Kwa haya, Serikali haina nia ya kufanyika kwa uchaguz Jijinii Arusha


N

Njaare

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2010
Messages
1,080
Likes
6
Points
135
N

Njaare

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2010
1,080 6 135
Wana JF,

Sasa imethibitika pasipo shaka kuwa serikali ya CCM haiku tayari uchaguzi ufanyike Arusha. Serikali inafanya hivyo kwa kutumia kisingizio kuwa Arusha hakuna amani na hakuna mazingira mazuri ya kufanyika kwa uchaguzi. Jitihada hizi za serikali zinathibitika katika matukio yafuatayo

1
Kutokutangazwa kwa marudio ya uchaguzi kata ya Sombetini. Kwa muda mrefu kata ya Sombetini imekuwa haina diwani na inajulikana wazi kuwa diwani wake Alphonce Mawazo alihamia CHADEMA. Kwa maksudi tume Taifa ya uchaguzi iliamua kutokutangaza marudio ya uchaguzi katika kata hii. Sababu ya kutokutangaza inawezekana ikawa kusababisha wakazi wa arusha waandamane kuhoji ni kwa nini uchaguzi wa kata hiyo haujatangazwa. Kama ingetokea maandamano polisi kama kawaida yao wangeanzisha vurugu ili serikali ipate sababu ya kusema kuwa Arusha hakuna amani na uchaguzi uzuiwe katika kata zote.


2
Tukio la kukamatwa kwa Lema bila sababu za msingi. Inakumbuka kwamba Lema alikamatwa baada ya kuzuia fujo katika chuo cha uhasibu na kumsihi mkuu wa mkoa aje kuongea na wanafunzi. Badala ya mkuu wa mkoa kuwasihi wanafunzi watulie aliwaambia hawana adabu jambo lililosababisha wanafunzi kumzomea. Hata hivyo baadaye mkuu wa mkoa aligeuza kibao kwa Lema kuwa aliwashawishi wanafunzi. Baadaye polisi walienda usiku kumkamata Lema kama vile wanaenda kukamata jambazi. Nia ya polisi hawa walijua kuwa lazima wanaArusha wangeandamana ili Arusha ionekane kuwa ina fujo. Kwa busara ya watu wa Arusha waliona huu ni upuuzi wakadharau na fujo haikutokea hivyo azma ya kuahirisha uchaguzi ikashindikana.


3
Mlipuko wa Soweto. Sina haja ya kurudia yaliyotokea kwani kuna threads nying hapa JF zinayaongelea. Na hapa yaelekea azma ya serikali kufuta marudio ya uchaguzi Arusha itatimia. Serikali inazuia wana Arusha kuwaaga wapendwa wao akiwemo kiongozi wa chama chao kipenzi. Hapa ni mtihani mgumu kwa wana Arusha aidha kukubali serikali izike wapendwa wao bila wao kuwaaga uchaguzi urudiwe tarehe 30/06/2013 au wawage wapendwa wao uchaguzi usirudiwe. Vile vile hata serikali ikiwazika wapendwa wao bila wao kuwaaga bado inawezekana serikali ikazua tukio linguine na uchaguzi ukafutwa.
 

Forum statistics

Threads 1,275,109
Members 490,908
Posts 30,532,856