Kwa haya Nyerere aliitabiria ccm mwisho wake kama chama tawala

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
...Nani asiyejua kwamba msingi wa kufanikiwa kwa TANU, ni umoja wa TANU.
Kadhalika katika vyama vya ushirika au vyama vya wafanyakazi wanachama
wake wanaposhikana bega kwa bega, mambo yao yatawaendea vyema.

Wanachama wake wakigombana na kutengana, mambo yao na mambo ya taifa
zima yatakwenda tenge...


HICHO KILIKUWA NI KIPANDE CHA HOTUBA YA JK MWAKA 1961 UKILINGANISHA NA HAYA YANAYOTOKEA NDANI YA CCM HIVI SASA SI NDIYO HAYO ALIYOYASEMA NYERERE KTK HOTUBA YAKE ? NA SI MNAONA HIVI SASA MAMBO YA TAIFA YANAVYOKWENDA TENGE AU MRAMA KWA SABABU YA KUTOKUWA NA UMOJA HATA NDANI YA CHAMA CHETU KITUKUFU CHA CCM?



 
USAHIHI WA 'SIASA ZA ZAMU YETU YA URAIS' NDANI YA MUUNGANO KATIKA
MFUMO WA VYAMA VINGI NA TANZANIA YA SASA YENYE VIJANA
WENGI WAELEWA KAMA WAPIGA KURA


Unachosema ni sawa lakini mpaka kwanza tukaungane kuandika KATIBA MPYA na kupatikana Tume Huru za Uchaguzi kote Bara na Visiwani.

Lakini cha zaidi, huu utaratibu wa kupeana zammu kushika dola ya nchi hii (i) kwanza ilikua ni utamaduni binafsi ya CCM ambayo tayari wamewasaliti sana katika hilo, (ii) ilikua ni utamaduni wa mfumo wa chama kimoja lakini kwa sasa mpaka ushindani ndio kieleweke, (iii) Wagombea urai wenyewe wawe ni WASTAARABU WA SIASA NA WAKOMAVU kuliko hata alivyo hivi sasa Mzee Dr Ali Mohammed Shein.

Hatutarajii hata siku moja mkatuletee MACHEPELE ilimradi tu zamu imeangukia kwenu wala hatutarajii Vicheche WATAFUTAJI MASLAHI BINAFSI kama vile Maalim Seif kuletwa kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haka!!

Hakika, Wazanzibari wakitaka uzamu kuendelezwa basi ni (1) sharti kwanza wananchi sote tuwe kitu kimoja na kuzungumza lugha moja ya mabadiliko ndani ya taifa letu, (2) ni sharti kuwapa wale Wa-Zanzibari wasiofikirika (kwa sababu tu si watoto wa Karume, watoto wa akina Mwinyi ...) nao wapate nafasi ya kugombea kwani tunaamini hapo Visiwani wapo Wa-Tanzania wengi sana ambao huenda wakawa ni watu wazuri kuliko hata Dr Salim Ahmed Salim (ambaye siku zote hufitinishwa na nyinyi wenyewe huko) na Dr Ali Mohamed Shein (mstaarabu namba mbili wa siasa kote nchi Tanzania baada ya Mwl Nyerere, ambaye baada ya kumaliza kazi ya Urais hapo Visiwani ni sharti akapumzike nyumbani na kubaki mshauri wetu tu) au Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ambao WAKIPEWA NAO NAFASI wanaweza kukubalika kote nchini kiushindani bila shida.

Nasema kwamba endapo unataka 'SIASA ZA ZAMU YETU' kuzingatiwa na sisi vijana tukayakubali basi (iv) ni mpaka utakapowafikiria watu tofauti na Hussein Mwinyi aliyetuua kinyama kule Gongolamboto na kuendeleza ukaidi wa kutokujiuzulu licha ya kutapakaa damu mikono yake yote, (v) ni sharti umuondoe kabisa kwenye ndoto zako huyu M-Kondoa Shamsi Vuai Nahodha na jinsi alivyotuchinja kule Arusha na Mbeya na kukaidi agizo letu wananchi kwamba ajiuzu bila kusikiliza kitu.

Nikipata nauli nitafika Zenji tukashauriane zaidi juu ya namna gani SIASA ZA ZAMU YETU zinavyoweza kuzingatiwa ndani ya Muungano katika Tanzania yenye idadi kubwa ya vijana waelewa na upevu wa akili na uhuru wa maamuzi.
 
...nani asiyejua kwamba msingi wa kufanikiwa kwa tanu, ni umoja wa tanu.
Kadhalika katika vyama vya ushirika au vyama vya wafanyakazi wanachama
wake wanaposhikana bega kwa bega, mambo yao yatawaendea vyema.

Wanachama wake wakigombana na kutengana, mambo yao na mambo ya taifa
zima yatakwenda tenge...


hicho kilikuwa ni kipande cha hotuba ya jk mwaka 1961 ukilinganisha na haya yanayotokea ndani ya ccm hivi sasa si ndiyo hayo aliyoyasema nyerere ktk hotuba yake ? Na si mnaona hivi sasa mambo ya taifa yanavyokwenda tenge au mrama kwa sababu ya kutokuwa na umoja hata ndani ya chama chetu kitukufu cha ccm?



ccm must vanish like it never existed b4!
 
CCM is radioactive with a shortest half life. Nobody wants to be close to any radioactive material, however its shortest half life brings some hope.
 
CCM is radioactive with a shortest half life. Nobody wants to be close to any radioactive material, however its shortest half life brings some hope.


CCM 2011 NA MAKAMBI YAKE MBALI MBALI NCHINI

Hivi kati ya hizi CCM mbali mbali hivi sasa nchini, mwenzetu wewe ni wa kundi gani hasa hapa chini???

1. CCM- Uadilifu (Wazee wenzake na Mwalimu Nyerere ambao ni watulivu, wakomavu na masikini wa kutupwa kwa kuipenda sana nchi na wenye moyo kuitetea Tanzania).

2. CCM- Ufisadi ( Ni kundi dogo linalojiita Wanamtandao au kumbakumba wa kila dili / mchecheto wa kila senti irukayo hewani wenye utayari wa kuuza hata mtoto wake alimradi fedha ipatikane zaidi kufanyia kila aina ya uchafu unaoweza kufikiria; ni wale ambao mpaka hivi sasa wamepepetwana pembeni wasio na kitu na kubakia RA + EL).

3. CCM-Unguja (Chama cha Wazanzibara kama Vuai wa Kondoa na Hussein Mwinyi wa Kisarawe Umatumbini).

4. CCM-Yatima (Ni wale akina Sumaye, Kigoda, Mungai, banduka, Komanya, Ngulume, na wengine waliokua chini ya BWM).

5. CCM-Bongo Flava (Rizi1, Februari Ma-Ropes, Ndungai, Malisa, Nchimbi, ... hawa hawana hela ila kamsimamo wa uongo na kweli)

6. CCM-Mwandosya / Mangula (Kanda ya Juu Kusini)

7. CCM- Six/John Liquor Ma-Padlocks (Kanda ya Ziwa)

8. CCM- Two Coins Mramba / Mrema / Mbatia (moshi Vijijini)

9. CCM-Uislamu (Pwani/ Tanga / Mashariki na Pemba)

Sasa hapa mtu unapoongelea CCM ni sharti uwe makini sana sana na ijulikane kwamba unazungumzia CCM ipi hasa.
 
Back
Top Bottom