Kwa anayejua ufaulu unaohitajika Ilboru, Kisimiri au Tabora boys

Samahani ndugu zangu!

Naomba kuuliza, Kuna dogo langu amepata division one ya 8, ila combination anazotamani kusoma yaan PCM,PCB na PGM, ufahulu wake ni (CAA) make Physics ana "C " afu hayo masomo ni "A".

Swali langu ni je anaweza kupata nafasi kwenye hizo shule za vipaji maalumu?
Kama ana C ya physics O level na ufaulu wake huo nahisi Hilo somo litamtesa huko mbele, kwa nn asisome CBG?? manake A level physics mziki wake mnene sana, ni ushauri wangu tu
 
Pambana aende Kibaha boys kama connection ipo, utanishukuru baadae, japokuwa mimi nilisoma Ilboru
 
Kwa special school hawezi kwenda kwa sababu ya C yake ya physics labda kwenye selform angejaza comb ambazo amepata AAA zinazopatikana ktk hizo special school mfano hgl tabora boys lazima angechaguliwa tu then akifika shuleni abadilishe aende comb anayoitaka
 
Mambo yanabadilika mkuu usikariri mim nilisoma na jamaa advanced level......huyo alikuwa wa kawaida sana kwenye namba(hesabu) na alipata C NECTA form four ila advanced level akaja kuuwasha vibaya yaan akatoka na A ya advanced maths A level
 
Samahani ndugu zangu!

Naomba kuuliza, Kuna dogo langu amepata division one ya 8, ila combination anazotamani kusoma yaan PCM,PCB na PGM, ufahulu wake ni (CAA) make Physics ana "C " afu hayo masomo ni "A".

Swali langu ni je anaweza kupata nafasi kwenye hizo shule za vipaji maalumu?
Kwani lazima akosome kwenye hizo shule?; Kwanini uumize kixhwa mtoto asoma shule flani wakati shule zipo nyingi nchi hii?! Wewe tafuta Ada mpeleke mtoto kwenye shule iwe private au Serikali atafanya vizuri tu.

Watu wengi unaowaona nchi hii wenye mafanikio (wafanyakazi Wa Serikali, wanasiasa, wafanyabiashara, wafanyakazi private sekta, etc etc) wametokea shule zingine nyingi tu nchi hii nje ya hizo ulizotaja. Achana na mawazo mgando ya miaka hiyo.

Tafuta hela mwezeshe mtoto asome akiwa na nahitaji yote muhimu ya shule, hata shule za Kata anatoboa. Almradi umsimamie vizuri.
 
Mambo yanabadilika mkuu usikariri mim nilisoma na jamaa advanced level......huyo alikuwa wa kawaida sana kwenye namba(hesabu) na alipata C NECTA form four ila advanced level akaja kuuwasha vibaya yaan akatoka na A ya advanced maths A level
Alikuwa PCM au EGM
 
Kwani lazima akosome kwenye hizo shule?; Kwanini uumize kixhwa mtoto asoma shule flani wakati shule zipo nyingi nchi hii?! Wewe tafuta Ada mpeleke mtoto kwenye shule iwe private au Serikali atafanya vizuri tu.

Watu wengi unaowaona nchi hii wenye mafanikio (wafanyakazi Wa Serikali, wanasiasa, wafanyabiashara, wafanyakazi private sekta, etc etc) wametokea shule zingine nyingi tu nchi hii nje ya hizo ulizotaja. Achana na mawazo mgando ya miaka hiyo.

Tafuta hela mwezeshe mtoto asome akiwa na nahitaji yote muhimu ya shule, hata shule za Kata anatoboa. Almradi umsimamie vizuri.
shule zinatofautiana ubora ndugu ndo maana zimeitwa special
 
Kwa ufaulu huo anasoma shule yoyote ile aitakayo Tanzania, hata kwa CBM/G then badae arudi PCM. Nakumbuka mwaka 2013 kisimiri na Ilboru walipokea hadi 2.18 sasa 1.8 akose sio kweli
Hahaha sio na PCB na PCM,kisimiri hiyo 2013 haikupokea div 2 yaani fikiria shule Kama minaki 2013 pcm waliingia wote na div 1
 
Back
Top Bottom