Kwa hili ITV chukueni hatua

Kwa hili ITV chukueni hatua

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,521
Reaction score
96,267
Kitendo cha waandishi wa ITV kuzomewa pale diamond siku ya kuwakabidhi vyeti Magufuri na samia kutoka tume ya taifa ya uchaguzi na kitendo cha kuzomewa mwenyekiti mtendaji wa IPP Dr Mengi ni kitendo cha kuwavunjia heshima na si cha kiungwana kwani kinaondoa heshima kwa wahusika nawashauri kuchukua hatua ya kuwasusia hao.
 
mafuriko yameelekezwa baharini!
Upinzani umefanya makosa mengi ya msingi na wengi wameshaandika haya - kuna kupokea makapi, kuna kuweka mayai yote kapu moja (kuachiana), kuna kushindwa kutangaza sera hata siku ya ufunguzi wa kampeni, kuna kudhulumiana ndani ya ushirika, kuna kutowafikia wananchi wengi vijijini kwa kupenda starehe na misifa ya helikopta, kuna kutokujibu tuhuma nzito dhidi ya afya ya mgombea wao, kuna kutojibu tuhuma kuhusu chama kikuu ndani ya Ukawa kununuliwa, kuna kudharau mpinzani wao mkuu kana kwamba kazeeka au kachoka sana, kuna kudharau umuhimu wa watumbuizaji katika jamii ya kiafrika na kuwaita fiesta, n.k. Makosa ni mengi mno. Ila hii ilitokana na nini? UNYUMBU!

Nyumbu inasadikika ndiye mnyama mwenye IQ (ufahamu) mdogo kuliko wanyama wengi mbugani. Ni mnyama ambaye mwindaji hasumbui akili yake sana japo nyumbu ana maguvu na mapembe makali! Kichwani hamna kitu! Nyumbu hujihami kwa kuotea! Huota kuwa simba au mwindaji mwingine yeyote akija atamla jirani yake na si yeye! Kwa hiyo aendapo nyumbu mwenzie na yeye huenda! Nyumbu mwenzie akipiga kona na yeye hupiga kona! Nyumbu mwenzie akisimama na yeye husimama! Nyumbu mwenzie akiruka na yeyehakawii!

Ndio maana katika lile ajabu mojawapo la dunia litokealo mtoMara kule Serengeti mamba hujilia nyumbu hadi wanakinai! Akitokea nyumbu mmoja akaruka mtoni au akamsukuma mwenzie basi nyumbu wote watarukia mtoni au watasukumana hadi wadumbukie mtoni.

Tabia hii ya nyumbu tumeiona katika kampeni za Ukawa! Wenyewe kwa vinywa vyao tumewasikia wakijinadi ALIPO NA SISI TUPO! Yaani hata akitumbukia mtoni na wao watajiloweka humo! Hata pale ilipokuwa dhahiri kipenzi chao ni mgonjwa taabani tumewasikia wakisema TUTAMPA KURA HUYOHUYO HATA KWA MACHELA TUTAMPELEKA IKULU! Ni unyumbu ulikuwa upo kazini! Ndioo! Nyumbu hawanamuda wa kufikiri hata kidogo! Husukumana na huigana matendo!

Ni katika unyumbu huu watu walishindwa kufanya tafakuri yakina! Hata pale nyumbu mkuu aliposema atawaachia watu waliohukumiwa na mahakama ya juu kabisa nchini kwa makosa mazito kabisa bado nyumbu wadogo walirukaruka kushangilia!Si nyumbu? Hata pale wawindaji walipotuhumu kuwa nyumbu mkubwa nimgonjwa badala ya kuweka mkakati wa kuwaaminisha wapigakura kuwa nyumbu mkuu yuko ngangari wao ndio kwanza wanasema TUNATAKA HUYO HUYO MGONJWA!

Tabia hii ya unyumbu imesababisha anguko kuu nililolitabiri liwe kweli! Hili ni anguko kuu kwa kuwa hakika mwaka 2020 watu watasita kugeuka nyumbu! Bahati mbaya sana barani Afrika ili upinzani uweze kushika dola unyumbu unahitajika.

Kwa kawaida huwa anatokea almaarufu (celebrity) ambaye anatengeneza manyumbu wengi! Huyu Almaarufu akijua kucheza politics of wildbeasts anawashangaza watawala. Akishindwa huwa anatoweka kama alivyochomoza! Ni kwa kuwa kwa bahati mbaya zaidi unyumbu haujirudii! Ukipita umepita.
 
Mi nsaachana na ilo li itv

nipo azam na kingam,uzi ; nimemekitupa kwenye dust bin

m,,.... Zi mku.bwa
 
Ukipenda mwanya hata pale unapoona pengo kwako poa tuu. So si lazima uangalie ITV.
 
Mi nsaachana na ilo li itv

nipo azam na kingam,uzi ; nimemekitupa kwenye dust bin

m,,.... Zi mku.bwa
Sasa king'amuzi gani umekitupa ktk dust bin? Nijuavyo mimi ITV haina king'amuzi, ipo kote kote tu, yaani ulipo ipo! Utajikuta umetupa ving'amuzi vyote!
 
Itv iendelee kuonesha isidingo na tamthilia kwa mahousegirls habari ziko Kwingine
 
Wapuuzi wachache hawawezi kuiondolea heshima ITV na Mengi.
Waungwana tutaendelea kuiangalia na kumheshimu Mengi.

Tulia dozi iwaingie, Lowasa wenu anaenda kuchunga ng'ombe vipi mtamsindikiza?
 
siku hizi nimehamia zangu channel 10, Azam Tv na Star tv
 
Mi nsaachana na ilo li itv

nipo azam na kingam,uzi ; nimemekitupa kwenye dust bin

m,,.... Zi mku.bwa

We inaelekea unafata mkumbo kunanga usichokijua katika hicho kingamuzi cha AZAM, ITV inaonekana vizuri zaidi
 
mafuriko yameelekezwa baharini!
Upinzani umefanya makosa mengi ya msingi na wengi wameshaandika haya - kuna kupokea makapi, kuna kuweka mayai yote kapu moja (kuachiana), kuna kushindwa kutangaza sera hata siku ya ufunguzi wa kampeni, kuna kudhulumiana ndani ya ushirika, kuna kutowafikia wananchi wengi vijijini kwa kupenda starehe na misifa ya helikopta, kuna kutokujibu tuhuma nzito dhidi ya afya ya mgombea wao, kuna kutojibu tuhuma kuhusu chama kikuu ndani ya Ukawa kununuliwa, kuna kudharau mpinzani wao mkuu kana kwamba kazeeka au kachoka sana, kuna kudharau umuhimu wa watumbuizaji katika jamii ya kiafrika na kuwaita fiesta, n.k. Makosa ni mengi mno. Ila hii ilitokana na nini? UNYUMBU!

Nyumbu inasadikika ndiye mnyama mwenye IQ (ufahamu) mdogo kuliko wanyama wengi mbugani. Ni mnyama ambaye mwindaji hasumbui akili yake sana japo nyumbu ana maguvu na mapembe makali! Kichwani hamna kitu! Nyumbu hujihami kwa kuotea! Huota kuwa simba au mwindaji mwingine yeyote akija atamla jirani yake na si yeye! Kwa hiyo aendapo nyumbu mwenzie na yeye huenda! Nyumbu mwenzie akipiga kona na yeye hupiga kona! Nyumbu mwenzie akisimama na yeye husimama! Nyumbu mwenzie akiruka na yeyehakawii!

Ndio maana katika lile ajabu mojawapo la dunia litokealo mtoMara kule Serengeti mamba hujilia nyumbu hadi wanakinai! Akitokea nyumbu mmoja akaruka mtoni au akamsukuma mwenzie basi nyumbu wote watarukia mtoni au watasukumana hadi wadumbukie mtoni.

Tabia hii ya nyumbu tumeiona katika kampeni za Ukawa! Wenyewe kwa vinywa vyao tumewasikia wakijinadi ALIPO NA SISI TUPO! Yaani hata akitumbukia mtoni na wao watajiloweka humo! Hata pale ilipokuwa dhahiri kipenzi chao ni mgonjwa taabani tumewasikia wakisema TUTAMPA KURA HUYOHUYO HATA KWA MACHELA TUTAMPELEKA IKULU! Ni unyumbu ulikuwa upo kazini! Ndioo! Nyumbu hawanamuda wa kufikiri hata kidogo! Husukumana na huigana matendo!

Ni katika unyumbu huu watu walishindwa kufanya tafakuri yakina! Hata pale nyumbu mkuu aliposema atawaachia watu waliohukumiwa na mahakama ya juu kabisa nchini kwa makosa mazito kabisa bado nyumbu wadogo walirukaruka kushangilia!Si nyumbu? Hata pale wawindaji walipotuhumu kuwa nyumbu mkubwa nimgonjwa badala ya kuweka mkakati wa kuwaaminisha wapigakura kuwa nyumbu mkuu yuko ngangari wao ndio kwanza wanasema TUNATAKA HUYO HUYO MGONJWA!

Tabia hii ya unyumbu imesababisha anguko kuu nililolitabiri liwe kweli! Hili ni anguko kuu kwa kuwa hakika mwaka 2020 watu watasita kugeuka nyumbu! Bahati mbaya sana barani Afrika ili upinzani uweze kushika dola unyumbu unahitajika.

Kwa kawaida huwa anatokea almaarufu (celebrity) ambaye anatengeneza manyumbu wengi! Huyu Almaarufu akijua kucheza politics of wildbeasts anawashangaza watawala. Akishindwa huwa anatoweka kama alivyochomoza! Ni kwa kuwa kwa bahati mbaya zaidi unyumbu haujirudii! Ukipita umepita.

Kilaza mkuu wa vilaza wote ndani ya nchi hii
 
We inaelekea unafata mkumbo kunanga usichokijua katika hicho kingamuzi cha AZAM, ITV inaonekana vizuri zaidi

Mkuu ukisikia manyumbu ndio hao kufuata mkumbo
 
Back
Top Bottom