Kwa hali hii ni bora niahirishe kuoa tu

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,514
2,000
Ndugu zangu ni kitambo sana sijaweka neno hapa, nimekuwa nikisoma yanayoendelea kutukumba binadamu sisi kwenye maisha yetu ya kila siku.
Kwa mara ya mwisho niliweka uzi wangu hapa, baada ya mpenzi wangu kujikata mshipa wa mkono wake akitishia kuijiua kama nitaondoka kwenda kwa mzazi mwenzangu Dodoma.(uzi ule upo hapa jukwaani)

Kilichonifanya kuleta uzi huu hapa jukwaani ndugun zangu ni tukio la hivi karibuni, ambalo kimsingi sikulitegemea hata kidogo, na limefanya nibadili kabisa mtazamo wangu kwa baadhi ya wanawake.

Baada ya ile misuko suko ya mpenzi wangu kutaka kujiua kupita, maisha yaliendelea pasipo purukushani zenye athari kwenye maisha yetu. Nilijitahidi kutafuta uhamisho kutoka Tanga kwenda mkoa mwingine wowote hasa MWANZA ili nianze upya kabisa maisha yangu, na kuwaza namna gani naweza kuandaa kesho ya watoto wangu, maana mimi nadhani ujenzi wa familia kamili yenye muunganiko wa baba mama na watoto unaelekea kunishinda kutokana na matukio yanayoendelea kunitokea kimahusiano. kwa hiyo hitimisho pekee nililokuwa nimelifikia ni kuanza maisha mapya ya peke yangu, na kuwatunza watoto wangu.

Ajabu ni kwamba nikiwa nawaza namna ya kumhamisha mtoto wangu wa kwanza kutoka anakoishi na mama yake nitakapofanikiwa kuhamia Mwanza,nikapokea Simu ya mama wa watoto wangu (ukirejea uzi wangu nilieleza kuwa mzazi mwenzangu tuna watoto wawili japo hatujaoana), akaniambia kwa sasa AMEOKOKA NA HIVYO anataka kuongea nami kwa mambo kadhaa ili awe huru, nikampongeza kwa uamuzi mzuri huku moyoni nikijua sasa hapa ndo penyewe, kama akibadilika na kuwa mwema sina namna itabidi nimuoe tu.

Nikiwa naendelea kumsikiliza nikashikwa na butwaa aliponambia "UKWELI NI KWAMBA WATOTO HAWA SIO WA KWAKO!!!,ROHO INANISUTA NA SIO RAHISI KUUSEMA HUU UKWELI, LAKINI KWA KUWA SASA NIMEAMUA KUOKOKA NAKWAMBIA ILI UAMUE, UKIUJUA UKWELI HUU" NAOMBA MSAMAHA WAKO NA KWA MUNGU PIA,ILI NIWEZE KUWA NA AMANI,NAOMBA SANA MSAMAHA WAKO!!"

Nilisikia mwili mzima umepigwa ganzi, kwani miaka yote ninajua watoto ni wangu, kwa mantiki hiyo naanza kuingia mashaka kwamba yawezekana hata huyu wa Tanga sio wangu, maana kwa namna yule mwanamke wa Dodoma alivyokuwa, sikuwa kudhani kama anaweza kuwa alinisingizia, lakini nguvu ya IMANI imeyafunua haya.
Najisikia kizungu zungu kila nikiwaza, mpaka sasa nimemuuliza mara kadhaa, na majibu yake hayajabadilika hata kidogo, anasisitiza watoto sio wangu!

Naomba mwenye kujua hatua za kupima uwezo wa mbegu za kiume kuzalisha anisaidie, nianzie hapo kwanza, kwa kujua kama nina weza kuzalisha au lah, then baada ya hapo nifanye vipimo vya DNA na huyu wa Tanga, then nijue namna ya kuiendea kesho yangu!
NIMECHOKA SANAAA!
Pole sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom