Kwa hili, Dr. Slaa wewe ni 'Mdini' pia!

Status
Not open for further replies.

KIBE

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
943
Reaction score
186
Katika gazeti la Tanzania Daima la tarehe 13/05/2015 limetoka na kichwa kikubwa cha habari "Slaa amlipua JK, Asema amemwaga sumu ya udini misikitini"

Kwanza kabla ya yote ukweli ulio wazi gazeti la Tanzania Daima ndio gazeti ambalo kwa sasa linaongeza mpasuko katika nchi yetu kwa kutokufuata maadili ya kazi na kutoangalia taarifa zipi za kuandika na zipi si za kuandika. Wanatoa taarifa kwa sababu tu kasema kiongozi na boss wa gazeti lao. Taarifa nyingi za Tanzania Daima ni za kueneza chuki baina ya watanzania. Mhariri wa gazeti hili, nchi ikichafuka hutamuona Mbowe wala Slaa ila ndugu zako ndio watakaotaabika kwa shida na mateso.

Pili, Dr. Slaa unaposema JK ni mdini, vyema ukajiangalia na wewe mwenye usafi wa roho yako katika hili. Mimi nakumbuka mwaka 2010 kwenye uchaguzi kwa macho na masikio yangu wewe ulitumia Kanisa kuombe kura na Maaskofu wengi wakiwa kina Pengo na wengine walikuwa mstari wa mbele kukupigia kampeni na kutoa waraka kibao kuonyesha wewe Dr. Slaa uchaguliwe ndio chaguo la wakristo. Na wewe ulipitakwa viongozi wa makanisa kawaomba wakuaidia kwa waamini wao wakuchague mkristo mwenzao.

Dr. Slaa leo unaongea hayo kuwa JK ni mdini, hizo ni chuki binafsi na sababu kubwa ni kushindwa katika uchaguzi.

Swali: Je, wewe ungeshinda uchaguzi 2010 kwa kura za wakristo ulizoomba, vipi leo ungesemaje?

Nawashukur watanzania hasa wenye akili timamu wasio wajinga kama wale wanaoshabikia udini waliliona hilo na wakaacha kukuchagua.

Wito wangu kwa watanzania na hasa vyombo vya habari kama Tanzania Daima: Turudi nyuma tuwe wazalendo kwa kuacha kutumika kueneza jambo ambalo kila mtanzania analichukia kwa sababu mwisho wake ni mbaya sana, maana udini kwa sasa imekuwa kama agenda ya kupandisha chati baadhi ya vyama vya siasa.

Nchi ikianguka hii hakuna atakayepona hasa sisi maskini... Hawa kina Dr. Slaa na Mbowe wana fedha watahamia nchi nyingine.

============================
Habari kamili, 'Slaa amlipua JK
============================

 
Hiyo ni sera ya CHADEMA kwani uongozi wao wa nyanda za juu kusin ni wakiaskofu kwa hyo upo sahihi mbna cjackia sheikh fulan?mtasema hawajasoma maaskofu ndo wamesoma eti?to hel with ur cdm dr slaa acha kuja kuombaomba mbeya nenda mosh
 
Kwanza hakuna ubishi kwamba Dk Slaa ni mdini kama alivyo mtu mwingine kwa sababu amewahi kutumikia dini kwa ahadi kabla hajaamua kusaliti na kurudi uraiani nadhani kwa lengo la kuwatumikisha.

Pili, hakuna ubishi kwamba gazeti la Tanzania daima ni kampeni meneja wa CHADEMA na tatu hakuma ubishi kwamba kuna wimbi kubwa la masuala ya udini.

Ushauri wangu:
Kama kweli hawa viongozi wanataka kututawala na kuongoza nchi hii waache huu ujinga wa kupandikiza udini miongoni mwa watanzania.
 
Hilo gazeti la kufungia vitumbua na maandazi lisipofungiwa sasa litakuja kusababisha machafuko katika nchi yetu.
Ni vyema Serikali ikaliona hili mapema.
 
ukweli unauma lengo lako kubwa unataka magamba walifungie tanzania daima kama walivyofanya mwanawetu kipenzi mwanahalisi looh!
 
Hebu tuwekee waraka halafu utuonyeshe mahali palipoandikwa CHADEMA au Dr Slaa !!
 
Awe Raisi, mzazi wangu, kub akiongelea udini au flani mdini mi huwa namuona mjinga tuu.
Swala lishajadiliwa huu ni wakati wa kutoa tofauti mtu anakuja kusema tena flani ni mdini si ujinga huu.
 
Eti kwa macho na masikio yako ulishuhudia slaa akiomba kura kupitia maaskofu!?!

Tumwogope Mungu jaman!!
Hivi ule waraka uliotolewa na maaskofu uliwahi kuusoma?!

Nakumbuka mwanahalisi wali'compare na ku'contrast nyaraka hizi zilizotolewa na viongozi wa dini! Sidhani kama ulipata nafasi ya kupitia hilo gazeti.

Tusiandike vitu kwa sababu tu tunaingiza elfu saba!!
 
WEWE NI MZALENDO KWA UDINI HUU? TANZANIA DAIMA UNAOWATUHUMU KUWA NI WABAYA, mbona wewe umeleta utumbo uleule?

Hii ni safu ya wachangiaji haya ona sasa wachangiaji wanakuja kwa misingi ya dini!!!!........

Hoja zenu hizi si za kisiasa ni za dini.
 
WABHEJASANA

Kaka unaposem dr slaa ni mdini kwani yeye ni serikali. Tuache ushabiki ili titatue maswla haya mazito yanayolikabli taifa kutokana na udhaifu wa serikali iliyopo madarakani.

Serikali ituambie imetekeleza lipi kati ya yaliyotokea kuhusiana na migogoro ya kidini zaidi ya kuonesha sinema kwenye runinga ya watu wanaohusika lkn hatuon kinachoendelea.

Kwa pamoja tuitake serikali kuchukua hatua kwa wakati na si kudanganya kwani kipindi cha kuwadanganya wa Tanzania kimepita.
 
Last edited by a moderator:
Wagawe uwatawale na wahenga wanena Nyani haoni kundele.
Udini/mdini ni mtaji siku hizi zamani ilikuwa kimyakimya ila zama hizi waziwazi.
Tutaona mengi hadi 2015 ccm wakiingia tena magogoni wengine wakiendeleza majungu yao.
 
Nchi zinazo ongongozwa kwa mfumo wa kidini duniani ni za Kislam tu, hizo ambazo ni za Kikrsito wala hata hayo maadili ya Kikristo sio lazima kiongozi awe nayo, nchi pia zinazo ongozwa kwa Kislam ndizo zinazoongoza kwa machafuko, kwa ufupi, huwezi kutofautisha fujo, chuki na mauaji na Uislam.

Hivi Al Asad si ni mwislam na nini anawafanya Waislamu wenzie? jumuia ya kimatifa kama Marekani ndizo ambazo zinajaribu kumshawishi Al Asad aache kufanya mauaji ya kikatili, mbaya zaidi Iran, nchi ambayo ndio mfano bora kwa Waislam duniani, ina support mauaji anayoyafanya Al Asad, narudia, huwezi kutofautisha chuki, fujo, mauaji na Uislam!
 
Mie sipati picha CCM wanasema Chadema wadini wana UKRISTO na Chadema wanasema Kikwete ni mdini anawapendelea Waislaam sasa hizi pande zote mbili wanataka Waislam na Wakristo wazidi kuchukiana?

Unaposema Kikwete mdini anapendelea Waislaam unatuma ujumbe gani kwa waumini wa madhehebu ya Kikristo?Je na waumini wa Kiislaam nao wataupokeaje ujumbe wako unaosema huyo Rais wa madhehebu yenu wanawapendelea?

Kwa sasa tujue hizi choko choko za Dini zinaletwa na wanasiasa wala sio wauminu wenyewe sijui nchi inaelekea wapi!!
 
Dr Slaa bora ungekaa kimya kuliko kuendelea kujidhalilisha na kauli zako.

Ueleweki mara useme ulishinda uchaguzi usalama wa taifa wakaiba kura.

Kwa kukusaidia tu JK toka aingie madarakani misikiti anayokwenda ni ya Bakwata ambayo haina waumini wengi.

Huwezi kumkuta JK kwenye misikiti mikubwa hapa Dar kama Kichangani, Mtambani, Idrisa, Mtoro.

Labda tuambie misikiti gani alikuwa anafanya udini, halafu una uhakika gani kuwa Waislam wote walimpigia JK.
 
Mmebugi; mnaambiwa ukweli na Dr. Slaa halafu mnaweke thread ya udini, sasa mdini nani?
 
Tatizo huwa tuna BWETEKA na kila moja hupenda dini yake..hiyo ni haki yako.. Lakini kuna TAIFA na uzalendo kwanza.
Masilahi ya nchi yako iwe mbele baadaye hayo mengine kama yana ulazima yatafuata.
 
WEWE NI MZALENDO KWA UDINI HUU? TANZANIA DAIMA UNAOWATUHUMU KUWA NI WABAYA, mbona wewe umeleta utumbo uleule?

Hii ni safu ya wachangiaji haya ona sasa wachangiaji wanakuja kwa misingi ya dini!!!!........

Hoja zenu hizi si za kisiasa ni za dini.

mkuu, unalitetea sana gazeti la Tanzania Daima na Dr Slaa wakati wanahamasisha mpasuko katika hilo. Dr slaa ni mchochezi wa udini na anajua huo ndo mtaji wao. wanatumia vibaya zile takwimu za uongo kuwa wakristo ni wengi kuliko waislam. anajua kuwa akitumia gia ya udini atashinda. huo ni ujinga wa kutisha na mtu kama huyu akemewe kwa nguvu zote
 
Udini uko Ccm na ndiyo waasisi wa huo udini.Hebu tafakari mtiririko huu ni udini mtupu ndio uliyotumika hapa.Raisi wa kwanza wa Tz ni Nyerere dini yake mkristo.Raisi wa pili ni Mwinyi dini yake muislam.Rais wa tatu ni Mkapa dini yake ni mkristo.Rais wa nne ni Kikwete dini yake muislam.Awamu inayofuata kwa mtiririko wa Ccm ni ya mkristo.Kwa hali hii Ccm wanakataa vipi kuwa wao siyo wadini?.
 
Kama kweli Dr. Slaa amesema hivyo basi atakuwa hajafanya busara, tunajua umuhimu wa upinzani.
Ila kwa hili la fukuto na viashia vya udini, viongozi wote wa kisiasa wanatakiwa kuwa sehemu ya suluhisho,

Watanzania nawaombeni kwa nyakati tulizopo na kwa jambo hili tujaribu kuwa sehemu ya suluhu, tutoe mawazo yatakosaidia taifa lijiponye na jini huyu mbaya wa udini.

Maslahi ya nchi kwanza
Wenu Mpenda Nchi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…