Kwa hali hii Tanesco mtatuangusha kwenye SGR

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Messages
3,956
Points
2,000

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2014
3,956 2,000
Wiki mbili hizi umeme umekua ukikatika na kurudi baada ya muda naona sasa inaongezeka, Kijichi toka asubuhi wamekata na haujarudi hadi sasa.

Shida moja shirika letu huwa halina taarifa mara nyingi, ni kitu cha ajabu kukatika umeme kwa masaa sita halafu hupewi taarifa ya kabla au baada ya umeme kurudishwa.

Wasiwasi wangu, je mradi huu wa SGR ambao tunaambiwa utatumia nishati umeme itakuaje ikiwa mwenendo wetu wa umene ni huu? Au tutegemee Tanesco kubadilika sana katika miundombinu na utendaji?

Tatizo hili nakumbuka tokea awamu ya tatu ndio lilianza kujitokeza kwa mapana yake hadi leo tuko awamu ya tano bado solution haijapatikana licha ya kuvumbua gesi na vituo kadhaa vya ku-boost power.

Je, tutafika?
 

Forum statistics

Threads 1,366,453
Members 521,454
Posts 33,369,495
Top