Kwa dalili zinazoendelea, huyu nahodha alishushwa chomboni?

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
images (16).jpeg

Pichani: Maili Miambili Kisiwa Cha umofia

Nadhani katika jamii yetu hakuna ambaye hajapata kusikia umaarufu wa meli ya MV Twiga iliyokuwa na jina la kiswahili katika Taifa la umofia. Hii Ni meli kongwe ambayo iliendeshwa na manahodha stadi watano kwa kipindi Cha miaka 62 huku Bwana Janfedha akiendesha kwa kipindi kirefu zaidi Cha miaka 20 na kadhaa.

images (17).jpeg

Pichani: Meli ya MV Twiga iliyopewa jina kutokana na Urefu wake

Masimulizi ya umofia na meli hii ni mengi mengine ya kutisha na yakutia hofu, hakuna miongoni mwa watu wasio fahamu simulizi la Bwana Dukatatu mtu mrefu Sana aliyedumu kumsaidia Bwana Janfedha kuendesha chombo, aliposhushwa ghafla hadharani mwishoni mwishoni mwa unahodha wa Janfedha watu wa zamani wanamkumbuka vizuri bwana huyu wa miraba minne na maamuzi magumu!

images (15).jpeg

Pichani: Bwana wa Milaba minne siku zote alinisaidia Janfedha kuendesha Mv Twiga

Lakinipia yapo mengi mazuri ya MV Twiga katika Taifa letu la umofia ambayo haya hata manahodha watano hawa huyasimulia na kuyafundisha katika shule zetu. Yale mabaya huwa Siri kubwa Sana hapa umofia na Ni watu mashuhuri tuu kama akina Gentamycin wanaweza kuyazungumza kwa mafumbo.

images (20).jpeg

Pichani Prognosticator Gentamycin

Nisiwachoshe Sana. Katika Karne ya 17 mwaka wa nne tarehe 20 majira ya mvua mwezi hapana kumbukumbu katika umofia yote yule bwana nahodha hodari watano Mr Ugimbi alishushwa ghafla chomboni. Katika tukio hili la kushtushwa na lenye usiri Wana umofia walielezwa bwana huyu amekiacha chombo na kutumbukia majini!

Kwa umashuhuri wa Mv Twiga na mikogo ya bwana huyu nisichelee kusema kuwa hili Ni tukio Gumu Sana kuwahi kutokea umofia.Zipo simulizi nyingi kuhusu nahodha huyu huku wasaidizi wake wakisema kuwa amelemewa tuu na usingizi kama ilivyokuwa kwa nahodha wa Ulubwanji nchi ya konde na mataifa mengine mengi,lakini hili Ni tukio la kwanza na la kipekee Umofia.

Kweli tuliamini ameshuka chomboni agharabu kabla ya Mvua nne chombo kutia nanga na tulionesha hisia zetu za kusikitishwa mno!

Kinacho nifanya niandike hekaya hii ni yale yaliyoendelea umofia baada ya kushuka kwake chomboni, yananifanya nijiulize je Huyu nahodha alishuka chomboni au alishushwa?

Nakumbuka kabla ya Matanga kumalizika siku iliyofuata bwana yule kushushwa chomboni wanaumofia walisomewa taarifa namna Bwana Ugimbi alivyokuwa akiendesha MV Twiga. Taarifa Ile ndiyo Ile ambayo walitarajia asomewe Mtukufu Ugimbi ikiwa asingeshuka chomboni. Kinyume na matarajio yetu tulishuhudia taarifa Ile ikiwa na maneno ya mwenendo mbaya Sana wa Bwana Ugimbi, nahodha mpya Mwenye asili ya Uajemi akamshusha chomboni mmoja Kati ya waangalizi wa Mali wakati wa Bwana Ugimbi!

Hali hii ilitushtushwa Sana wanaumofia tukaanza kuwaza je hii taarifa iliandaliwa lini? Je tukiwa kwenye masikitiko makubwa ya Bwana huyu baadhi yao walikuwa wakipika taarifa hii? Je hatukuwa nao katika maombolezo watu Hawa? Je sio wenzet Hawa.

Yaliyofuata baada ya hapo Ni taarifa hii kusomwa Tena Mara ya Pili safari hii si mbele ya Muajemi huyu loh! Haijapata kutokea taarifa hii kusomwa Mara mbili au tatu Tena Mara hii ikimponda zaidi Bwana Ugimbi ikigusa vile vipaumbele vyake alivyovifanya kwa uhodari mkubwa pasipo kuchola.

Wengi miongoni mwa wanaumofia walimuona Bwana huyu mpika taarifa hamnazo, maana hajawahi kupika taarifa Kama hii wakati wa unahodha wa Bwana Ugimbi.

Ni Jambo wazi kuwa yupo kukamilisha kazi iliyoandaliwa na walio mshusha chomboni nahodha yule wa Mv Twiga. Lakini kumbe mpika taarifa si peke yake wapo wengi hasa katika kile chumba Cha washauri ambao wao kwa miaka kadhaa ya uongozi wa Mbabe huyu Ugimbi hawakufanya kazi isipokuwa kumsifia tuu! Tulipo ingia katika chumba Chao tulikuta mazito! Yule kiongozi wao Mkuu Sabu aliyewahi kupendekeza nahodha wetu Ugimbi atuendeshe hata kwa miaka 40 Leo anapinga mkakati mgumu Sana wa Bwana Ugimbi wa kuokoa fedha za wasafiri wa chombo Jambo ambalo tunahisi kuwa Ni moja Kati ya mambo yaliyomshusha chomboni nahodha wetu. Je? Ni msimamo wake au anatumwa na lile genge lililomshusha chomboni nahodha wetu?

images (22).jpeg

Pichani: Mkuu Sabu na Baraza la washauri

Yapo Mambo mengi Sana Pele Umofia! Hata wale waliokuwa wakila meza moja na Mr Ugimbi akina mkuu Sabu na Yule kijana asiye na maadili Leo wanamtuhumu Mr Ugimbi kwa Tuhuma ambazo hawezi kuzijibu.

Mr Ugimbi ataendelea kukaa akilini mwa wanaumofia kwani viongozi wengi wachini yake waliwaaminisha wanaumofia kuwa Ugimbi pekee ndiye wa kutuvusha. "Hata Mimi ingali sikumsifia mwanzo kwa kuepuka ujinga wa sifa zile Sasa nitasimama na Ugimbi maana sitaki kuwa sehemu ya wanafiki" alisema mzee mtwa mkulu wa umofia kwenu.

images (21).jpeg

Pichani: mtwa mkulu wa mtu mwenye hekima na nadhifu wa umofia

Zipo sababu mbili ambazo huenda zilipelekea lile genge linaloaminika kuimiliki umofia huenda lilizitumia kumshusha nahodha huyu wa umofia

1. Kwakuwa mtukufu Ugimbi alikuwa akiiendesha Mv Twiga na kuipeleka kusiko eleweka, wao kwa ukongwe wao huenda waliliona hili wakaamua wamshushe.

2. Mtukufu Ugimbi alikuwa akienda vizuri Ila wamemshusha kwa maslahi yao na kwakuwa hasa alikuwa akipingana na Sera zao.

images (19).jpeg
Pichani: Nahodha wa kwanza wakike aliyefahamika Kama Muajemi kwa asili yake. Mwanzo alimsaidia Ugimbi kushika usukani

Hatuwezi kujua mazingira ya siku za mwisho za Bwana Ugimbi. Kinachokumbukwa Ni sura za majuto na huzuni kubwa kwa wale wawili walio kuwa wakikaa nyuma yake ambao huenda walijua yakiyo mkuta Ugimbi siku za mwisho za safari yake. Mengi yanabaki kuwa Siri Kama ilivyo desturi ya Wana umofia.

Hiki ndicho Kisa kilicho sababisha Umofia kutawaliwa na Muajemi. Na watoto wa Umofia husimuliana masimulizi ya Bwana Ugimbi hodari daima katika viambaza vyao nyakati za jioni.

Haya ndiyo niliyoyaona kisiwani umofia kabla ya Ile safari ya kumuona Fuma Lyongo.

images (18).jpeg

Pichani Ni sanamu ya Ugimbi katika mji mkuu wa katikati ya Umofia!
 
Weye zungumza tu.

Taifa la umofia linaongoza kwa idadi ya watu.

Lakini mbona kama msaidizi wa tatu wa nahodha alilia sana alipokosa majibu ya ni sehemu ipi nahodha alijikwaa kabla ya kushuka chomboni na kutumbukia majiini?

Au alishushwa na kutumbukia majiini.
 
Hakika nahodha UGIMBI alikuwa ni Nahodha hodari Sana hakuna samaki ambaye aliyethubutu kusogelea chombo ya NAHODHA UGIMBI Yani ile mipapa na MINYANGUMI yote sasa imeanza kurudi kwa Kasi kuyumbisha MELI" tuzidishe Dua zetu chombo ya kanali itie NANGA salama.
 
Tuombe Mungu hii isiingie akilini mwa abiria kuwa nahodha wao alishushwa baharini maana kitakachotokea ni tafrani vurugu mechi vuta nikuvute na hata nahodha mpya hatoweza kuhimili chombo tena.
 
Tuombe Mungu hii isiingie akilini mwa abiria kuwa nahodha wao alishushwa baharini maana kitakachotokea ni tafrani vurugu mechi vuta nikuvute na hata nahodha mpya hatoweza kuhimili chombo tena,,
Amina
 
hakika nahodha UGIMBI alikuwa ni Nahodha hodari Sana hakuna samaki ambaye aliyethubutu kusogelea chombo ya NAHODHA UGIMBI Yani ile mipapa na MINYANGUMI yote sasa imeanza kurudi kwa Kasi kuyumbisha MELI" tuzidishe Dua zetu chombo ya kanali itie NANGA salama.
Umofia kwema?
 
Weye zungumza tu.

Taifa la umofia linaongoza kwa idadi ya watu.

Lakini mbona kama msaidizi wa tatu wa nahodha alilia sana alipokosa majibu ya ni sehemu ipi nahodha alijikwaa kabla ya kushuka chomboni na kutumbukia majiini?

Au alishushwa na kutumbukia majiini.
Labda kwenye mwamba mkubwa wa jiwe baharini... Au mawimbi makubwa yalimpa hofu
 
Tuombe Mungu hii isiingie akilini mwa abiria kuwa nahodha wao alishushwa baharini maana kitakachotokea ni tafrani vurugu mechi vuta nikuvute na hata nahodha mpya hatoweza kuhimili chombo tena,,
Tatizo bwana ugimbi alikua mnyanyasaji mno ukimuambia huendeshi chombo vizuri unatoswa baharini. Mwache aende tu acheni ramli chonganishi ugonjwa wa mlipuko ulioyokea karne ya 17 na aliudharau sana na abiria wake wengi waliondoka na hata nahodha mstaafu akaondoka na ule uhonjwa wa mlipuko.
 
Hata Mimi ingali sikumsifia mwanzo kwa kuepuka ujinga wa sifa zile Sasa nitasimama na Ugimbi maana sitaki kuwa sehemu ya wanafiki" alisema mzee @mtwa mkulu wa umofia kwenu.


Ni kipande hiki ndipo umefichua fumbo LOTE mkuu, kama hujui, uandishi wa mafumbo nayo ni taaluma!!!, 🤣🤣
 
Tatizo bwana ugimbi alikua mnyanyasaji mno ukimuambia huendeshi chombo vizuri unatoswa baharini. Mwache aende tu acheni ramli chonganishi ugonjwa wa mlipuko ulioyokea karne ya 17 na aliudharau sana na abiria wake wengi waliondoka na hata nahodha mstaafu akaondoka na ule uhonjwa wa mlipuko.
Basi Kuna habari nyingi huko nchini umofia kumbe kulitokea ugonjwa wa mlipuko?
 
Back
Top Bottom