Kwa hili JK anastahiki pongezi!

Rebel volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2012
Posts
403
Reaction score
86
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni,mwaka huu mh:Raisi JK kajitahidi sana kuondoa ile kata kata ovyo ya umeme, baada ya vikosi vyake kuanika hadharani uozo uliopo katika shirika la tanesco na kuleta marekebisho.
mnakubaliana nami ama?
 
Una uhakika na unachoandia? au umetumwa uje kutuchimba? nikuulize swali?"

wewe unaweza kukubali kuwa Kiongozi wa nchi changa kama hii ambapo kila siku inalipa kampuni fulani X shilingi milioni 132 kila siku, siku saba kwa wiki, siku 30 kwa mwezi na miezi 12 kwa mwaka, kwa miaka kadhaa na ukae kimya?"

Tunaogopa kusema wazi hadharani tunaogopa kuUlimbokiwa!!
 
Reactions: uto
usiishi kwa woga nchi ya amani hii kama unalako la kuzungumza panda jukwaani utasikilizwa tu,ya nini kutijisha??!!
 
kinachoudhi unataka kuviza hata akili zetu ndogo.Wabadhirifu waliteuliwa na nani?ubadhirifu wa TANESCO ulianza mwaka upi?unafikiri makataba ile miovu ya TANESCO imeshafika mwisho mfano IPTL?SYMBION?
 
ni kweli apewe pongezi maana ameruhusu watu waseme na kuhoji na kufanya mabadiriko pasi ya kuhoji uteuzi aliofanya
hongera JK
 
Ni mapema mno kutoa tathmini ya hali ya TANESCO kabla tuhuma zilizoanikwa hadharani hazijafanyiwa kazi.
 
Uogope au usiogope kulimbokwa kifo kiko pale pale. Kwa hiyo ni afadhali kufa kishujaa kuliko kufa kwa woga na fedheha.
 
Huu ni wajibu wake, sioni haja ya kumpongeza, si ndo miongoni mwa ahadi zake, sasa kwa nini tukae hapa kujadili upuuzi huu badala ya kufanya mambo mengine. Stupid haya ni majukumu ya serikali
 
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni,mwaka huu mh:Raisi JK kajitahidi sana kuondoa ile kata kata ovyo ya umeme,baada ya vikosi vyake kuanika hadharani uozo uliopo katika shirika la tanesco na kuleta marekebisho.
mnakubaliana nami ama?

jk anastahili pongezi la kudhamiria kushusha thamani ya pesa yetu na si pongezi la kuimarisha tanesco.

Yeye ni kama nani apewe pongezi au rabda kwa sababu ya udhaifu wake. wananchi ndoo wanastahili pongezi kujitatulia tatiza la umeme kwasababu wao ndo wadau wakuu na si kikwete!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…