Kwa Baraza Hili Tutafika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Baraza Hili Tutafika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kamanzi, Feb 2, 2011.

 1. k

  kamanzi Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  NAzidi kujiuliza maswali kuhusu mustakabali wa nchi yangu Tanzania. Lakini kila nikiliangalia baraza la mawaziri nazidi kukata tamaa. Hawa ni baadhi ya wahusika wanaotakiwa kutupeleka kwenye muongo mpya wa 2011-2020.

  1) Dr Dr Dr Kikwete: Huyu anahusika kwa njia moja au nyingine na kashfa za Richmond na DOWANS. Ni rafiki wa mafisadi na Dr Hosea wa TAKUKURU alishasema amempa amri asijaribu kushughulikia mafisadi halisi. Katika kuitumia familia kuhodhi nchi, amemzidi Mkapa (unamkumbuka mama Mkapa?) na Mwinyi (mnamkumbuka mama Sitti Mwinyi)

  2) Makamu wa Rais Gharib: Huyu nalikuja na gia nzito ya kuhakikisha waislamu wanapata mahakama ya kadhi. Hoja imefifia na si tu kawadanganya waislamu bali hata maelezo kwa nini alifanya hivyo hajatoa. Kwa kuzingatia ukosaji kazi wake, Dr Dr Dr Kikwete alimshauri awe anafundisha UDOM

  3) Pinda: Huyu bwana anachojua ni kulia lia tu. Watu wanamuita mtoto wa mkulima lakini wanasahau kuwa baada ya akina Lowasa kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, alienda Igunga akawaambia wapiga kura kule kuwa "achaneni na mambo ya bungeni, Rostam ni mtu mwema"

  4) Sitta: Huyu bila huruma ametumia shilingi milioni 850 kujijengea ofisi Urambo. Ni huyuhuyu aliyeshiriki kumsimamisha ubunge Zitto Kabwe wakati huo Zitto alikuwa akijitambua bado

  5) Magufuli: Huyu anakashfa ya kuuza nyumba kwa bei chee wakati akiwa waziri wa Ujenzi. Inasadikika alimpa madeal mengi kaka yake pia wakati huo.

  6) WAziri wetu wa fedha: Fisadi namba moja aliyehusika kwenye kashfa wakati akiwa mkurugenzi wa mfuko mmoja wapo wa jamii.

  7) Wassira: aka Tyson, ni kikongwe anayesifika kupiga watu ngumi pila kuwa na uwezo kiutendaji.

  8) Nyalandu: Kahaba fisadi ambaye habari zake zitazirudia maana zimeandikwa kwa kirefu kwenye threads zingine

  9) Nchimbi: Fisadi anayehusishwa moja kwa moja na kumdhibiti marehemu mtoto wa Malecela alipokuwa akitayarishwa kuingia UVCCM

  10) Ngeleja: Wakili wa Rostam (Vodacom) asiyejua aibu inapokuja kupigania maslahi ya BOSI wake (rostam)

  11) Nahodha: Kamanda aliyesimamia mauaji ya zaidi ya wapemba 20 wakati wa kipindi cha udikteta wa Mkapa na Salmin

  12) Membe: Mtu mwenye uchu wa madaraka ambae yupo radhi kuwadanganya waislamu kuwa atawapa OIC kama zawadi ikiwa wataendelea kumkubali

  13) Sina haja kuwaongelea vimwana akina Kabaka, Kombani na mamah mwenyekiti wa wakinamama wa CCM ambao kazi yao ni kuimba taarabu na kumpa sifa Dr Dr Dr Kikwete.

  Anaedhani nchi hii itakuja kuendelea ni aidha MLEVI au AKILI YAKE HAINA AKILI
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbona umeingia na jazba baada ya kupotea muda wote huu? Nyingi ya assessments zako ni za ovyo na ambazo hazina vigezo. Zimeegemea zaidi kwenye chuki yako dhidi ya am serikali au baadhi ya mawaziri hao. Chimba zaidi ili tupate data za uhakika mkuu!
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  Achimbe ninitena wakati data kakumwagia hapo nanyingi zinaukweli tanzania ya sasa tofauti na uliyoizoea sikuhizi hatudanganyikiiiii!!!!!
   
 4. m

  mkulu Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  inawezekana unayosema yakawa na ukweli ndani yake but hujui kujenga hoja, na wala maelezo yako hayawezi kumconvince mtu!!Maelezo yako yameongozwa na hisia zaidi
   
 5. HIMO ONE

  HIMO ONE Senior Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maelezo yake yamejitosheleeza na amefikisha ujumbe barabara,sema wapo watu ameacha kuwataja ambao wanaizamisha Tanzania waziwazi

  -Mathias Chikawe
  -Shukuru Kawambwa
  -Sophia Simba
  -Mustafa Mkulo
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nimeanza kuamini kwamba humu chumbani wengi tunaongea kishabiki sana kuliko kauli mbiu ya room(DEEP THINKERS). Kaka mbona umejaribu ku pick cream ya CCM na kuipaka matope ili mradi tu wenye kuona karibu kama ww tusiweze kugundua kuwa unawachafua VICE PRESIDENT PM, SITTA, MAGUFULI, NYALANGU MEMBE na wengine. Kwa nini umetumia sana walinganya waislamu? bora ungetumia kiswahili cha wameshindwa kutimiza ahadi zao! Hivi mke wa SLAA alijipaka rangi kule Arusha na kudai kuwa ni damu ya risasi za polisi yeye akiwa kama mwana-CHADEMA au fisrt lady? . Ama kweli kazi tunayo wana jamii forums kuchambua pumba na jamii ili hata pale tunapowasimulia wengine angalau waambulie kitu na kutuona kama mwanga kwa jamii.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Amemtaja mkulo kama waziri wa fedha na Sofia Simba kama Kimwana. Huyu bwana Kamanzi amekaaa kitaa sana. nadhani kuingia humu room ni kama ameingia choo cha kike.
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0


  Mary Nagu mbona umemwacha?

  Tibaijuka je?
   
 9. m

  mzambia JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Shamsa mwangunga
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kamwe hutabaki kuna mtu mwema na msafi kama hujaanza kujikosoa wewe mwenyewe kwanza. mwaga hapa udhaifu wako ndipo tutakuwa na nafasi ya kuchambua pumba na mchele.
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Inaonekana kwa mtazamo wako binadamu wamekamilika kama malaika hata wale waliofanya vizuri kama Sitta au Magufuri nao umewatilia mashaka, yupi kwako atakuwa safi. maana yangu sio kwamba Sitta au magufuri hana kasoro la hasha lakini hata wakiingia chadema bado makosa ya kibinadamu watakuwa nayo. Kama kiongozi atafanya mazuri asilimia 90 na mabaya asilimia 10 basi huyu tumuweke kwenye kundi la waliojitahidi kufanya mema.
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Post hii imekaa kisiasa ingekuwa vyema kama ungeleta hoja ya kumchambua waziri mmoja mmoja huku tukianisha mazuri na mabaya yake kisha tungepima uwezo wa kila waziri wa kuwatumika watanzania. Unaweza kuwa unamfahamu kiongozi kwa mabaya tu lakini kumbe kunaweza kuwa na mtu hapa JF akatufahamisha na mazuri yake.
   
 13. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hapo pekundu - Hiyo kweli, kweli yote na kweli tupu?
   
Loading...