Tangai saka la masalai pm7, mabadiliko 2013, tishio la kumuua Arusha kwa bomu, kumbeba kwa ndege ya kijeshi na pingu, kufungulia kesi nyingi ili akate tamaa, kumzushia, na sasa kuingiza vita bungeni kwa ajili yake mwenyewe, ujumbe wa mabadiliko 2013 ulikuwa ukimtusi kamanda kama mtu binafsi badala ya kupambana na cheo chake.
Ikulu hatutaingia kama tunakwenda harusini au kwenye maulid, au padirisho au kipaimara, lazima wengi watalia , wataumia na kuumizwa, wengi watatoka nduki na watazusha mengi ili kupaka wenye nguvu kinyesi.
Pm7 wakiwa chini ya ZZK walikuwa na project moja kuhakikisha wanamdoofisha Mbowe kama wa Anga. Hii project Mwigulu, CCM Lumumba project ambayo ilitengeneza kila aina ya sarakasi ili kummaliza Mbowe wakijua wakimdoofisha hakuna mtu mwenye nguvu na anayeweza kustahimili vishawishi vya CCM kama Mbowe.
Hongo, rushwa, na kununuliwa kisiasa ni tunda la umasikini na ukosefu wa ajira, ubunifu na uwezo wa kufanya biashara kisasa. Mbowe ni mbunifu, mfanyabiashara mahiri, mwansiasa hodari na anayo bila ya shaka kuonyesha mafanikio yake.
CCM ikitumia akina ZZK, Dr Kitila, Mchange, Kafulila, Shoza na wengine wengine walijitahidi kuingiza udini, ukabila, ukanda, ugaidi, fujo, nk ili kuidhoifisha CDM, haya yote yalishindwa vibaya sana. Baada ya agents wao kutimuliwa CDM na kuona mbinu zao zote za kuwekeza kwa informer ndani ya CDM inashindikana wakaambia informer na jemederi wao wafanye Character assanation na mtu pekee wakummaliza ni Mbowe kwani ndiye Kizingiki kikubwa sana ndani ya CDM kwasababu ni tajiri mkubwa asiyeyumbishwa na vijisenti vya akina Mwigulu wanavyowapa kina Shoza, Mchange, ZZK, Dr K nk.
Wamejipanga kuhakikisha wanatumia personal attacts. Najua ni siasa za maji taka. Ila lazima CCM, Team ZZK na vibaraka wao wote wajue kwamba hayumbishwi mtu CDM kwa siasa zao chafu. CDM tutaendelea kuprone masalia, na vibaraka wote wa CCM msiba uhamie Lumumba. Hatuwezi kuishi na nyoka ndani. Kama hawa leo waliowahi kujiita CDM ni viongozi wazuri kwanini wasichukue vyumba CCM awe waende kwa Mrema TLP au waungane na Mapesa Udp au Christopher Mtikila kule DP. Inakuwaje leo wote wanataka kumtoa nyongo Mbowe.
Ukweli utabakia Fedha za Mbowe zimesaidia sana kukijenga Chama na kukifikisha hapa kilipo. Ni mbunifu asiye na makuu na aliyekuwa tayari kuwapa wasomi platform ya kujijenga, kujistawisha na kutumia elimu yao vizuri.
Kamati kuu ya Chadema ndio kamati kuu yenye wasomi waliobobea na elimu nzuri na sifa za kutosha kuitwa wasomi kuliko kamati kuu ya chama chochote cha siasa Tanzania. Mbowe akiwa kiongozi mkuu wa Chadema anaamini na aliamini kuwa bila wasomi wenye uwezo wa kitaaluma mambo hayaendi. Viongozi wa Chadema kuna viongozi wasomi vijana, wazee na watu wenye uzoefu unaokubalika. Hii yote ni kazi ya Mbowe kuruhusu haya ndani ya chama hiki.
Wakati huu CDM inapokuwa kwa kasi, wapo baadhi wanajiona wao ni zaidi ya nguvu ya umma, wanasahau kwamba hata CCM inalia sio kwasababu ya Mbowe, Slaa, Lisu nk bali kwasababu ya nguvu ya umma. Wananchi wamejitambua kwasababu ya elimu iliyomwagwa na CDM mitaani. Leo watanzania wanathubu kudai haki zao popote pale walipo , kuanzia mtwara, Lindi, Mwanza, Arusha, tanga, Moro, na kila sehemu ya nchi na kila mwananchi anakiri hii ni elimu ya CDM.
CCM na team ZZK hata mkiweza kumzoifisha Mbowe kama Mbowe kamwe hamtaiweza CDM. Ni wakati mwafaka wakujua kuwa wapinzani wa CDM ni wale wote wenye nia ya kuuwa hiki chama kwa kauli zao, matendao yao, fikra zao na tamaa zao binafsi. Sipendi kabisa kmnyang'anya mwanachama kadi, natamani hii adhabu isiwepo kwenye chama cha siasa ila kuwe na adhabu ya kumzuia mwanachama kutogombea au kuwa kiongozi wa chama kwa muda fulani. Hii adhabu inatosha sana, na kumwacha mwanachama aamue yeye mwenyewe kutoka ama kukaa ndani ya chama. Najua wazi Masalia, PM7, Mabadiliko 2013 hawawezi kuishi ndani ya chama chochote cha siasa bila madaraka.
CDM sio viongozi ni wanachama ambao wao ndio chanzo cha wabunge, madiwani, na chahcu iliyopo sasa. Nawashukuru sana wananchi waaminifu.
Chief Mkwawa
Mbowe ni mwiba wa MaCCM na magent wake, leo wanalia sana kwasababu yake.