Kwa hali hii ni bora niahirishe kuoa tu

ThaGreatman

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
654
1,000
Ndugu zangu ni kitambo sana sijaweka neno hapa, nimekuwa nikisoma yanayoendelea kutukumba binadamu sisi kwenye maisha yetu ya kila siku.
Kwa mara ya mwisho niliweka uzi wangu hapa, baada ya mpenzi wangu kujikata mshipa wa mkono wake akitishia kuijiua kama nitaondoka kwenda kwa mzazi mwenzangu Dodoma.(uzi ule upo hapa jukwaani)

Kilichonifanya kuleta uzi huu hapa jukwaani ndugun zangu ni tukio la hivi karibuni, ambalo kimsingi sikulitegemea hata kidogo, na limefanya nibadili kabisa mtazamo wangu kwa baadhi ya wanawake.

Baada ya ile misuko suko ya mpenzi wangu kutaka kujiua kupita, maisha yaliendelea pasipo purukushani zenye athari kwenye maisha yetu. Nilijitahidi kutafuta uhamisho kutoka Tanga kwenda mkoa mwingine wowote hasa MWANZA ili nianze upya kabisa maisha yangu, na kuwaza namna gani naweza kuandaa kesho ya watoto wangu, maana mimi nadhani ujenzi wa familia kamili yenye muunganiko wa baba mama na watoto unaelekea kunishinda kutokana na matukio yanayoendelea kunitokea kimahusiano. kwa hiyo hitimisho pekee nililokuwa nimelifikia ni kuanza maisha mapya ya peke yangu, na kuwatunza watoto wangu.

Ajabu ni kwamba nikiwa nawaza namna ya kumhamisha mtoto wangu wa kwanza kutoka anakoishi na mama yake nitakapofanikiwa kuhamia Mwanza,nikapokea Simu ya mama wa watoto wangu (ukirejea uzi wangu nilieleza kuwa mzazi mwenzangu tuna watoto wawili japo hatujaoana), akaniambia kwa sasa AMEOKOKA NA HIVYO anataka kuongea nami kwa mambo kadhaa ili awe huru, nikampongeza kwa uamuzi mzuri huku moyoni nikijua sasa hapa ndo penyewe, kama akibadilika na kuwa mwema sina namna itabidi nimuoe tu.

Nikiwa naendelea kumsikiliza nikashikwa na butwaa aliponambia "UKWELI NI KWAMBA WATOTO HAWA SIO WA KWAKO!!!,ROHO INANISUTA NA SIO RAHISI KUUSEMA HUU UKWELI, LAKINI KWA KUWA SASA NIMEAMUA KUOKOKA NAKWAMBIA ILI UAMUE, UKIUJUA UKWELI HUU" NAOMBA MSAMAHA WAKO NA KWA MUNGU PIA,ILI NIWEZE KUWA NA AMANI,NAOMBA SANA MSAMAHA WAKO!!"

Nilisikia mwili mzima umepigwa ganzi, kwani miaka yote ninajua watoto ni wangu, kwa mantiki hiyo naanza kuingia mashaka kwamba yawezekana hata huyu wa Tanga sio wangu, maana kwa namna yule mwanamke wa Dodoma alivyokuwa, sikuwa kudhani kama anaweza kuwa alinisingizia, lakini nguvu ya IMANI imeyafunua haya.
Najisikia kizungu zungu kila nikiwaza, mpaka sasa nimemuuliza mara kadhaa, na majibu yake hayajabadilika hata kidogo, anasisitiza watoto sio wangu!

Naomba mwenye kujua hatua za kupima uwezo wa mbegu za kiume kuzalisha anisaidie, nianzie hapo kwanza, kwa kujua kama nina weza kuzalisha au lah, then baada ya hapo nifanye vipimo vya DNA na huyu wa Tanga, then nijue namna ya kuiendea kesho yangu!
NIMECHOKA SANAAA!
 
fogoh2

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
3,518
2,000
kujua mtoto ni wako au sio wako ni rahisi sana.damu haipotei nenda kwa hao watoto ukiwa na ndugu yako mkubwa,either kaka,dada,baba mdogo au mzazi mkague mtoto kama ni wako kuna alama tu za ukoo wenu zitaonekana ila kama itatokea hamjafafana andaa laki tano kapime DNA .ila nina uhakika huyo mwanamke amepata bwana na huyo bwana kajitolea kubeba mwanamke na watoto hivyo ushatolewa kwenye reli mkuu
 
sundoka

JF-Expert Member
Oct 9, 2011
1,794
2,000
Uamuzi wako kwenye paragraph ya mwisho ni mzuri sana. Kupima fertility ya mbegu ni kazi ndogo sana. Kwenye labs nyingi za kawaida wanapima tu. Na sio bei kubwa ni around 10,000 labda mpaka 20,000 kutegemea na hosputal/lab yenyewe au na jinsi unavyofahamiana na wahusika. Ni vema ukajua uwezo wako wa kutungisha mimba ili uamue sasa kutafuta mtoto wa damu yako halisi na kama uwezo wa kutungisha mimba hauna uache kuhangaika na hayo mambo yanayokupotezea hela kwa kubambikiwa mimba.

Suala la DNA silijui vizuri. Tusubiri watabe wa haya mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
alumn

JF-Expert Member
Jul 15, 2018
1,373
2,000
Pole sana mkuu, ndio ya ulimwengu. Ila kuna mambo usiombe yakukute ni kuendelea kuyasikia tu kama hivi..
 
ThaGreatman

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
654
1,000
kujua mtoto ni wako au sio wako ni rahisi sana.damu haipotei nenda kwa hao watoto ukiwa na ndugu yako mkubwa,either kaka,dada,baba mdogo au mzazi mkague mtoto kama ni wako kuna alama tu za ukoo wenu zitaonekana ila kama itatokea hamjafafana andaa laki tano kapime DNA .ila nina uhakika huyo mwanamke amepata bwana na huyo bwana kajitolea kubeba mwanamke na watoto hivyo ushatolewa kwenye reli mkuu
Inawezekana ikawa kweli, lakini wanawake walio wengi ni dhaifu sana linapokuja swala la hisia, NIMEWAZA KWAMBA KWA HILI LA KUOKOKA inawezekana kabisa kuwa ameniambia uhalisia wa jambo lenyewe!

Watu wengi linapokuja swala la imani, likakaa sawa sawa katika hisia, tunaweza kusema siri ambazo hatujawahi kuzisema popote!!
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,498
2,000
Kwahiyo watoto wako lakini hakuna hata ka alama kamoja kakukupa matumaini kuwa ni wa kwako..?
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,604
2,000
Ndugu zangu ni kitambo sana sijaweka neno hapa, nimekuwa nikisoma yanayoendelea kutukumba binadamu sisi kwenye maisha yetu ya kila siku.
Kwa mara ya mwisho niliweka uzi wangu hapa, baada ya mpenzi wangu kujikata mshipa wa mkono wake akitishia kuijiua kama nitaondoka kwenda kwa mzazi mwenzangu Dodoma.(uzi ule upo hapa jukwaani)

Kilichonifanya kuleta uzi huu hapa jukwaani ndugun zangu ni tukio la hivi karibuni, ambalo kimsingi sikulitegemea hata kidogo, na limefanya nibadili kabisa mtazamo wangu kwa baadhi ya wanawake.

Baada ya ile misuko suko ya mpenzi wangu kutaka kujiua kupita, maisha yaliendelea pasipo purukushani zenye athari kwenye maisha yetu. Nilijitahidi kutafuta uhamisho kutoka Tanga kwenda mkoa mwingine wowote hasa MWANZA ili nianze upya kabisa maisha yangu, na kuwaza namna gani naweza kuandaa kesho ya watoto wangu, maana mimi nadhani ujenzi wa familia kamili yenye muunganiko wa baba mama na watoto unaelekea kunishinda kutokana na matukio yanayoendelea kunitokea kimahusiano. kwa hiyo hitimisho pekee nililokuwa nimelifikia ni kuanza maisha mapya ya peke yangu, na kuwatunza watoto wangu.

Ajabu ni kwamba nikiwa nawaza namna ya kumhamisha mtoto wangu wa kwanza kutoka anakoishi na mama yake nitakapofanikiwa kuhamia Mwanza,nikapokea Simu ya mama wa watoto wangu (ukirejea uzi wangu nilieleza kuwa mzazi mwenzangu tuna watoto wawili japo hatujaoana), akaniambia kwa sasa AMEOKOKA NA HIVYO anataka kuongea nami kwa mambo kadhaa ili awe huru, nikampongeza kwa uamuzi mzuri huku moyoni nikijua sasa hapa ndo penyewe, kama akibadilika na kuwa mwema sina namna itabidi nimuoe tu.

Nikiwa naendelea kumsikiliza nikashikwa na butwaa aliponambia "UKWELI NI KWAMBA WATOTO HAWA SIO WA KWAKO!!!,ROHO INANISUTA NA SIO RAHISI KUUSEMA HUU UKWELI, LAKINI KWA KUWA SASA NIMEAMUA KUOKOKA NAKWAMBIA ILI UAMUE, UKIUJUA UKWELI HUU" NAOMBA MSAMAHA WAKO NA KWA MUNGU PIA,ILI NIWEZE KUWA NA AMANI,NAOMBA SANA MSAMAHA WAKO!!"

Nilisikia mwili mzima umepigwa ganzi, kwani miaka yote ninajua watoto ni wangu, kwa mantiki hiyo naanza kuingia mashaka kwamba yawezekana hata huyu wa Tanga sio wangu, maana kwa namna yule mwanamke wa Dodoma alivyokuwa, sikuwa kudhani kama anaweza kuwa alinisingizia, lakini nguvu ya IMANI imeyafunua haya.
Najisikia kizungu zungu kila nikiwaza, mpaka sasa nimemuuliza mara kadhaa, na majibu yake hayajabadilika hata kidogo, anasisitiza watoto sio wangu!

Naomba mwenye kujua hatua za kupima uwezo wa mbegu za kiume kuzalisha anisaidie, nianzie hapo kwanza, kwa kujua kama nina weza kuzalisha au lah, then baada ya hapo nifanye vipimo vya DNA na huyu wa Tanga, then nijue namna ya kuiendea kesho yangu!
NIMECHOKA SANAAA!
Cc. myplusbee
Mwenye watoto ni mama yao.
 
fogoh2

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
3,518
2,000
Inawezekana ikawa kweli, lakini wanawake walio wengi ni dhaifu sana linapokuja swala la hisia, NIMEWAZA KWAMBA KWA HILI LA KUOKOKA inawezekana kabisa kuwa ameniambia uhalisia wa jambo lenyewe!

Watu wengi linapokuja swala la imani, likakaa sawa sawa katika hisia, tunaweza kusema siri ambazo hatujawahi kuzisema popote!!
kwani watoto hujawaona? mimi nina watoto wawili ukiwaona unaweza kusema ni wadogo zangu wa baba mmoja mama mmoja ,hata kama hujaambiwa ni wanangu ila ukiwaona na ukiniona mimi huulizi mara mbili.vp wewe huko
 
Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
12,296
2,000
Na hii ni possiility kubwa.
Basi la kufanyika ni akapime dna.
Asikubali kuback down kirahis hivyo. Akapime Dna that will be the final decion.
Kama huyo mwanamke anamdanganya ataumbuka
kujua mtoto ni wako au sio wako ni rahisi sana.damu haipotei nenda kwa hao watoto ukiwa na ndugu yako mkubwa,either kaka,dada,baba mdogo au mzazi mkague mtoto kama ni wako kuna alama tu za ukoo wenu zitaonekana ila kama itatokea hamjafafana andaa laki tano kapime DNA .ila nina uhakika huyo mwanamke amepata bwana na huyo bwana kajitolea kubeba mwanamke na watoto hivyo ushatolewa kwenye reli mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,855
2,000
Hii story part kubwa unaonekana wewe ni bwege, mademu wanakuchukulia poyoyo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom