CCM imetufikisha hapaaaaa!!! Jamani, wakuu wangu, viongozi wangu mliotuambia Maisha Bora kwa kiiiila Mtanzania... Tangu 2005 hadi leo. Tunasota, tunakaangwa, Kiwete Baba, siku moja moja pitia hili jamvi la walala hoi.
Milioni moja nikae nayo siku thelathini nilipe milioni na laki mbili na hamsini elfu. Baba Kikwete, nitaifanyia biashara gani ili iniletee hiyo riba?? Yaani hili ni tatizo juu ya tatizo jingine tu. Tutafanyaje, na hii ndo Tanzania yetu sote? Ya wenye nazo na wanaotegemea shida zetu ili warefushe ile pengo kati yetu na wao?? Wanaendelea kula matawi ya juuuu.
Huyo mwenye gari akikupa hiyo kadi, si inamaana amekuwa mtumwa wako? Haya Baba K, Tanzania yako kuna walio huru na waliojiuza utumwani humu humu TZ.