frakerg
Member
- Jan 15, 2014
- 15
- 4
Salaam,
Mimi ni Mkenya mzawa wa Nairobi na ningependa sana kuzuru Dar kwa nia ya kujivinjari. Hii itakuwa mara yangu ya kwanza kuzuru Tanzania, na simjui Mtanzania yeyote. Ningependelea sana kuzuru sehemu zilizokaribu na bahari.
Haja yangu sana ni kuyaelewa maisha ya watanzania, na kuishi nao hata kama ni kwa muda mfupi. Sina haja na kuzuru mbuga za wanyama lakini nitafurahia kuzuru maeneo ya kistoria ambayo kwa sasa siyajui.
Pia sijui nitasafiri vipi kwa basi au kwa ndege. Hili swali itabidi nimewauliza Wakenya wenzangu hapa ambao wamewahi safiri Dar. Kwa sasa simjui mtu yeyote ambaye amewahi safiri Tanzania itabidi nitafute.
Sina hela nyingi za kutumia kwa ziara yangu na sithani nitahitaji hela nyingi kwa sababu natumai kuyaishi maisha ya kwaida kama mtanzania yeyote yule kwa muda nitakaokuwa huko kuabiri daladala, kula kwa hoteli za kawaida, kwenda vilabu vya kawaida na kathalika.
Sijui kama kunaye katika hili jukwaa anaweza nipa mawaidha yatakayonisaidia kupanga ziara yangu. Mtaniwia radhi Kiswali changu si kizuri nimefunzwa kiswahili darasani sikiongei kila siku.
Asante