
Kinachoniumiza roho ni jinsi watu kwenye idara zote za Kiserikali watakavyokuwa wanalindana, maana wakikuhisi kuwa wewe ndio wale, lazima uundiwe zengwe tu hahahahaaaa
Mkuu kamwe hawawezi kukuhisi hata kidogo. Kama wewe ndio wale wa kujionyesha na sida za kingese sawa.
Moyoni wewe unajua kuwa ni mtoa umbea mkuu wa serikali na sio mtu mwingine.
 
Mkuu kamwe hawawezi kukuhisi hata kidogo. Kama wewe ndio wale wa kujionyesha na sida za kingese sawa.
Moyoni wewe unajua kuwa ni mtoa umbea mkuu wa serikali na sio mtu mwingine.
hahahaaaaaaaa kuna watu wana machale balaaaa
 
TISS ya Tanzania inatumikia ccm sio usalama wa nchi
Wewe unajuaje hayo? Unafahamu sheria iliyounda TISS inasemaje kuhusu wapiga majungu dhidi ya TISS? Nchi zote zina taasisi kama TISS, sasa nyie baadhi yenu kwa nini muiogope TISS? Why? Ni nani alikuambia TISS inatumikia CCM na sio usalama wa nchi? Kwanini mtu ujifiche humu JF na kusema uchuro wa aina hii? Hujui kuwa kwa kuandika humu JF milions of people wanasoma? Sasa kwanini uandike kitu kwa lengo la kudanganya milions of people eti "TISS ya Tanzania inatumikia CCM sio usalama wa nchi?". Pitia sheria ya the Tanzania Intelligence and Security Service Act, 1996. Baada ya hapo ndipo uanze kutoa mawazo yako kuhusu vyombo nyeti kama hivi. Acheni kusemasema ovyo bila mpango.
 
Kwa jinsi mambo yanavyoenda naona usalama wa taifa umerudi kwenye mstari wa umakini na kufanya kazi kwa weledi.

Nimemsikiliza vizuri jana dr JPM huku akiwa ameshikilia orodha ya wafanyakazi wa BOT na cv zao..Aliwaeleza hiyo orodha anayo lakini hakupewa na wao,hilo linaashiria moja kwa moja ni usalama wa taifa wamefanya kazi yao vilivyo..

Miaka ya nyuma usalama wa taifa ilionekana kama imepwaya hivi!siri nyingi za ndani ya serikali zilikuwa zikivuja na hata kwenye issue za msingi bado walionekana kama wamepwaya..zama hizi mpya naona kama wako serious sana na unyeti wa mambo ya kitaifa..

Hili la BOT liwe fundisho kwa halmashauri zetu ambapo mimi naamini ndiko kwenye uozo uliotukuka,usalama uko macho!

Its a matter of time tu,wakurugenzi na waweka hazina wa halmashauri mjiandae kwani usalama unafanya kazi yake ipasavyo!

Kila la kheri usalama wa taifa na hongereni kwa kazi nzuri!
Ni kanuni nyepesi ya maisha, ukifanya kazi kwa bidii na uaminifu mkubwa, ikathaminiwa na kufanyiwa kazi muhusika anapata hamasa n shauku ya kufanya vizuri zaidi; lakini ukifanya kazi; ukawasilisha ripoti ama ikakejeliwa na kutupwa kapuni; unavinjika moyo na kuamua moja wapo; "if you can't fight them, you join them!"
TISS kuna watu wazee kwa vijana waadilifu, weledi na wazalendo kwelikweli, lakini mbele ya Chekacheka; mzee wa mipasho na kejeli wasingefua dafu! Ni jamaa zetu tunaishi nao, wana masikitiko yao mengi kuhusu jinsi mambo yalivyokuwa yanaendeshwa; lakini The buck stops at the presidents door! Mwenye mbwa akitaka mbwa wake awe mkali, atakuwa tu! Big up JPM.
 
Wewe unajuaje hayo? Unafahamu sheria iliyounda TISS inasemaje kuhusu wapiga majungu dhidi ya TISS? Nchi zote zina taasisi kama TISS, sasa nyie baadhi yenu kwa nini muiogope TISS? Why? Ni nani alikuambia TISS inatumikia CCM na sio usalama wa nchi? Kwanini mtu ujifiche humu JF na kusema uchuro wa aina hii? Hujui kuwa kwa kuandika humu JF milions of people wanasoma? Sasa kwanini uandike kitu kwa lengo la kudanganya milions of people eti "TISS ya Tanzania inatumikia CCM sio usalama wa nchi?". Pitia sheria ya the Tanzania Intelligence and Security Service Act, 1996. Baada ya hapo ndipo uanze kutoa mawazo yako kuhusu vyombo nyeti kama hivi. Acheni kusemasema ovyo bila mpango.

Wee wee 1954 wacha hizo; mtu mzima hatishiwi nyau, usitufundishe woga! Mtu Katoa mawazo yake na ni haki yake ya msingi, wewe mwenyewe unajificha nyuma ya jf kujifanya msemaji wa tiss! TISS ni chombo cha umma, hakiko juu ya sheria, wananchi wana haki ya kuhoji mwenendo wake kama unamawaaa! Wageni kama weakleaks na transparent international wakisema mnanywea, akiongea mtanzania unatoa povu!
 
kaka iko wazi hiyooo we unafikiri nani anaweza toa document nyeti namna hiyo amabazo zina mpaka idadi ya pesa inayotakiwa kulipwa kama siyo usalamaa, ? basi umempa wewe
Jamani kweni BOT iko chini ya wizara gani? Na wakaguzi wa hesabu za serekali wako.hakuna Siri yeyote pale BOT.
Muhimu ndugu zetu wa usalama heshima Yao imerudi. Maana ilikuwa kero.
 
Naomba nikazie tu, hili la ajira za kupeana lina gusa watu wengi, ebu katika kila sekta hasa serikalini na kwenye zile authority, ebu ile michato ya ajira ipitiwe kwa kuangalia ninani alifaulu na kama alifaulu alipata hiyo kazi, hapo ndio utagundua 98% waliopata kazi ni wale walioshika nafasi za mwisho katika usaili.
 
Kwani kuna ubaya wa mtu kuwa TISS? Kwanini watu wawe waangalifu na huyo jamaa? Kwanini uigope TISS?
Pengine naye ni jipu huyo. Ila kwa sasa TISS wanafanya kazi zilizotukuka na bahati nzuri zinafanyiwa kazi ilivyo.
 
Mbaya zaidi hata wale walioaminika na kupewa madaraka ya juu wao ndio wa kwanza wa kufanya mambo ya ajabu.
 
Back
Top Bottom