Kwa akili hizi umaskini utatuondoka?


Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,698
Points
2,000
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,698 2,000
Kwa miaka kadhaa hapa Tanzania imekuwepo sheria ya Mabasi ya Abiria kutotembea usiku. Sheria hii inavyoonekana ipo hapa Tanzania tu kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati na imekuwa kikwazo kwa biashara za ndani na zile nchi jirani kwani inapunguza uwezo wa wafanyabiashara kusafiri kwa wakati.

Sababu kubwa za serikali yetu kutekeleza mfumo huu ni USALAMA. Asubuhi hii, kamanda wa Vikosi vya Usalama barabarani Kamishna Mpinga akiongea na Radio One amesema, ni kweli kuwa nchi jirani magari ya abiria yanatembea masaa 24 lakini kwa Tanzania imekuwa ni changamoto kwa kuwa nchi yetu ni kubwa ukilinganisha na Kenya na Uganda, Kongo na Rwanda.

Swali la kujiuliza ni hili; hii Tanzania ni kubwa kwa ardhi tu?

Idadi ya watu ni sawa na Kenya na Uganda? Rasilimali ni sawa na Kenya na Uganda? Jeshi letu ni sawa na Kenya na Uganda?

Hapa utaona kuwa sisi ni watu tusiokosa sababu kwa madhaifu yetu. Mimi binafsi sioni sababu ya majambazi kutufanya tujifiche ndani kwa kuhofia mabasi yatatekwa. Huko Kenya, kwa wafanyabiashara watakubaliana na mimi, ukipita usiku, utaona Road Blocks na wanajeshi wakiwa na taa zao pembeni wapo pundamilia wakila maganda ya machungwa na hali ya usalama wa barabara ni shwari.

Sisi tunaotembea mchana, wastani wa ajali za barabarani kwetu bado upo juu na tunakufa mchana huo huo. Binafsi sielewi kuona POLISI NA JESHI WANAWEZAJE KUTUMIWA KUTULIZA MAANDAMANO LAKINI UKASHINDIKANA KUPATIKANA UTARATIBU WA KUTULINDA TUKAFANYA BIASHARA ZETU KWA UHURU.

Wengi yawezekana msione umuhimu wa hili, lakini mimi niliwahi kuwa mwajiriwa na mfanyabiashara kwa wakati mmoja. Biashara ilikuwa ngumu sababu ya utaratibu huu mbaya. Laiti kama tungefanya kama wenzetu, basi kulikuwa kuna uwezekano wa mimi kutoka DAR usiku, nikaingia Mombasa asubuhi, nikafunga mizigo yangu mchana kutwa, na usiku nikaingia tena safarini asubuhi ikanikuta Dar na nikafungua duka langu na kuendelea na biashara zangu. Lakini piga picha inanichukua muda gani kukamilisha zoezi lile lile kwa utaratibu huu uliopo?

Mimi nafikiri umefika wakati wa serikali kuacha hii primitive attitude na kuishi kwa malengo. Haiwezekani changamoto za namna hii ziitwe sababu muafaka za sisi kuwa nyuma na tukachekelea. Tanzania si kubwa kama Congo. Na nchi ikiwa kubwa ni more advantageous kuliko ingekuwa ndogo kwa hiyo serikali itutoe hapa bila visingizio.
 
Billie

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Messages
8,046
Points
2,000
Billie

Billie

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2011
8,046 2,000
Ilo kweli hapo tunalea Umasikini jambo lingine linalonisikitisha ni lile la mji maarufu wa kibiashara hapa Tz i mean Dar es Salam ku oparates nusu siku yaan day time tu.Hapo hapo tunatunza sera za kukuza uchumi wa nchi.Nenda hapo Nairob uone watu wanavyochakalika 24/7.SISI NI MASKINI WA KUTUMIA AKILI ZETU IFIKE POINT TUBADILIKE.
 
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Messages
7,464
Points
1,250
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined May 21, 2012
7,464 1,250
Na ni bora dsm unaweza tembea hata mpaka saa sita usiku .lakini miji mingine yote iliyobakia saa mbili usiku hamna daladala ni kero sana utatumia hela nyingi kwa usafiri,dodoma jiji kubwa ila saa mbili hupati hata ice barabara ni sasa hii sikulea umaskini ple kkoo wakijitahidi mpaka saa sab unaweza pata gari ila ni worse kabisa hata dsm,hatuu\wezi endelea kwa mpango huu kabisa
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,698
Points
2,000
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,698 2,000
Ilo kweli hapo tunalea Umasikini jambo lingine linalonisikitisha ni lile la mji maarufu wa kibiashara hapa Tz i mean Dar es Salam ku oparates nusu siku yaan day time tu.Hapo hapo tunatunza sera za kukuza uchumi wa nchi.Nenda hapo Nairob uone watu wanavyochakalika 24/7.SISI NI MASKINI WA KUTUMIA AKILI ZETU IFIKE POINT TUBADILIKE.
Kwa nini hawa viongozi wetu wanakuwa wazuri kwa visingizio, mimi mbona kama siamini mkuu. Eti majambazi watateka mabasi, hivi majambazi wapo Tanzania tu?
 
Tango73

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Messages
1,678
Points
1,195
Tango73

Tango73

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2008
1,678 1,195
Hivi wewe mpaka leo huji kuwa Tanzania kuwa watu wajuao kujenga chama tuu na wala hawajui kujenga uchumi? Tanzania ilifikia mahali ilkuwa na chama chenye nguvu mara mbili ya nyumba za Ibada. kumbuka usemi huu, usipuuze amri za chama!!!

Hivyo huyo Polisi anyebonga hovyo namna hiyo, hilo sio kosa lake kabisaa, ila ni kosa la malezi ya Chama chake.

JUzi juzi humu jamvini nilioneshwa thread isemayo, Kenya suburbs. Yaani nilisikia uchungu mpaka kifua kilijaaa rami. Kenya kufikia maendeleo makuu namna hii, na kutupita vibaya namna hiyo, hii inaonesha kuwa hatukuwa na watwala bali watu waliotaka kufanywa na jaamii kuwa wao ni mungu watu. naomba ile thread iwe inatolewa kila mara kila mara ili watu wajionee wenyewe jinsi nchi hii ilivyotumia pesa za msaada wa kutoka sweeden kujenga chama badala ya miji.
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,698
Points
2,000
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,698 2,000
Shida ni pale tunapolalama kuwa watu fulani wanatudharau. Si kwamba sisi wenyewe tunajiaibisha? Tumekuwa primitive kiasi cha nature kututawala?

Hivi ni nini mfugaji mwenye busara anafanya: Anaacha kufuga kwa kuwa mbung'o wanang'ata ng'ombe au anatokomeza mbung'o? Yaani kweli tunalala ndani tunaogopa majambazi. Ina maana hawa majambazi wakipata uthubutu wa kupora mchana tutakuwa hatusafiri kabisa.

Isingekuwa kwa sheria hizi, biashara ingekuwa rahisi sana mkuu. Mimi nashangaa sana watu hawa. Mchana lami imechemka mipira ya matairi inalika kweli kweli, ndio maana utaona hata wenye malori wanatembea usiku kupunguza risks za pancha, lakini loh, tumepatikana kweli kweli.
 
Mshuza2

Mshuza2

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Messages
5,893
Points
2,000
Mshuza2

Mshuza2

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2010
5,893 2,000
Kiukweli inauma,maamuzi mengi yanatolewa bila kuzingatia weledi,kila kitu ni siasa! Naamini tunaweza kubadilisha mfumo uliopo kama tutaamua,wenzetu mbona wameweza? Ni kweli ukiingia Nairobi usiku utashangaa jinsi watu walivyo busy,na ndio muda wa mabasi kujidai! Huku kwetu tunajifanya wajuaji tunazidi kuwa legged behind!
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,698
Points
2,000
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,698 2,000
Kiukweli inauma,maamuzi mengi yanatolewa bila kuzingatia weledi,kila kitu ni siasa! Naamini tunaweza kubadilisha mfumo uliopo kama tutaamua,wenzetu mbona wameweza? Ni kweli ukiingia Nairobi usiku utashangaa jinsi watu walivyo busy,na ndio muda wa mabasi kujidai! Huku kwetu tunajifanya wajuaji tunazidi kuwa legged behind!
Tunachoweza kuiga Kenya ni kuzima simu za kichina, masuala yanayohusu uchumi na biashara= nchi yetu kubwa
 
Bilionea Asigwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
16,349
Points
2,000
Bilionea Asigwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
16,349 2,000
Hii nchi sijajua tatizo ni wananchi kutokutambua na kudai mambo ya msingi au ni serikali kujisahau..Suala la kutokusafiri kwa mabasi usiku kwa kisingizio cha usalama halina mashiko hasa kwa maendeleo ya nchi yanayofukuana na wakati... Tanzania haina matishio ya ugaidi kama wenzetu wakenya wala haina matishio ya waasi kama wenzetu waganda, Congo , Rwanda na Burundi lakini ndio waoga namba moja wa usalama...Sijajua hali ingekuaje kama kungekua na waasi na matishio ya ugaidi humu , nchini yawezekana mwisho wa kutembea magari ikawa saa 10 jioni. Sheria kama hizi mara nyingi hutungwa kama sheria za dharura ili kulinda hali fulani kwa nyakati fulani za kiusalama lakini cha ajabu usalama unaporudi sheria hizi haziondolewi hapa ndipo ninaposihangaa sana hii nchi
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,698
Points
2,000
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,698 2,000
Hii nchi sijajua tatizo ni wananchi kutokutambua na kudai mambo ya msingi au ni serikali kujisahau..Suala la kutokusafiri kwa mabasi usiku kwa kisingizio cha usalama halina mashiko hasa kwa maendeleo ya nchi yanayofukuana na wakati... Tanzania haina matishio ya ugaidi kama wenzetu wakenya wala haina matishio ya waasi kama wenzetu waganda, Congo , Rwanda na Burundi lakini ndio waoga namba moja wa usalama...Sijajua hali ingekuaje kama kungekua na waasi na matishio ya ugaidi humu , nchini yawezekana mwisho wa kutembea magari ikawa saa 10 jioni. Sheria kama hizi mara nyingi hutungwa kama sheria za dharura ili kulinda hali fulani kwa nyakati fulani za kiusalama lakini cha ajabu usalama unaporudi sheria hizi haziondolewi hapa ndipo ninaposihangaa sana hii nchi
Mkuu umepiga mahali pake. Kweli huyu aliyesema tuna changamoto kwa kuwa nchi yetu ni kubwa anastahili kujitazama. Sababu hizi hazina msingi. Hivi ni kweli hatuna jeshi linaloweza kufanya vile wanavyofanya Wakenya? Hopeless case!
 
Bilionea Asigwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
16,349
Points
2,000
Bilionea Asigwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
16,349 2,000
Mkuu umepiga mahali pake. Kweli huyu aliyesema tuna changamoto kwa kuwa nchi yetu ni kubwa anastahili kujitazama. Sababu hizi hazina msingi. Hivi ni kweli hatuna jeshi linaloweza kufanya vile wanavyofanya Wakenya? Hopeless case!
jeshi lipo na linaweza kufanya hayo yoote...tatizo tunaishi kiswahiba sana nchi hii...hakuna wakuhoji vitu kama hivi....
 
F

filonos

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2011
Messages
651
Points
225
F

filonos

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2011
651 225
Tunachoweza kuiga Kenya ni kuzima simu za kichina, masuala yanayohusu uchumi na biashara= nchi yetu kubwa
mimi naona hii mada ni Mzuri likini wachangia mada ndio wamesahau tuliko toka wanakumbuka tulipo2 cha muhim ni katoa Ushauli sio kulaumu tujipange upya tuangalie Changamoto zilizopo na kuondoa Mapungufu ili tutoke hapa tulipo twende tuendako kwa mbadiliko na Hali halisi ilivyo naimani watayasikia na kuyafanyia kazi yote kwa jumla......
 
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,097
Points
1,500
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,097 1,500
ninachoshngaa kenya usalama si mzuri lakin bus zinatembea usiku,wamefanikiwa kwa kuweka ulinzi ukipanda bus mkienda hatua fulani mnakuta polis,ninachoona kwa tanzania ni polisi wavivu kufanya kazi usiku wanataka walale tu,wanakwepa majukumu na visingizio lukuki
 
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
13,698
Points
2,000
Mwana Mtoka Pabaya

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
13,698 2,000
ninachoshngaa kenya usalama si mzuri lakin bus zinatembea usiku,wamefanikiwa kwa kuweka ulinzi ukipanda bus mkienda hatua fulani mnakuta polis,ninachoona kwa tanzania ni polisi wavivu kufanya kazi usiku wanataka walale tu,wanakwepa majukumu na visingizio lukuki
Hivi umewahi kujiuliza katika hali tu ya kawaida vijana wa JWTZ huwa wana kazi gani makambini zaidi ya kufyeka nyasi nje ya kambi na kufanya gwaride asubuhi na mchana wote wanashinda chini ya miti. Ndio maana wanakuwa na akili mbovu some times kiasi wanapiga watu hovyo. Hawashirikishwi kwenye mambo productive, wanadumaa ubongo
 
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2008
Messages
4,071
Points
1,250
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2008
4,071 1,250
hii nchi sijajua tatizo ni wananchi kutokutambua na kudai mambo ya msingi au ni serikali kujisahau..suala la kutokusafiri kwa mabasi usiku kwa kisingizio cha usalama halina mashiko hasa kwa maendeleo ya nchi yanayofukuana na wakati... Tanzania haina matishio ya ugaidi kama wenzetu wakenya wala haina matishio ya waasi kama wenzetu waganda, congo , rwanda na burundi lakini ndio waoga namba moja wa usalama...sijajua hali ingekuaje kama kungekua na waasi na matishio ya ugaidi humu , nchini yawezekana mwisho wa kutembea magari ikawa saa 10 jioni. Sheria kama hizi mara nyingi hutungwa kama sheria za dharura ili kulinda hali fulani kwa nyakati fulani za kiusalama lakini cha ajabu usalama unaporudi sheria hizi haziondolewi hapa ndipo ninaposihangaa sana hii nchi
yote kwa pamoja ni matatizo yetu ya kudumu
 
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2008
Messages
4,071
Points
1,250
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2008
4,071 1,250
ni kweli ipo haja ya kubadili mifumo yetu ya uchumi ili tuendelee kuna mambo mengi sana ukijiuliza unakosa majibu ya msingi. kuna maeneo mfano mbeya wananchi wanakatazwa kuuza sukari ya tz malawi lakini ya malawi inaingia kwa fujo na imejaa madukani sasa sisajua maana ya sisi kukatazwa kuuza huko na ya huko kuingia hata kama ni kinyemela.
imefika wakati na sisi tuamke tujue mbinu za kupambana katika uchumi huu wa kibepari. ubepari unataka ushapu wa akili na nguvu. sisi vyote hatuna. kwa namna hii serikali yetu innazidi kuturudisha nyuma katika michakato ya kujikwamua kiuchumi.
 
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2008
Messages
4,071
Points
1,250
Iron Lady

Iron Lady

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2008
4,071 1,250
jeshi lipo na linaweza kufanya hayo yoote...tatizo tunaishi kiswahiba sana nchi hii...hakuna wakuhoji vitu kama hivi....
mkuu sio kuishi kiswahiba hata hao viongozi hawajisumbui kuwaza hayo kwa sababu kilichowaweka hapo sio maslai ya taifa ni maslai ya kwao wao. kujipa tenda wenyewe za serikali, kuna ma 10% ya mikataba na kuuza nchi. hicho ndicho wanachoweza na wanachohangaika kukifanya kila kukicha.
ila pia na sisi wananchi tumezidi kuwa kimya ya msingi hatuyasimamii kidete na kukakikisha yanafanyika tukipewa ahadi tunaridhika tukitishwa tunaogopa. kizazi cha kuhoji ni cha sasa lakini kimejaa woga. tukiacha haya tunaweza kusogea kutoka hapa tulipo.
 
B

blueray

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Messages
2,219
Points
0
B

blueray

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2012
2,219 0
Mkuu umetoa hoja nzuri na hii ni changamoto kwa serikali.

Tatizo serikali yetu inapenda shortcut. Hawafanyi analysis za kitaalamu. Hata leo ukiwauliza baada ya kukataza mabasi kusafiri usiku imesaidia kwa kiasi gani kupunguza ajali au kupunguza ujambazi wa magari hakuna atakayekujibu!

Kingine ni aibu kwa serikali kusalimu amri na kurudisha nyuma maendeleo yake kwa sababu ambazo inaweza kuzidhibiti!

Imefika wakati sasa serikali iamke na ibebe majukumu yake badala ya kulala. Huku kukosa kazi za kufanya askari wetu ndio maana sasa wanatumwa kudhibiti demokrasia na kuua wananchi wasio na hatia
 
B

Bahati Risiki

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Messages
530
Points
0
B

Bahati Risiki

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2012
530 0
Yaani tunaitafuta serikali kwa uchumi. Imeshindwa hata kulinda maadili tu hiyo akili ya uchumi itaipataje? Mmewahi mwona Kibaki akikokotwa na matoroli ya wazungu, futilia mbali kubembea? Tanzania haina kiongozi wala serikali. Kilichobaki ni usanii tu ndiyo maana hatuendi popote. Ebu oneni ya Mwangosi, Ulimboka, ally wa Morogoro, na wengine wengi tu. Serikali imefanya nini? Nchi yetu inaondoka taratibu sii kiuchumi tu, bali ktk utu na maadili. Ole wa Kikwete na maswahiba wake. Hiyo siku watakayoona mwanga wa Nyerere wataanguka chini. Tumelia ya kutosha sasa tufanye mabadiliko na kuondokana na udhalimu wa ccm. Tusipofanya hivyo kesho tutapewa sahani za ubwabwa, vitambaa vya kijani, na kanga. Sheria wakati huo itakuwa mabasi yapite hadi saa saba mchana mwisho hatuwezi kupambana na jua maana miti imeisha.
 

Forum statistics

Threads 1,285,560
Members 494,675
Posts 30,866,790
Top