Kwa hapa tulipofika, ni Dr Slaa tu anastahili kuwa rais wa Tanzania: Sababu ni hizi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hapa tulipofika, ni Dr Slaa tu anastahili kuwa rais wa Tanzania: Sababu ni hizi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RMA, Jan 12, 2012.

 1. R

  RMA JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.


  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!


  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini?


  Ni Dr Slaa anayeweza kushughulikia suala la mfumko wa bei. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingi za uongo mpaka kesho hazitatimizwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu yao ya maisha. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..


  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirika wakubwa na wamepindisha sheria na kuruhusu wizi huo kwa maslahi yao. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.


  Ni Dr. Slaa ambaye alipanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. CCM imeparamia suala la katiba wakati hata halikuwemo katika ilani yake ya uchaguzi. Ni chama kinachonuka ufisadi na utapeli! Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi?


  Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?


  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?


  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo! Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Sasa juzijuzi Uingereza wamehoji kwa nini Tanzania ni nchi ya kwanza barani Africa kwa kuombaoomba wakati ni nchi ya tatu katika africa kwa utajiri wa dhahabu baada ya Africa kusini na Ghana! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!


  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! .


  Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama unayo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani kuna hela..
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,784
  Trophy Points: 280
  kikwete ni janga la Taifa
   
 3. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama ulibahatika kwenda shule hiyo inaitwa fallacy.
  Unamweka wapi Hayati sokoine? Rais kikwete hujaona juhudi zake kupambana na ufisadi?
  OTIS
   
 4. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa mtazamo wako hafifu.
  OTIS
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,784
  Trophy Points: 280
  bila shaka wewe ni mamluki...angalia uchumi wa nchi in general unaelekea wapi...huyu huyu jk bila shaka anataka kumuweka fisadi lowasa madarakani(urais)..ila kama upo kwenye system sikushangai mkuu
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ndoto zingine ni mbaya na hasa kama unategemea kwamba kuna mtu yuko mahali fulani atakupa mafanikio endelea kumuota Dr slaa atakujengea nyumba na kukupa elimu bure
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kikwete ni janga la Taifa
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Na wewe ni mamluki unataka kutulazimisha wote tumkubali Dr silaa.
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  ID yako inakuwakilisha vyema. Halafu inaonyesha kuna kigogo anakuCameron.
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Lakini bado atakuwa ndiye Rais wako hadi 2015 mwambie Dr Slaa awe na Subira hata Maalim Seif alikuwa maarufu huko znz zaidi ya Slaa kwa sasa anasoma magazeti na Lipumba kaikimbia nchi, Mrema kwishinei.
   
 11. M

  MPG JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa ni rais wa Tanzania,Tumaini la watanzania,Kikwete mabangoni,Dr slaa mioyoni mwetu.
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Natabiri Jk anaelezwa hapa kama janga la Taifa atamaliza kipindi chake salama tu na Dr Slaa atagombea mara 3 atashindwa zote
   
 13. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Uchumi wako wauangaliaje wewe mamluki.
  OTIS
   
 14. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu hao washazoea kuhongwa t-shirt na kanga hauwawezi.
   
 15. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Bila kutukana hamuwezi kujenga hoja.
  OTIS
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Sisiemu ni janga la taifa hakuna walichofanya hata kimoja kikaonekana,usije ukasema sisiemu inajenga daraja ni hapana,ni fedha zetu za kodi na pili ni fedha zetu tulizochanga nssf,narudia tena serikali ya sisiemu hakuna hata kimoja walichofanya.
   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ulikuwa unafanya nini chumbani nikiwa na kigogo kama hakutupanga foleni/zamu ya kutuCameron. kumbe na wewe unapenda kamchezo hako ka chama cha conservative chama rafiki wenu mmmmh ningeshangaa kama hukatumii
   
 18. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Shirikisha ubongo wako mara moja moja tafadhali.
  OTIS
   
 19. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usikute hawa ndio mboga ya wakubwa wakiwa katika kampeni na ziara za viongozi wa chama mikoani.
   
 20. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  word.
  OTIS
   
Loading...