Kwa aliyosema Ole Sendeka leo, Zitto tupe majibu!

Kwa aliyosema Ole Sendeka leo, Zitto tupe majibu!

sonaderm

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2015
Posts
618
Reaction score
1,817
Mh Ole Sendeka leo alikuwa na mkutano na waandisi wa habari na moja ya kitu kilichonishtua ni tuhuma kuwa Zitto ana urafiki na baadhi ya wezi na kuwakingia kifua kipindi akiwa kiongozi wa kamati fulani bungeni..

Naweza kusema tuhuma hizi ni nzito na ningemuomba bwana Zitto atueleze wana ACT-Wazalendo juu ya tuhuma hizi kama ni kweli, pili utueleze kama uko teyari akaunti zako za benki na mali zako zikaguliwe ili kuweza kupata usahihi wa yaliyosemwa na ndugu Sendeka..Kama kuna mengine wazalendo wenzangu watasema ila mimi nimeishia hapo kwa sasa...

 
Zito anayo yakujibu ! Aje hapa atuambie ukweli. Zito kaiweka ACT kikaangoni!
 
Ole sendeka ni nani ndani ya serikali hii mpaka, mpaka zimtoe zitto kujibu hizo tuhuma mafumbo zake..!!??

Kama ni kweli Sendeka angewataja hao watu kwa majina kama alivyo weza kumtaza Zitto kwa jina...

Pili Zitto mali zake zote alishaziweka waz na Act inazijua kama ilivyo kwa viongoz wengine wote ndani ya Act, kusema leo akaguliwe account zake, sio jambo baya lkn ni account zake zipo waz na Act inazifaham sio yeye pekee na viongoz wenzake wote ndani ya chama.....

Ole sendeka afanye kazi aliokuwa nayo sio kutafuta vitu ambavyo hana uhakika navyo.....
 
Mh Ole Sendeka leo alikuwa na mkutano na waandisi wa habari na moja ya kitu kilichonishtua ni tuhuma kuwa Zitto ana urafiki na baadhi ya wezi na kuwakingia kifua kipindi akiwa kiongozi wa kamati fulani bungeni..

Naweza kusema tuhuma hizi ni nzito na ningemuomba bwana Zitto atueleze wana ACT-Wazalendo juu ya tuhuma hizi kama ni kweli, pili utueleze kama uko teyari akaunti zako za benki na mali zako zikaguliwe ili kuweza kupata usahihi wa yaliyosemwa na ndugu Sendeka..Kama kuna mengine wazalendo wenzangu watasema ila mimi nimeishia hapo kwa sasa...
hakuna yeyote (pigia mstari yeyote) aliyeko ndani ya CCM mwenye moral authority ya kuwasema wapinzani (the lesser of the two devils).
 
Ni vema tuhuma Zikajibiwa na ninavyomjua ZZK hatokaa kimya kwenye hili.. Hata kama hatokuja kwenye platform hii ataZijibiasehemu nyingine. La muhimu tuhuma ni muhimu kujibiwa.
 
Sasa Kama chama kinacho tawala kina lalamika na kutoa tuhuma kama chama cha upinzani, are they serious my brother?

Mbona mlitwambia mnao ushahidi wa rich mond mpka sasa hamuutoi na wala kuwapeleka mahakamani hamtaki?

Mtu yeyote aliye timamu kiakili hawezi amini tena tuhuma zinazo tolewa na serikali hii dhidi ya upinzani.
 
Sendeka anabwabwaja tu kwani yy ni nani kama kweli kaamua kusema basi awataje hao ambao zitto anawakingia kifua
 
Katu interest yangu haiwezi kuwa dhidi ya Zitto bali serikali ya CCM ambayo Ole Sendeka ndie msemaji wake...! Serikali ya Sendeka imefanya nini hadi sasa dhidi ya hao wezi waliokuwa wanakingiwa kifua na Zitto manake siamini kwamba Zitto ana maguvu kuliko serikali mzima ya CCM na kama ana maguvu hayo basi itakuwa ni serikali iliyopoteza uhalali ikiwa mbunge mmoja anaweza kuwakingia kifua wezi dhidi ya serikali mzima!
 
Zitto Mtoto wa kigoma uwa akubari kushindwa kama sendeka kamwaga unga wewe toka umwage mboga kuanzia kivuko cha bagamoyo mpaka bombadia
 
Kwa hapa Sendeka kawakuna CDM...

Atapata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa CDM hata hata kama hoja aliyoitoa haina mashiko.
 
Mwenye biti ya ccm mbele kwa mbele ani pm niitumie kuimba mie nipunguze stress
 
Wakati mwingine ukimsikiliza au ukasoma alichoandika mtu unaweza kisia ufaulu wake shuleni au chuoni kwani unauona uwezo wake wa kujenga hoja.
Sishangai sana maana matokeo yake ya kidato cha sita yalushawekwa wazi humu.
Na wakati huo ndo kichwa kilikuwa swaaafi kinadai. Je sasa kimechoka ndani na nje unategemea nini?
 
Sendeka acha siasa uchwara, serikali ya ccm ina jeshi,polisi,mahakama ya mafisadi na .....kama usemalo ni kweli kwa nini msimkamate na kumuweka ndani
 
Back
Top Bottom