Kwa heri 2017, kwa heri maumivu!

Malcolmx Shabaaz

Senior Member
Nov 21, 2017
128
174
KWA HERI MWAKA 2017, KWA HERI MAUMIVU!

Mwaka 2017 umemalizika leo tarehe 31.12.2017. Tuliuanza wengi, baadhi yetu tunaumaliza huku wengine tukiwa tumewaacha njiani, hawajafikia mwisho!

Mwaka 2017 umekuwa wa mafanikio kwa baadhi ya watu (wachache sana) huku watu wengi wakiwa wameachiwa maumivu makali mioyoni mwao.

Kuna watu mpaka hivi sasa ujumbe huu unaandikwa wapo wameshikiliwa na vyombo vya usalama kwa kesi za kusingiziwa na wengine kesi zao bado zinaendelea, ikiwemo makumi ya watu wenye kesi za uchochezi.

Kuna watu wamefilisiwa mali zao na dola dhalimu ikiwemo watu wa vyama vya mageuzi ambao mali zao zimeharibiwa kwa amri za viongozi dhalimu. Kwa mfano, Mzee Sumaye mashamba yake yamechukuliwa kwa nguvu na serikali huku Mbowe mashamba yake yakiharibiwa kwa amri ya serikali!

Kuna watu wamejeruhiwa kwa kuteswa na polisi wengi wao wakiachwa na ulemavu wa kudumu. Kuna watu ndani ya huu mwaka wamepoteza wapendwa wao kwa namna hii ama ile, wana maumivu makali. Wapo waliopigwa risasi na polisi kama kijana Said Mheka wa Mikumi.

Kuna watu wametekwa na mpaka leo hawajulikani walipo; ametekwa Azory Gwanda mwanahabari wa Mwananchi na familia ya Ben Saanane wanaufunga mwaka huu wakiwa katika kiza totoro juu ya wapi Ben alipo!

Mwaka huu ni mchungu kwa familia ya Tundu Lissu, anaugulia maumivu ya risasi 16 zilizoingia mwilini mwake kati ya risasi 38 zilizoshambulia gari lake! Tangu tarehe 07 Septemba 2017 mpaka sasa yu hospitali!

Vyama vya upinzani vinaugulia maumivu ya kunyimwa haki ya kufanya shughuli za kisiasa japo kikatiba vyama hivyo vinayo haki ya kuendesha shughuli zao za kisiasa!

Kiuchumi, vyuma vimekaza, hali ni ngumu, biashara zimedorora, serikali inakusanya fedha kwa nguvu kwa kubumba faini za magari nk. Ajira hakuna, wasomi wanarandaranda mitaani hakuna kazi. Vijana wengi wa chuo wamekosa mkopo mwaka huu na wengine wameahirisha masomo yao!

Kibiti hali si shwari, watoto kwa watu wazima wanauawa; polisi kwa raia wanauawa, huu ni mwaka mchungu kwa wakazi wa Kibiti na Watanzania wote wapenda amani!

KWA HERI 2017, NENDA SALAMA!

Na Malcolm X Shabaaz!

imagepng-2517559_p9.jpg
 
Back
Top Bottom