Kwa hili la Ben, CCM wasikose utu

Hizi tabia kuonyesha hadharani chuki dhidi ya upinzani italipeka pabaya Taifa hili.Nani ambaye hatafikiria upande wa pili kwa jinsi ya matamshi na matendo yao?Hata RCwa Dar naye kimya?
 

Ukiihusisha CCM na kupotea kwa Ben Saanane utakuwa unakosea sana na pengine usifanikiwe katika kupata ukweli nani hasa muhusika wa kutoweka kwa Ben. Intelligence Theories hazioneshi kama CCM wana kitu chochote na Ben, Ben hakuwa tishio kwao, si kwa umaarufu wake kisiasa, si kwa uwezo wake wa kujenga hoja, wala si kwa jimbo ambalo angeweza kugombea kwani lina mgombea wa kutoka chama chake.

Uhusiano wa Ben na chama chake ulikuwa wa mashaka sana kiasi Ben kutamka kuwa kuna kitu atakachosema kukihusu chama chake ambacho labda kingeleta mtikisiko. Hiki kilikuwa kipindi cha kuondoka kwa mentor wa Ben, Dr Slaa na kuja kwa mtu ambaye Ben alimuona fisadi na mwizi. Ben alihamanika sana, alipomuuliza dr Slaa cha kufanya. Dr alimjibu afanye kile anachokiamini, afanye for the right course! Ben hakuwahi kukisema hicho kitu na msimamo wake ulieleweka.

Kuteuliwa kwa Ben kuwa msaidizi wa Mbowe kunafikirisha sana. Ben na Mbowe si marafiki, Ben hakuwa mfuasi wa Mbowe alikuwa mfuasi wa Slaa na pasi shaka walikuwa wakiwasiliana.

Lini Ben alichukuliwa na mwenyekiti mwenyewe na kupewa kazi binafsi akitolewa katika zile za kichama na lini tukio limetokea kunaweza kukatupa theories nyingi nyingine.

Mengi yanaweza kuwa possibilities, tuache uchunguzi ufanywe pasipo kunyooshea kidole mtu au kutaka tuhuma ziende upande gani bila kujenga nadharia za kipelelezi na kiuchunguzi zenye hoja.Kwenye vyama vya siasa kuna mengi, wanayoyasema na kutaka tuyasikie kwa nje sivyo ilivyo au sivyo wafanyavyo ndani. Labda kama hutaki ukweli ujulikane na watu waendelee kupumbazika!
 
Hizi tabia kuonyesha hadharani chuki dhidi ya upinzani italipeka pabaya Taifa hili.Nani ambaye hatafikiria upande wa pili kwa jinsi ya matamshi na matendo yao?Hata RCwa Dar naye kimya?
Usijali hao ni watu walio pandikizwa jf na wanalipwa na chama gamba dhidi ya RAIA wema wa tz
 
Kila nikiona taarifa ya Ben,Roho inaumaa.tumbo linauma.na kama kuna mtu anafurahia hilo basi mungu ashughrike nae kadri apendavyo ila si kama nionavyo,Hakuna marefu yasiyo na ncha.
 
Kuna thread imefutwa gafla katuma jamaa anajiita KADA.WA CHADEMA

Duuh kama kweli jinsi alivyo eleza Mbowr,huyo.katibu mkuu na mdada flan wanatakiwa wakahojiwe


Ila nauliza swali huyo ben saanane ni nani??
Alikuwa na.cheo gan zaid??
Simjui naomba.mnifahamishe wakuu
 
Kama humfahamu basi hata madai unayosema kaandika kada wa chadema hayatakua na maana
 
Kukosoa PHD ya Mtukufu ilikuwa kosa kubwa, niliwaza kitakacho mtokea sasa nimekiona. Kama ni vikosi vya madelu au pale lumumba au ticc Mungu ana waona.
 
Ubinadamu umetoweka kati yetu! yaani mapenzi ya vyama yanatufanya tuwe kama wanyama.
Nilishangaa kipindi kile alivyofariki Kapten John Komba na wengine wa CCM jinsi watu walivyokuwa wanashangilia hadharani, hata msiba wa mzee Samweli 6 watu walishangilia bila haya!
 
Kama humfahamu basi hata madai unayosema kaandika kada wa chadema hayatakua na maana
Hivi umesoma alicho.andika au??
Maana kaeleza fact hata humjui mtu kiusalama ni hatua nzur kufwata

Wamedelete sio mda mrefu,binafsi siasa sijui so nilipo soma ndio nikataka kujua nani haswaa huyu jamaaa??

Kwann kapotea??
So ungenijibu ni nani ktk chama.gan ningeunganisha dot
 
ok mkuu nimekuelewa. asante
 
U ukiona watu wanafanya jambo jua kuna sababu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…