OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,015
- 114,360
Joto la Siasa lipo juu sana kwa sasa. Joto hili linakolezwa zaidi na mwenendo wa Rais Magufuli,ziara zake na baadhi ya kauli tata ambazo amekuwa akizitoa katika ziara zake
Pamoja na kuwa mwenendo na kauli zake umekuwa ukipata upinzani mkuu chini kwa chini na hasa mitandaoni,lakini siasa za majukwaa zimepigwa marufuku
Baadhi ya wanasiasa wa upinzani hasa Freeman Mbowe,Tundu Lisu,Zitto Kabwe,Julius Mtatiro,Hashim Rugwe na Maalim Seif wamekuwa wakiweka wazi kutokuunga mkono mwenendo wa rais Magufuli.....
Hali ni mbaya zaidi mitaani ambapo makundi mbalimbali yamekuwa yakishangazwa na kauli tata za rais ikiwa ni pamoja na mwenendo wake
Ukijaribu kusikiliza kauli za Tundu Lissu akiongea na media,na mkutano wa Zito Kabwe huko Kigoma na hata ziara za Lowasa utakubaliana nami kwamba siku ambayo mikutano ya Siasa ikiruhusiwa katika hali aliyonayo Magufuli itaweza kusababisha vita Kali sana ya maneno na hatimaye kuleta mpasuko mkubwa.
Vita hii itaweza kusababisha nchi kutokutawaliwa kabisa kwa kuwa wananchi watakorogwa isivyo kawaida. Katika hali ya kawaida itakuwa kila atakapopita rais atapita mwanasiasa mwingine kujibu au kutia sumu
Ushauri kwangu ni kuwa ni lazima washauri wa rais au hata wazee wetu wajitokeze kumshauri rais asome alama za nyakati na aweze kujirekebisha akipojikwaa. Hakuna ubishi sio sisi tu tunaoshangazwa na mwenendo na kauli zake,wako wengi wana CCM ambao wanaumia kimya kimya wakimezea. Aibu wanazopata wakimtetea Magufuli ni kuwa sana.Mazuri anayofanya yaponzwa na ubabe na ukali usio na ulazima.
Kubadilika kwa rais kutashusha Joto la siasa kama ilivyokuwa wakati wa Kikwete ambapo siasa za majukwaani hazikuwahi kututenganisha wala kuombeana mabaya na kutukanana