MartinCoder
JF-Expert Member
- Feb 20, 2018
- 700
- 630
(kama wafanyavyo baadhi ya watu): chukulia ni wewe umenunua kiwanja ambacho hakijapimwa kwa bei shilingi milioni nane (8,000,000/=), halafu katika kufanya mchakato wa kupata hati ya kiwanja hicho mkakubaliana wewe na aliyekuuzia kiwanja kuwa mseme mauziano yalikuwa milioni mbili (2,000,000/=) kwa lengo la kukwepa 15% au 10% ya 8,000,000/=; kwa maana hiyo mtalipa 15% au 10% ya 2,000,000/= katika ku-process hati. Sasa baada ya muda(mfano miezi mitatu) ikabainika lile eneo lote (kikiwemo kiwanja chako) linahitajika na selikali kwa shughuli maalum; hivo ukahitajika ulete hati na documents nyingine zinazoonesha thamani uliyonunua kiwanja; itakuwaje wakati uliongopa!!!!!!!!!!! si hasara ya kujitakia