Kwa aneyetambua hospitali yenye mpiga ultrasound wa kike

JAMBONIA LTD

JF-Expert Member
Jan 22, 2014
576
263
Habari zenu wadau wa JF dokta...

Natafuta hospitali au kituo cha afya ambacho anayepiga picha za ultrasound hasa kwa akina mama ambaye naye ni mwanamke..

Kwa anayeijua anijuze tafadhali kwani nimetafta sana hapa dar ila bado cijafanikiwa....
 
Usitafute jinsia,tafuta maarifa na ujuzi.Hicho kipimo ni subjective kwa maana kinategemea kisomo na uzoefu.Ukampata kanjanja eti kwa vile ni mwanamama,anaweza kwambia mkeo ana ujauzito miezi mitano,kumbe ni uvimbe unaohitaji upasuaji wa haraka!
 
Ukiwa mjinga wa kuficha uchi wako au wa mkeo hata labour hutampeleka . wanaume wengi na masistaduu wanajifanyaga wako wanaficha nyuchi zao/za wapenzi wao. Na ukiona mtu anayeulizia jinsia ya mhudumu basi ujue haumwi au hana uhitaji wa kipimo. Mi huwa sielewi hata kinachofichwa ni nini! Na kibaya zaidi watu wazuri na wanaokubalika kwa kudeal vizuri na mambo ya wanawake ni wanaume.
 
Habari zenu wadau wa jf dokta..natafuta hospitali au kituo cha afya ambacho anayepiga picha za ultrasound hasa kwa akina mama ambaye naye ni mwanamke..kwa anayeijua anijuze tafadhali kwani nimetafta sana hapa dar ila bado cijafanikiwa....

kuna clinic moja nzuri sana ila jina nimesahau kwa maelezo unaweza kufika, ipo muhimbili mbele ya gate la mochwari(sio mkabala na gate) upande wa kushoto utaona bango
 
unatafuta jinsia ya ke au unatafuta docta mzuri wa kukuhudumia
 
Back
Top Bottom