Kwa heshima na taadhima sisi Wastaafu tunaolipwa na LAPF pamoja na HAZINA hatujalipwa pensheni zetu

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Kwa heshima na taadhima sisi Wastaafu tunaolipwa na LAPF pamoja na HAZINA hatujalipwa pensheni zetu za mwezi Julai 2019 na HAZINA. Maisha ni magumu sana huku mitaani na pensheni ndiyo tegemeo letu kwa sasa ukichukulia umri wetu na magonjwa yanayotunyemelea kwa sababu ya uzee. Tulipeni haki zetu.
 
Hiki kipengele sijakielewa! LAPF pamoja na HAZINA ama LAPF pekee?
Mbona wastaafu chini ya hazina, hakuna mwezi wanaodai?
 
Tunalipwa kama ifuatavyo:- Kabla ya kuingia Serikali za Mitaa nilikuwa nafanya Serikali Kuu kwa miaka kadhaa na kuchangia mafao yangu na baadaye nikaingia Serikali za Mitaa na kuchangia pensheni yangu pale pia. Hivyo katika kukokotoa pensheni yangu natakiwa kulipwa pensheni ya Serikali Kuu niliyofanya kazi na kuchangia mafao yangu kabla ya kuingia Serikali za Mitaa na pili ninatakiwa kulipwa pensheni ya Serikali za Mitaa kupitia LAPF. Natumaini umenielewa.
 
Back
Top Bottom