ACT Wazalendo yamjibu Ole Sendeka, yasema mali, madeni, maisha ya Zitto yako wazi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kimeshtushwa na tuhuma dhidi ya kiongozi wake wa chama, Zitto Kabwe kwamba ana miliki mali za kifisadi pamoja na kuhusishwa na ununuzi wa ardhi maeneo ya Kigamboni uliofanywa na NSSF kwa bei ya milioni 800 kwa ekari moja, wakati bei halisi ni milioni 25 na kwamba kitendo hicho kimeitia hasara serikali .

Tuhuma hizo zilitolewa jana na Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Christopher Ole Sendeka, ambapo alivitaka vyombo vya uchunguzi kufanya uchunguzi katika shirika hilo ili kubaini waliohusika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria, huku akimhusisha Zitto katika uchunguzi huo.

Ole Sendeka alitaka akaunti za benki za Zitto pamoja na maisha yake binafsi kuchunguzwa kama yana uhalisia na kipato chake halali.

Tuhuma hizo zimekiibua chama cha ACT, ambapo leo Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa ACT, Habibu Mchange amevitaka vyombo vya uchunguzi haraka iwezekanavyo kuchunguza mali, madeni, akaunti zote za benki pamoja na mfumo wa maisha ya Zitto.

“ACT imeshtushwa na tuhuma, kashfa, porojo na matusi mbalimbali yaliyotolewa jana na Ole sendeka dhidi ya kiongozi wa chama chetu,” amesema.

Amesema kuwa, katiba ya chama hicho huwataka viongozi wote kuweka hadharani matamko ya mali zao na madeni na kwamba Zitto alitekeleza matakwa hayo ya kisheria hivyo mali na madeni yake yako hadharani na mtandaoni.

“Tunaamini kama kuna kiongozi ambaye mali, madeni, maslahi, na akaunti zake viko wazi basi ni ndugu Zitto,” amesema.

Aidha, Mchange amedai kuwa, kilichomsukuma Sendeka kutoa tuhuma hizo kwa Zitto ni harakati zake za kuupinga muswada mpya wa habari.

“Tuhuma za olesendeka kuna kitu nyuma yake, jitihada za zito za kupambana na mswada wa habari ndizo zilizomuibua, sababu wanataka upitishwe ili kuviua vyombo vya habari,” amesema.

Amesema ACT itaendelea kuisimamia serikali katika mambo ya bungeni kama anavyofanya mbunge na kiongozi wao wa chama.

Chanzo: Dewji Blog
 
Hivi fisadi anatakiwa awe wapi.. CCM fanya mambo kiakili mlisema lowasa fisadi bado yuko mtaani leo zitto. INA maana nyie tumewakabidhi dola na HAMWEZI kuitumia
 
Hivi mwenye akili timamu anaweza kuliamini hilo tamko la mali na madeni linalofanywa hadharani na mhusika kwa asilimia 100%?
Si anaweza kuwa ameficha zingine? Anaweza akawa na account kwenye mabenki ya Uswizi na asiyatolee tamko na kadhalika. Kwani zile Hammers zinazosemwa semwa alizitaja kwenye hilo tamko?

Kwa nini mwandishi wa hii habari una wasi wasi kwa wataalamu kufanya uchunguzi wa kitaalamu kuhusiana na mali yake? Kwanza ni kwa faida yake kisiasa atakapokuwa cleared na uchunguzi huu.
 
Aiseee kwanza niseme kwanza habari ya Jana kama ilikosewa vile maana mtangazaji alisema chama cha mapinduzi kimeongea na vyombo vya habari kuhusu tathimini na mafanikio ya Raisi kwa mwaka mmoja Salio kaa madarakani cha ajabu sikusikia hiyo tathimini zaidi ya shutuma kwa vyama vya upinzani kwamba wanaopinga anayoyafanya Raisi ni makapi duh!
 
Hivi mwenye akili timamu anaweza kuliamini hilo tamko la mali na madeni linalofanywa hadharani na mhusika kwa asilimia 100%?
Si anaweza kuwa ameficha zingine? Anaweza akawa na account kwenye mabenki ya Uswizi na asiyatolee tamko na kadhalika. Kwani zile Hammers zinazosemwa semwa alizitaja kwenye hilo tamko?

Kwa nini mwandishi wa hii habari una wasi wasi kwa wataalamu kufanya uchunguzi wa kitaalamu kuhusiana na mali yake? Kwanza ni kwa faida yake kisiasa atakapokuwa cleared na uchunguzi huu.
Nilifikiri kwa vile ni Dr basi utakuwa na werevu japo kidogo,kumbe wewe ni sawa na wale wakina Dr manyaunyau!.

Kama katika hizo mali alizoainisha na madeni pamoja na akaunti ni za uongo na vingine kaficha mnashindwa kumchukulia hatua wakati mna dola?.

Mmekabidhiwa dola ili kushughulikia watu waongo,wanafiki na mafisadi kama huyu Zitto mnashindwa vipi kumchukulia hatua?.

Tume ya maadili kwa watumishi wa uma siipo,mnashindwa kwenda kuangalia Mali huko alidhoorodhesha mkajiridhisaha kama kasema ukweli au laa ili mumchukulie hatua hatua huyu fisadi aliejificha kwenye mashirika ya uma?.

Ama kweli njoo Tanzania uone maajabu ya madaktari wa huku!.
 
Ccm wameshapanic, wameona anaingia anga zao wanataka kumpooza,,Zito hana rafiki anapiga kotekote
 
Zitto aje aseme pesa za kusimamisha wabunge nchi mzima alipata wapi?....

Aseme kwanini mwanzo alikuwa anamuunga mkono magufuli katikati akabadili gia angani?.....

Tatizo lake ni maslai binafsi kuliko nchi
Kwa ujumula na yeye ni fisadi.........
 
Ndio maana tunasema siasa mchezo mchafu nakumbuka jinsi alivyo kuwa beneth na chama tawala hata kipindi cha uchaguzi waliakaa meza moja kisirisiri kuhakikisha ushindi unapatikana kwa hali na mali. Sasa leo hii wamegeukana.
 
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kimeshtushwa na tuhuma dhidi ya kiongozi wake wa chama, Zitto Kabwe kwamba ana miliki mali za kifisadi pamoja na kuhusishwa na ununuzi wa ardhi maeneo ya Kigamboni uliofanywa na NSSF kwa bei ya milioni 800 kwa ekari moja, wakati bei halisi ni milioni 25 na kwamba kitendo hicho kimeitia hasara serikali .

Tuhuma hizo zilitolewa jana na Msemaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Christopher Ole Sendeka, ambapo alivitaka vyombo vya uchunguzi kufanya uchunguzi katika shirika hilo ili kubaini waliohusika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria, huku akimhusisha Zitto katika uchunguzi huo.

Ole Sendeka alitaka akaunti za benki za Zitto pamoja na maisha yake binafsi kuchunguzwa kama yana uhalisia na kipato chake halali.

Tuhuma hizo zimekiibua chama cha ACT, ambapo leo Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa ACT, Habibu Mchange amevitaka vyombo vya uchunguzi haraka iwezekanavyo kuchunguza mali, madeni, akaunti zote za benki pamoja na mfumo wa maisha ya Zitto.

“ACT imeshtushwa na tuhuma, kashfa, porojo na matusi mbalimbali yaliyotolewa jana na Ole sendeka dhidi ya kiongozi wa chama chetu,” amesema.

Amesema kuwa, katiba ya chama hicho huwataka viongozi wote kuweka hadharani matamko ya mali zao na madeni na kwamba Zitto alitekeleza matakwa hayo ya kisheria hivyo mali na madeni yake yako hadharani na mtandaoni.

“Tunaamini kama kuna kiongozi ambaye mali, madeni, maslahi, na akaunti zake viko wazi basi ni ndugu Zitto,” amesema.

Aidha, Mchange amedai kuwa, kilichomsukuma Sendeka kutoa tuhuma hizo kwa Zitto ni harakati zake za kuupinga muswada mpya wa habari.

“Tuhuma za olesendeka kuna kitu nyuma yake, jitihada za zito za kupambana na mswada wa habari ndizo zilizomuibua, sababu wanataka upitishwe ili kuviua vyombo vya habari,” amesema.

Amesema ACT itaendelea kuisimamia serikali katika mambo ya bungeni kama anavyofanya mbunge na kiongozi wao wa chama.

Chanzo: Dewji Blog
Kama yapo wazi mbona ZITTO anaishi kwa kujificha ficha? ????
 
Kama kuna kitu kibaya alichofanya ZZK amefanya akiwa na hao watawala. Kuna taarifa nyingi kwamba ZZK alitumiwa na akatumika. Miaka kama mitano au sita nyuma kuna gazeti liliandika jinsi alivyokuwa akichukua mamilioni ya pesa. Pesa nyingine ilibidi zipitie kwa mama Mmoja huko Ujerumani. Pia kuna mawasiliano yalinaswa akiwasiliana na kiongozi wa juu wa usalama wa Taifa kipindi cha uchaguzi mkuu 2010. Pia kuna taarifa kuwa ile kampuni yake ya kukuza vipaji au kuendeleza wasanii alichota mamilioni kwenye hiyo mifuko. Wasanii waliotokea Kigoma walilalamika kuwa hawafaidi chochote na kampuni hiyo kwani walitumiwa tu. Mipango ya kuipasua Chadema ndani ya chama ilishindikana, akaanza mikakati ya kuipasua chadema nje ya chadema. Hapo ndipo alipoanzisha ACT Tanzania baadate akabadilisha kuwa ACT Wazalendo.

Alikuwa anapata sapoti yote kwenye serikali ili malengo yao ya kisiasa yatimie.

Hivyo sitamshangaa Ole Sendeka akimtuhumu kuwa ni fisadi lkn ukichunguza huo ufisadi ulikuwa wa ushirika au ubia. Mmoja alikuwa anafaidika na pesa na mbia mwingine alikuwa na matarajio ya upinzani kuvurugwa hususani chadema.
Hivyo ZZK alishaacha siasa za upinzani tangia mwaka 2008 alipokubali kununulika.
 
Back
Top Bottom