Bornvilla
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 924
- 272
Watu wanamiminika Loliondo,tamko kwa waislam msiende huko,kakobe hiyo ni deci,askofu mpemba loliondo ni uchawi,wengine mbona shekhe yahaya? Nianze na waislam.Waislam mtume na nabii wa mwisho ni Muhammad(s.a.w) hivyo hakuna ndoto wala ujumbe zaidi ya maandiko matakatifu yaliyoachwa. Ili kuwa mtume na nabii utapata ndoto za kweli na pia kutokewa na kuletewa ujumbe na malaika Gabriel(Jibrili). Kwakuwa utume na unabii ulishafungwa wote wanaokuja kwa staili hiyo hao ni wafuasi wa shetani,na mashetani ndio wanaowaletea ndoto hizo. Wengi tu wameoteshwa ndoto na mashetani na waliyoota yakatokea.Kuhusu Shekhe Yahaya anayofanya kwa mujibu wa uislam anayofanya ni kazi ya shetani na ni ushirikina ambao umepigwa vita na uislam.Anatumia elimu yake kupotosha uislam na kufundisha uchawi,ambapo Qur'an inasema wazi kuwa watu wanamna hiyo watatumikia motoni milele. Kwa upande wa loliondo kwa waislam hiyo ni haramu.Kwa wakristo hivi sasa kumezuka wimbi kubwa sana la manabii wa uongo na wachawi wakubwa.Madhehebu safi sasa za kikristo zinahesabika.Mfano ni hapa jijini Mwanza ambapo manabii wauongo wametia nanga sasa wanahaha baada ya kufichuliwa kwa shuhuda nyingi zinazotolewa kwaneema fm.Mengi niwaachie wachangiaji kwani ndio wanaojua mengi zaidi,na itatusaidia sisi wote kujifunza,kwani lengo kuu ni kuupata ule ufalme wa mbinguni.Haya na tuongozane.