Kwa android phone security: Je kuna tracking app/software yoyote inayoweza kukwepa 'factory/hard reset'?

kayanda01

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
1,086
913
Wakuu na wataalaamu wa phone security,

Nini mtu afanye ili kuiwekea ulinzi smart phone ili itakapoibiwa ama kupotea aweze kuitrack?

Wezi wanaflash (factory reset) na kubadili IMEI number. IMEI NUMBER inapokuwa changed, habari kwishney, polisi wanakuwa hawana msaada wowote tena.

Je, kuna tracking app yenye uwezo wa kutoathirika na IMEI number change or hard reset? Mfano hizi simu za android family kama vile INFINIX, etc

Tupeane maujanja wakuu. Wizi wa simu unashamiri!! hasara inakuwa kubwa sana kwa wahanga.
 
Security interventions kwenye android smart phone KABLA haijapotea/haijaibwa.
 
Hata ikiwepo haitasaidia, simu nyingi za wizi zinasambaratishwa na kuuzwa kama spare parts

Rejea iPhone, zina iCloud lock ambayo unaweza activate ikiibiwa, lakini wapi, haisaidii, simu kesho yake ishasambaratishwa unakuta spare za kioo kule mtaa wa Aggrey
 
hata ikiwepo haitasaidia, simu nyingi za wizi zinasambaratishwa na kuuzwa kama spare parts

rejea iPhone, zina iCloud lock ambayo unaweza activate ikiibiwa, lakini wapi, haisaidii, simu kesho yake ishasambaratishwa unakuta spare za kioo kule mtaa wa Aggrey

Sawa. Ila nadhani kuna maeneo ya huko mikoani pembezoni mwa townships, hizo njia kama zipo zaweza kuwa msaada.

Kuna mtu anaokota simu na anaaza kuitumia yeye mwenyewe. Pia kuna maeneo (mbali na majiji) wezi washamba wapo, anaiba na kuflash au kubadili IMEI number kisha anamuuzia mtu.
 
pembezoni mwa townships
Hizo townships ni za watu wenye kipato cha chini/kati wenye uwezo wa kununua Infinix, Tecno, simu zenye SoC ya ovyo kabisa, SoC yenye modem ambayo unabadili IMEI on the fly

kwakua SoC ni ya ovyo, hakuna namna yoyote ya kuweka ulinzi humo
 
Hard reset na factory reset unaweza kama utaigeuza anti theft kuwa system app sema njia hii inahitaji uwe na root access, akiflash nayo inakwenda na maji.

Kuanzia android za karibuni kuna mambo ya partition kwenye Android sijajua kama unaweza tumia hizi partition kutrack simu maana unapoflash partition moja tu ndio inafutika. Hili linahitaji research zaidi.
 
Mkuu tumia simu kama iphone na baadhi ya simu za Android ambazo huwezi kufanya hiyo kitu kama Samsung matoleo ya juu na Huawei kama sijakosea

Hizi simu za kichina kama Tecno itel na jamii zake huwezi

Uki root simu zipo app ambazo hizo app hazitoki uki hard rest lakini kwa mtaalamu anazifuta
 
Hard reset na factory reset unaweza kama utaigeuza anti theft kuwa system app sema njia hii inahitaji uwe na root access, akiflash nayo inakwenda na maji.

Kuanzia android za karibuni kuna mambo ya partition kwenye Android sijajua kama unaweza tumia hizi partition kutrack simu maana unapoflash partition moja tu ndio inafutika. Hili linahitaji research zaidi.

Naomba elimu zaidi kwenye hiyo njia ya kwanza ya kutumia anti-theft with root access.
 
Mkuu tumia simu kama iphone na baadhi ya simu za Android ambazo huwezi kufanya hiyo kitu kama Samsung matoleo yajuu na Huawei kama sijakosea

Hizi simu za kichina kama Tecno itel na jamii zake huwezi

Uki root simu zipo app ambazo hizo app hazitoki uki hard rest lakini kwa mtaalamu anazifuta

Mkuu, kuanzia Samsung model gani hiyo
 
Kusajili 'google account' , Je itanipa security mpaka level gani?
 
Cerberus ni app husika inafanya hii kazi ila ni ya kulipia. Simu ukiwa umeiroot itaomba root access kujiunga n rom yAko.

Cheers mkuu. Usichoke kutupa mwanga.

Hivi vitu vinne vinanichanganya kuvielewa vyema (nimejaribu kugoogle lakini bado vinanichanganya): HARD RESET; FACTORY RESET; FLASHING; IMEI CHANGE... ni kitu kile kile? au ni procedures tofauti?

If ni procedures tofauti, Cerberus (with root access) ina uwezo wa kusurvive all of them?
 
cheers mkuu. Usichoke kutupa mwanga.

Hivi vitu vinne vinanichanganya kuvielewa vyema (nimejaribu kugoogle lakini bado vinanichanganya): HARD RESET; FACTORY RESET; FLASHING; IMEI CHANGE... ni kitu kile kile? au ni procedures tofauti?

If ni procedures tofauti, Cerberus (with root access) ina uwezo wa kusurvive all of them?
Hard na factory reset inaweza maanisha kitu kimoja, hii ni kuifanya simu ifute vitu vyote irudi kama ilivyokuwa.

Kuflash ni kubadili operating system
iliokuja na simu kwa kuweka os mpya ama ile ile.

Kubadili imei ni jambo jengine kabisa, simu huja na no ambazo ni Unique ili kuwasiliana na mitandao ya simu zinaitwa Imei, huwa simu za wizi watu wanabadili wasidakwe. Ni kosa kisheria kuzibadili.
 
Back
Top Bottom