Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.
Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!
Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini?
Ni Dr Slaa anayeweza kushughulikia suala la mfumko wa bei. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingi za uongo mpaka kesho hazitatimizwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu yao ya maisha. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..
Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirika wakubwa na wamepindisha sheria na kuruhusu wizi huo kwa maslahi yao. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.
Ni Dr. Slaa ambaye alipanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. CCM imeparamia suala la katiba wakati hata halikuwemo katika ilani yake ya uchaguzi. Ni chama kinachonuka ufisadi na utapeli! Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi?
Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!
Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?
Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?
Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo! Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Sasa juzijuzi Uingereza wamehoji kwa nini Tanzania ni nchi ya kwanza barani Africa kwa kuombaoomba wakati ni nchi ya tatu katika africa kwa utajiri wa dhahabu baada ya Africa kusini na Ghana! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!
Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! .
Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama unayo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani kuna hela..