Kwa hii kashfa ya Mbowe kugeuza CHADEMA kuwa kichaka cha Mafisadi, anapaswa kujiuzulu

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Siku zote viongozi na wafuasi wa upinzani wamekuwa wakipiga kelele sana kunapojitokeza tuhuma za ufisadi hasa kwa upande wa serikali na chama tawala. Siku zote wapinzani wamekuwa wakijiona wao ni malaika kwamba ni wasafi na hawakosei.

Ila ukiangalia kwa jicho angavu, viongozi wa upinzani ni wasanii, wababaishaji na wapiga deal kimya kimya. Mpaka sasa, sioni uhalali wa Freeman Mbowe kusimama hadharani na kuinyooshea kidole serikali katika kashfa za ufisadi ambazo hazipo wazi ilhali yeye ndiye anawakumbatia mafisadi na amekuwa akiwapa madaraka makubwa makubwa ndani ya CHADEMA.

Alianza na Lowasa ambaye amesemwa kwa zaidi ya miaka 8 kuwa ni fisadi. Ufisadi wa Lowasa si wa kificho na ndio uliomng'oa kwenye nafasi ya Uwaziri Mkuu mwaka 2008. Tangu wakati huo, Lowasa amekuwa akisemwa ama kuhusishwa kwenye matukio kadhaa ya ufisadi na Freeman Mbowe na Timu yake walitumia nafasi hiyo kuueleza umma juu ya ufisadi wa Lowasa. Kwa mtu mwenye akili timamu, aibu na dhamira njema ya kupambana na Ufisadi kivitendo, asingetegemea kuona Mbowe huyu huyu anasimama hadharani na kumtambulisha Lowasa kuwa ni mwanachama wa CHADEMA na kumpa dhamana kubwa ya kumteua kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya chama chake na UKAWA. Hii ni aibu kubwa ambayo ni lazima Freeman Mbowe abebe dhamana.

Hata kabla kelele za kukemea uamuzi wa Mbowe kumpendekeza Fisadi Lowasa kuwa mgombea Urais hali iliyochangia anguko KUU la chama hicho na upinzani kwa ujumla hazijaisha, Freeman Mbowe huyu huyu anafanya maamuzi mengine ya GIZANI na ya aibu ya kumteua Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA licha ya mwanasiasa huyo kuhusika kwenye kashfa kadhaa ikiwemo kuuza nyumba za serikali na uuzwaji wa maeneo wazi (open space). Nafahamu kuwa CHADEMA hawana watu wenye maono kuongoza chama chao na ndo maana wanaokoteza tu hata makapi yaliyoachwa na CCM. Nafahamu kuwa mkakati wa Mbowe ni kuhakikisha kuwa Sumaye ndiye anapeperusha bendera ya CHADEMA kwenye uchaguzi Mkuu wa 2020. Ila kwa kashfa hii hakika Mbowe amepotoka

Hata hivyo, ni vema wana CHADEMA na Watanzania kwa ujumla wakajiuliza, i wapi dhamira ya dhati ya Mbowe na chama chake kupambana na ufisadi na mafisadi? Inakuwaje mafisadi sasa wameifanya CHADEMA kuwa ni maficho yao na wamekuwa wakipata good shelter? Huu ujasiri wa Mbowe kuwakumbatia mafisadi na kuwapa vyeo anaupata wapi licha ya wafuasi wa chama hicho kupiga kelele ya kupinga maamuzi hayo na yeye amekuwa KIZIWI na KIPOFU?

Kwa haya makosa ambayo Mbowe amefanya kwa kudhamiria, amepoteza hadhi ya kuwa kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Mbowe pia amepoteza hadhi ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na kwa hali hiyo anapaswa kuachia ngazi mara moja ili kulinda hadhi ya upinzani na chama chake.
 
Wenyewe wanasema siasa za utumishi sio muhimu la msingi ni kupambana kuongeza ruzuku.Mambo ya kupinga ufisadi na Mzee Mangula na kamati yake ya maadili CCM ndio apambane na ufisadi.Katibu mkuu ameanza kutumbua hela za ruzuku yupo Ghana.
 
umaarufu wa magu unashuka kwa kas sana kila siku badala ya kuimalisha chama chako na kumfanya magu aendekee kung'ara kama miez minne ya mwanzo unapambana na chadema akifikisha mwaka hoi kabisa maana aaiv hajulikani tena kasimamia wap kishapoteza direction.
 
Wanasema mhimili wa Bunge umepokwa nguvu, wamesahau kuwa wamewapoka wananchi nguvu ya kuwamini kuwa ni wapiga vita ufisadi.
 
umaarufu wa magu unashuka kwa kas sana kila siku badala ya kuimalisha chama chako na kumfanya magu aendekee kung'ara kama miez minne ya mwanzo unapambana na chadema akifikisha mwaka hoi kabisa maana aaiv hajulikani tena kasimamia wap kishapoteza direction.
Umaarufu wa magu upo na unazidi kuimarika. Ndo maana mnammiss Kikwete
 
Wenyewe wanasema siasa za utumishi sio muhimu la msingi ni kupambana kuongeza ruzuku.Mambo ya kupinga ufisadi na Mzee Mangula na kamati yake ya maadili CCM ndio apambane na ufisadi.Katibu mkuu ameanza kutumbua hela za ruzuku yupo Ghana.

KAMA CCM HAWATETEI WEZI KWA NINI KURASA 34 ZIMEKIMBIWA NA WABUNGE 250?

Ila upende flan kuficha bunge waliona mbali serikali ina miez 6 hebu fikiria unakutana na nondo za lema si mapema sana mngevuliwa nguo na kuonekana hamna maana acha kwanza wapate ka experience.
 
umaarufu wa magu unashuka kwa kas sana kila siku badala ya kuimalisha chama chako na kumfanya magu aendekee kung'ara kama miez minne ya mwanzo unapambana na chadema akifikisha mwaka hoi kabisa maana aaiv hajulikani tena kasimamia wap kishapoteza direction.
Magufuli hahitaji umaarufu, yuko kikazi zaidi, nyie endeleeni kutapatapa na nyumba za serikali zilizouzwa na Sumaye(Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema)
 
KAMA CCM HAWATETEI WEZI KWA NINI KURASA 34 ZIMEKIMBIWA NA WABUNGE 250?

Ila upende flan kuficha bunge waliona mbali serikali ina miez 6 hebu fikiria unakutana na nondo za lema si mapema sana mngevuliwa nguo na kuonekana hamna maana acha kwanza wapate ka experience.
CCM wangekuwa wanatetea wezi JIZI LOWASSA lingekuwa rais.
 
Magufuli hahitaji umaarufu, yuko kikazi zaidi, nyie endeleeni kutapatapa na nyumba za serikali zilizouzwa na Sumaye(Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema)

saiv hahitaji tena media kufanya ziara za ghafla maofisini kwisha habari zake ndembe ndembe

mi sijazungumzia habari zaaa......

endeleeni kutapatapa na nyumba za serikali zilizouzwa na Sumaye(Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema)

HUO WASWAS WAKO UNATAFUTA KICHAKA CHA KUJIFICHIA.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Siku zote viongozi na wafuasi wa upinzani wamekuwa wakipiga kelele sana kunapojitokeza tuhuma za ufisadi hasa kwa upande wa serikali na chama tawala. Siku zote wapinzani wamekuwa wakijiona wao ni malaika kwamba ni wasafi na hawakosei.

Ila ukiangalia kwa jicho angavu, viongozi wa upinzani ni wasanii, wababaishaji na wapiga deal kimya kimya. Mpaka sasa, sioni uhalali wa Freeman Mbowe kusimama hadharani na kuinyooshea kidole serikali katika kashfa za ufisadi ambazo hazipo wazi ilhali yeye ndiye anawakumbatia mafisadi na amekuwa akiwapa madaraka makubwa makubwa ndani ya CHADEMA.

Alianza na Lowasa ambaye amesemwa kwa zaidi ya miaka 8 kuwa ni fisadi. Ufisadi wa Lowasa si wa kificho na ndio uliomng'oa kwenye nafasi ya Uwaziri Mkuu mwaka 2008. Tangu wakati huo, Lowasa amekuwa akisemwa ama kuhusishwa kwenye matukio kadhaa ya ufisadi na Freeman Mbowe na Timu yake walitumia nafasi hiyo kuueleza umma juu ya ufisadi wa Lowasa. Kwa mtu mwenye akili timamu, aibu na dhamira njema ya kupambana na Ufisadi kivitendo, asingetegemea kuona Mbowe huyu huyu anasimama hadharani na kumtambulisha Lowasa kuwa ni mwanachama wa CHADEMA na kumpa dhamana kubwa ya kumteua kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya chama chake na UKAWA. Hii ni aibu kubwa ambayo ni lazima Freeman Mbowe abebe dhamana.

Hata kabla kelele za kukemea uamuzi wa Mbowe kumpendekeza Fisadi Lowasa kuwa mgombea Urais hali iliyochangia anguko KUU la chama hicho na upinzani kwa ujumla hazijaisha, Freeman Mbowe huyu huyu anafanya maamuzi mengine ya GIZANI na ya aibu ya kumteua Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA licha ya mwanasiasa huyo kuhusika kwenye kashfa kadhaa ikiwemo kuuza nyumba za serikali na uuzwaji wa maeneo wazi (open space). Nafahamu kuwa CHADEMA hawana watu wenye maono kuongoza chama chao na ndo maana wanaokoteza tu hata makapi yaliyoachwa na CCM. Nafahamu kuwa mkakati wa Mbowe ni kuhakikisha kuwa Sumaye ndiye anapeperusha bendera ya CHADEMA kwenye uchaguzi Mkuu wa 2020. Ila kwa kashfa hii hakika Mbowe amepotoka

Hata hivyo, ni vema wana CHADEMA na Watanzania kwa ujumla wakajiuliza, i wapi dhamira ya dhati ya Mbowe na chama chake kupambana na ufisadi na mafisadi? Inakuwaje mafisadi sasa wameifanya CHADEMA kuwa ni maficho yao na wamekuwa wakipata good shelter? Huu ujasiri wa Mbowe kuwakumbatia mafisadi na kuwapa vyeo anaupata wapi licha ya wafuasi wa chama hicho kupiga kelele ya kupinga maamuzi hayo na yeye amekuwa KIZIWI na KIPOFU?

Kwa haya makosa ambayo Mbowe amefanya kwa kudhamiria, amepoteza hadhi ya kuwa kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Mbowe pia amepoteza hadhi ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na kwa hali hiyo anapaswa kuachia ngazi mara moja ili kulinda hadhi ya upinzani na chama chake.

Lizaboni sema taratibu unajua na Mzee wetu the KING ana ishu za kivuko kibovu cha bei ya juu na zile Bil. 251 za malipo ya wakandarasi ambazo zinasemekana na CAG kuwa hazijalipwa mkandarasi yeyote, pia eti nyumba za serikali zililipwa watu ambao hawakuwa na sifa za kuuziwa..huu ni upepo tu utapita ndugu yangu waache wapige mikelele na Mafisadi yao huko..Kidumu Chama chetu Milele.
 
Magufuli hahitaji umaarufu, yuko kikazi zaidi, nyie endeleeni kutapatapa na nyumba za serikali zilizouzwa na Sumaye(Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema)
TataMadiba Sumaye alisema eti utaratibu ulifuata najua ni uongo wameuza kwa hila tu akishirikiana na Waziri wa Ujenzi kama mtekelezaji..lakini Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri ambaye ndiye anayetoa ruhusa na maamuzi kwa ajili ya uuzwaji..ina maana na Mh. wa awamu ya 3 naye amehusika kuuza nyumba za serikali kwa bei za hovyoo kabisaa. Huyu mjumbe wa Kamati Kuu ya CDm lazima ajibu pia kwa ufasaha.
 
Back
Top Bottom