Kwa hali hii Tundu Lissu ajitafakari

Kali _D

Senior Member
Feb 10, 2019
145
132
*WATANZANIA WENZANGU MMEMSIKIA TUNDU LISSU? NAULIZA TENA MMEMSIKIA?*

Yaani Tundu Lissu amepewa adhabu na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ya kutofanya kampeni kwa siku 7 kutokana na kukiuka maadili ya uchaguzi halafu anakimbilia kujirekodi malalamiko yake kwa kiingereza ili awatumie waliomtuma kuja kugombea urais kwa sababu hawaelewi kiswahili.

Ndio maana nauliza Watanzania wenzangu ambao mimi na nyie lugha yetu ni kiswahili bado hamjamuelewa huyu mtu na dhamira yake mbaya kwa nchi yetu?

Nimemkumbuka Mwigulu Nchemba aliyesema kuna baadhi ya wagombea wameshachukua ‘advance’ kwa mabeberu kwa ahadi ya kuja kuchukua kiti cha urais ili hao mabeberu waje kuichezea nchi yetu wanavyotaka, waje waturudishe kwenye ukoloni, watawale rasilimali zetu, watutumikishe kama watumwa, watunyime elimu, waharibu miundombinu, wanyang’anye mashamba yetu, waue viwanda vyetu, waue biashara zetu, waue miradi yetu mikubwa ya umeme, reli, ndege, maji, afya, elimu nk.

Tusikubali huyu Tundu Lissu katumwa, anataka kutumia usomi na uanasheria wake kutuumiza. Na ndio maana kwenye kampeni zake hazungumzi kuhusu mahitaji ya msingi ya Watanzania, anafanya kazi ya kuipaka matope Tanzania ili machoni mwa mataifa ya nje ionekane ni nchi ya hovyo. Yaani ni yeye tu ndio aonekane mtu wa maana na anayejua kila kitu hapa Tanzania.

NEC imechukua hatua kwa taratibu ambazo yeye mwenyewe aliziridhia na akatia saini kabla ya kuanza kampeni. Kampeni imeanza, ameanza kuvunja taratibu waziwazi halafu alitaka aachwe?

Acha hii ya kuvitusi vyombo vya Dola, NEC na Wagombea wenzake, kufanya uchochezi hasa aliposema Wasimamizi wa uchaguzi wameitwa na Rais Magufuli ili wavuruge uchaguzi kitu ambacho ni uongo mkubwa, huyu Tundu Lissu alianza vurumai mapema kabisa wakati wa kutafuta wadhamini ambapo alianza kampeni kabisa na kila mmoja aliona. Angeweza kushughulikiwa wakati ule aliachwa, lakini kwa michezo anayofanya sasa HAPANA!!

Hapa Watanzania tuwe macho sana, huyu mtu ametumwa kuja kutuvuruga, tusipokuwa makini tutavurugana kwelikweli na tukumbushane watakaoumia ni sisi wanyonge.

Tayari tumeshaona jinsi chama chake cha CHADEMA na washirika wao ACT Wazalendo wanavyosababisha madhara.

Kule Njombe vijana wa CHADEMA wakiongozwa na waliokuwa wagombea udiwani wamemuua kijana Emmanuel Mlelwa aliyekuwa kiongozi wa Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM), kule Tunduma kundi la vijana wa CHADEMA wakiongozwa na aliyekuwa mgombea udiwani wa kata ya Kaloleni wamemuua kijana Briton Wilfred Mollel aliyekuwa mwana UVCCM na ambaye ameacha mke na watoto 3 wa chini ya miaka 6 (wote mmeona Rais Magufuli alivyomwaga chozi alipokutana na mke wa marehemu, mama wa marehemu na watoto wadogo wa marehemu) na kule Zanzibar tumeona wafuasi wa ACT-Wazalendo walichokifanya, wamevamia msikiti na kushambulia wana CCM waliokuwa wanaswali Msikitini kwa mapanga, wamemkata shingoni Ndg. Hamis Nyange Makame mwenye miaka 63 na mpaka sasa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar akitibiwa jeraha la panga lililochimba shingoni kwa nchi 14.

Haya mambo hayafanyiki kwa bahati mbaya ndivyo viongozi hawa vibaraka walivyotumwa na mabeberu. Ndio maana Freeman Mbowe aliwahi kusema ili mambo ya upinzani yakae sawa lazima wafe watu kama 200 hivi na alitamka hadharani kwenye mkutano.

Narudia Watanzania tuwe makini, tuwakatae hawa mawakala wa mabeberu watatuharibia nchi yetu, watatuondolea amani ili jamaa wajipenyeze tena baada ya Rais Magufuli kuwabana kila mahali. Huu ndio ukweli.

Nani asiyejua kuwa wamenuna baadaya ya kubanwa kwenye madini ambako walikuwa wanasomba wanavyotaka na watanzania wanaachwa masikini?

Nani asiyejua walivyokuwa wanakwapua pesa zetu za umeme kupitia kampuni zao za kufua umeme wa mafuta ambapo Tanzania ilikuwa inalipa mabilioni ya pesa na sasa wamenuna baada ya Rais Magufuli kufuta mikataba hiyo na kuanza kujenga Bwawa la Nyerere ambalo litazalisha megawati 2,115 na litamaliza kabisa tatizo la umeme huu wa gharama?

Nani asiyejua kuwa wamenuna baada ya kufutwa kwa mikataba ya gesi ambapo hawa jamaa walijiandaa kubeba gesi yetu yote huku sisi tukiachwa bila kunufaika na chochote?

Nani asiyejua kuwa hawa jamaa hawakutaka kabisa tununue ndege zetu, walitaka walete makampuni yao ili waweze kutawala biashara ya utalii na usafirishaji wa abiria.

Nani asiyejua kuwa wamenuna baada ya kuona Rais Magufuli anakataa mikopo yao ya kinyonyaji yenye masharti yanayotweza utu wetu na yanawatukuza watu waliotutawala kabla ya kupata uhuru?

Nani asiyejua kuwa jamaa wamenuna baada ya vibaraka wao waliokuwemo Serikalini kutumbuliwa na Rais Magufuli baada ya kubainika kuwa wanalihujumu Taifa?

Nani asiyejua kuwa wamenuna baada ya wanasiasa waliokuwa wanawatumia kubanwa mbavu kiasi cha kupoteza umaarufu kabisa na kushindwa kupenyeza mambo yao.

Nani aisiyejua kuwa jamaa wamenuna baada ya Rais Magufuli kudhibiti uhamiaji halamu, ujangili na utoaji holela wa vibali vya kazi vilivyosababisha Watanzania kukosa ajili na maliasili zetu kutoweka.

Yapo mengi sana lakini itoshe kusema Watanzania tuwe macho na tuwaoneshe kwenye uchaguzi huu kuwa Tanzania ni nchi huru inayopaswa kujiamulia mambo yake yenyewe na sio kuamuliwa na watu wengine.

NEC iachwe itimize wajibu wake kwa mujibu wa sheria na wote waliopata nafasi ya kugombea wafuate sheria, taratibu na miongozo ya NEC. Haiwezekani mtu alete varangati halafu aachwe, huo sio utaratibu hata kidogo.

Na sie Watanzania tutimize wajibu wetu wa kuwakataa watu wanatengeneza mambo ya kutumaliza wenyewe.

Asanteni.

Mzee Julius Julius Mtendeleki
Dar es Salaam
Oktoba 3, 2020.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom