Kuzuia msafara wa Rais ni uhaini!

Kuzuia msafara wa Rais ni uhaini!

Yaani nchi hii ni ya maajabu sana, miaka hii jitu linaamini kuwa wanachi ndio huwa wanasimamisha msafara wa rais, ni ujuha wa hali ya juu!
 
tuna tatizo jingine la waandishi wa habari vilaza zaidi, unaweza kukuta anatangaza wananchi wa eneo fulani wanamuunga raisi mkono lkn ukisikliza wanachoongea wananchi ni malalamiko mwanzo mwisho
 
watu wametelekeza taaluma, imebaki kama wa wimbo saida kaloli, chambua kama kalanga.
 
Nijuacho watu wanapozuiwa wasikatize na askari wa barabarani ili kupisha msafara hujikuta wapi katika mkusanyiko mfano magari husimama kabisa kwenye center za miji na hapo rais akifika husimama yeye mwenyewe azungumze na wananchi hakuna RAIA anaweza kusimamisha msafara wa rais hapa Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni Rais wa JMT!Hebu jaribu mfanye kumsimamisha kimya kimya kama hamjalambwa shaba!
Kiki tu hizo!
Hata kukamata vichwa vya treni ambavyo mmiliki wake hajulikani ni kiki
Walimchagua, wanampenda.
 
Hizi habari za kusema wananchi wamezuia msafara wa Rais kumuelezea shida zao nadhani ifike mahala sasa tuseme ukweli!!!
Hakuna anayezuia msafara wa Rais,kama ushaona speed ya gari za kwenye msafara,utakubaliana na mimi kuwa hakuna mwananchi wa kawaida anayeweza kufanikiwa kuzuia msafara!

Turudi nyuma kabla ya kuzuia,unawaandaa watu kwenda kumpokea Rais halafu unasema wamezuia msafara!Mnafunga masoko na na kuwalazimisha walimu na watumishi wa serikali kwenda kujipanga barabarani halafu mnasema wamezuia msafara!!!!!

Hebu wananchi wajipange kimya kimya halafu wajue kuna msafara wa Rais,waende kuuzuia waone kitakachowakuta!

Hizi kiki ifike mahali media nazo ziache kutoa promo zisizo na kichwa wala miguu!

Kuna taarifa kuwa huko Tanga kesho soko litafungwa ili watu waende kwenye mkutano!Watumishi wataandikishwa hadi majina na ole wao wasioukuwepo!!!!
lowasa na wapinzani wakifunguliwa magufuli atakufa kwa presha
 
Hahaha bavicha bana mwanzo walisema haiwezekani ... Sasa wanadai uhaini ...
 
Nguvu zinazotumika kufanya ngonjera zingetumika kwenye mambo ya msingi, Sisonje angeaminika bila kikwazo lakini kwa mwendo huu anajidanganya tu.
 
Sasa wewe kinakuuma nini jamani wasimamishe wasisimamishe msafara wewe kinakuuma nini u unapungukiwa nini?
 
Back
Top Bottom