Kwa hii kashfa, Mchungaji Anthony Lusekelo (Mzee wa Upako) atajisafishaje?

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Hii "kashfa" Mchungaji Lusekelo alias Mzee wa Upako, Bulldozer, tingatinga na kiboko ya mapepo atachomokaje?

Mzee wa Upako amekumbwa na kashfa ya ulevi na kuleta vurugu kwa majirani zake huko Kawe nyumbani kwake,jirani na ilipo Radio Times.

Inaandikwa katika mitandao kuwa, Mzee wa Upako alfajiri ya jana, wakati mvua kubwa ikinyesha ktk jiji la Dsm, yeye alikuwa mtaani kwake akifanya fujo kwa majirani zake. Mzee wa Upako alikutwa akiwa kalewa "tilatila" huku akiporomosha lugha kali kwa majirani zake hao kupitia kwenye lango la nyumba hiyo.

Nyumba hiyo #KAW/MZN/1348 ni jirani na kwa Mzee wa Upako, malalamiko ya Mch. Lusekelo ni kuwa majirani hao wamekuwa wanamfuatilia muda mwingi kwa kumuita mlevi, na kwamba yeye ni mchungaji fake. Hivyo alfajiri hiyo Mch Lusekelo alikuwa anaenda kuwapa "vidonge" vyao hao majirani wachokozi.

Taharuki hii ya Lusekelo ilimfanya kuegesha gari lake katikati ya barabara na kuzuia watumiaji wengine kupita. Gari hiyo #T 126 DFN ilisimama katikati mwa njia na kusababisha foleni kubwa. Timbwili hilo la mchungaji lilifanyika mpaka kunapambazuka.

Hata alipoombwa kutulia, ndio kwanza aliita walinzi wake(Mabaunsa) ambao walikuja kumpa support.

Waliokuwa eneo la tukio wanasema mchungaji alikuwa pekupeku huku akiwa amekunja suruali na akiwa na "hangover". Huku baadhi ya mashahuda wakisema walinzi wanasema "Baba" yao hakuwa amelala nyumbani usiku uliotangulia.

Kwa kero hiyo, majirani waliita polisi wa Kituo cha Kawe na walikuja kumbeba "bulldozer" na kumuweka ndani. Baadae alihamishwa kituo kingine baada ya pale Kawe kuendelea kufanya fujo mle "Behind Ze Baz"

Wanyetishaji wanasema Mzee wa Upako ni mpenzi wa bapa ndogo na kubwa. Inawezekana juzi aliwapigia bapa majirani wanaomsakama ili kutoa aibu ya kuja kuwabwatukia, sababu wahanga wanasema "In Wine, There is truth". Yaani wengi huongea ukweli wakipata mvinyo kidogo.

Hii ni kama kashfa kwa mzee wa Upako, mchungaji maarufu na mwenye wafuasi lukuki ndani na nje ya nchi. Bulldozer mwenye kipindi channel Ten sasa anakatisha tamaa waumini wake. Je "kashfa" hii Mzee wa Upako atatoka hadharani na kuitolea ufafanuzi? Tusubiri na tuone.

Note: Naomba wenye "Daddy yao" tusiparuane tu hapa. Leo tumjadili Baba kwa matendo haya(Samahanini)




 
Kama kafanya makosa asikosolewe,asisemwe,?

Kwahy ni ruksa kwa kiongozi wa dini kufanya makosa na asisemwe

Aah mentality hii mm huwa siipendi kabisa
Rudia neno kwa neno nilichokiandika ili uelewe nini nilicho maanisha na sio kukurupuka tu mkuu
 
haha haha yaani huyo jamaa mwenye shati ya blue na suluari nyeusi ? makubwa
 
Hakuna jipya chini ya juaaa......... Vyote unavyoviona vilikuwepo...... Hata alchol...??? In Masanja mkandamizaji's voice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…