Maramla
JF-Expert Member
- Jan 8, 2014
- 581
- 642
KWA HILI LA BISWALO, CHADEMA TUJITAFAKARI KWA KINA!
Na, Julian Chacha – RORYA
Hivi karibuni kumeibuka utaratibu mpya wa kuitumia CHADEMA kama daraja la kupitisha hoja zenye maslahi binafsi kwa baadhi ya watu. Sisi wanachadema tuanelewa kwanini chama chetu kipo kilipo, hawa wanaojaribu kununua kesi binafsi kisha kuzivika gwanda la chama ionekane ni ajenda ya chama ni wahuni wasiovumilika. Martini Maranja kwa kushirikiana na Didier Mlawa (kigogo2014) ndio wanaoongoza kikundi cha kihuni katika mitandao kutumia mwamvuli wa chama na baadhi ya viongozi wetu wameingia king.
Hivi karibuni imeibuka hoja kuwa CHADEMA imemkataa Jaji Biswalo ambaye awali alikuwa DPP, Hivi sisi tumekosa hoja kiasi cha kufuata upepo wa kila linaloanzishwa na Mlawa katika mitandao? Hivi hatuna ajenda za namna bora ya kujijenga kama chama? Ni jitihada kama CHADEMA ni msingi zilizowezesha chama chetu kujenga mizizi na si stori za kihuni mitandaoni. Tujitafakari sana juu ya kuendesha chama, tujitofautishe na vyama vinavyojali fedha tu na umaarufu wa mitandaoni.
Ikiwa hali hii ya kufuata upepo itaendelea ndani ya CHADEMA, nitashawishi Vijana wa Rorya kuachana na CHADEMA maana haina haja ya kuwa na chama kinachoendeshwa kwa upepo wa siku katika mitandao. Tujiulize tumejipanga vipi na uchaguzi ujao? Tunawezesha vipi Vijana Kujifunza itikadi na sera za chama chetu au sera zetu ni kiki ya mitandaoni tu? Nani asiyejua kuwa CHADEMA haina mamlaka na uteuzi wa majaji? Stori kuwa kuna watu walionewa haimuhusu DPP yeye anafanya kazi kwa maelekezo ya sheria hivyo kumsulubu kwa kutimiza wajibu wake ni uzwazwa wa kiwango cha lami.
CHADEMA tuamke siasa si kupiga soga TL au Facebook. Siasa ni vitendo, tuende katika mitaa kueleza sera na itikadi za chadema badala ya kukaa nyuma ya kibodi tukiongozwa na Didie Mlawa ambaye mwaka jana alimtukana sana Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe kuwa kageuza chama kuwa chanzo chake cha mapato na kuwa Mbowe ni mvunjifu wa katiba kwa uchu wa madaraka. Biswalo ni Jaji sisi sio mamlaka ya uteuzi tujikite katika kazi zetu za msingi ili tuweze kushika dola.