Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

KWANZA MPAKA SASA SIAMINI ETI TANZANIA TUNASHINDWA KUFANYA PROCESS HIYO HAPA...MBONA KUNA WATU TUNAWAJUA NA WALIKUWA WANACHUKUA MATOLEO YA KWENDA KUFANYA KAZI YA KUTENGANISHA DHAHABU,SHABA,FEDHA KUTOKA KWENYE MCHANGA,NA WAMEKUWA WAKIFANYA HAPAHAPA HYO KAZI

OVA
Wanabodi
Hatua ya rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa kinachoitwa mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa, kitendo cha kishujaa cha hali ya juu sana kinachostahili pongezi za dhati kwa sababu kiukweli Tanzania lilikuwa ni shamba la bibi, tumekuwa tunaibiwa sana mchana kweupe kwa sababu hiki kinachoitwa mchanga wa dhahabu, kiukweli sio mchanga wa dhahabu bali ni makinikia ya dhahabu, ni gold concentrate yenye shaba na fedha, uwezo wa kutenganisha dhahabu, shaba na fedha, sio Tanzania hatuna, bara zima la África hatuna wala ulaya hawana. Wenye smelter ya uwezo huo ni Japan na China na Urusi ambao wanatumia umeme wa nuclear reactor.

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo, bahati mbaya alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata peanut na wenye migodi wakikomba faida yote.

Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania hatuna uwezo huo rais Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo kama nchi za Ghana na África Kusini zilizoko kwenye 10 bora hazijawa na uwezo huo, what are the chances ya Tanzania kujenga uwezo huo?. Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule! .

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nía ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji uwezo. Wachumi wa sekta ya madini tusaidieni, kwa umeme huu, na gold kiduchu hii kwa hizo smelter za uwezo huo jee Tanzania tunaweza? . Kama mikataba ya migodi hiyo huo ndio uliokuwa utaratibu wao, maamuzi kama haya yanamaana gani kwenye investment climate yetu? .

Kwa vile rais wetu ameonyesha nia kulinda rasilimali zetu, Tanzania tusiendelee kufanywa shamba la bibi, nashauri tusiishie kwenye mchanga tuu wa dhahabu, kwanini tusiende na kwenye gesi maana nako tunaibiwa!.
http://www.jamiiforums.com/threads/...anzania-tunaibiwa-mchana-kweupe.298561/page-3
Hakuna hata kitalu kimoja cha gesi kinachomilikiwa na Watanzania, kwa sababu hatuna uwezo wa kumiliki hata kitalu kimoja tuu!, sasa kama tumeshindwa hata kuchangishana mifuko yote ya hifadhi za jamii na mabenki yote kumiliki angalau kitalu kimoja tuu, what are the chances ya kumiliki gold smelter la nuclear power reactor?!.

Niliwahi kushauri
https://www.jamiiforums.com/threads...ye-uchumi-we-have-to-choose-or.1189637/page-3

Ili hizi zisije kuwa ni siasa tuu, Tanzania tunahitaji uniform standard formula na rules za kulinda rasilimali zetu zote kwa manufaa ya Watanzania na sio double standards kwa kuzuia tuu mchanga wa dhahabu huku gesi tunaibiwa, Tanzanite tunaibiwa, kwenye vitalu vya uwindaji, light aircrafts zinatua na kupaa huku no body cares zinabeba nini huku tembo wetu wakizidi kuyeyuka!.
To hell with mikataba ya kinyonyaji, to hell with wawekezaji majambazi wanaotuibia kwa kisingizio cha umasikini wetu, to hell with FDI dependence kwenye uwekezaji, tujenge uwezo kwa Watanzania kuijenga nchi yetu, kwa kutumia mitaji na rasilimali zetu za ndani kumiliki uchumi wetu, swali linabaki ni moja tuu "kwa kutumia nini from where and how? .

Paskali
 
Unazungumzia mikutano ya hadhara ya kisiasa, sisi Watanzania tusio na vyama kwetu hata ruzuku ya vyama ni ufisadi, hivyo tumeshauri ifutwe
https://www.jamiiforums.com/threads...ie-mbali-ruzuku-hii-ni-ufisadi.1129220/page-3

Paskali
Paskal,

Naona umejirudi.
Tutumie akili na uelewa wetu kwa manufaa ya taifa. Sio hii miluzi ya kupuuz isiyo na tija.

Ni kweli ngoja wafungue tuone, yawezekana ni semi processed gold, wengine wanaita kibongobongo 'Carbon'

Ujue inauma kaka.
Ni bora kufunga tuwaachie wachimbaji wadogo wazawa wajiachie huu ni upuuz.
 
Lengo ni zuri tatizo ni ukurupukaji. Hili zoezi lilihitaji majadiliano baina ya pande 2. Ikumbukwe hii si mara ya kwanza kwa zuio hili chini ya JPM. Mara ya kwanza lilifeli.

Kuchenjua madini kunahitaji uwekezaji mkubwa wa mitambo. Hivyo wawekezaji walipaswa kupewa muda mf miezi6 au mwaka kwa makubaliano ya pande zote 2. Huku kukurupuka ni sawa na zoezi la Viroba. Hakuna muda wa mpito kwa Mwekezaji.

Naskia migodi imesitisha mikataba na kampuni zote, wafanya kazi wote wamesimamishwa kazi, mafunzo yote yamesitishwa, nk. Kodi tunapoteza, ajira kwa watu wetu zinapotea, biashara za jirani zina athirika, nk.

Wanalipaga Kodi hao??????
Acha tuwachenjie tu Mara kibao wanadai wamepata hasara na kuondoka hawaondoki

In short ni kwamba gharama ya kusafirisha Mchanga inaathiri faida, faida ikiathiriwa hata kama ni kwa makusudi wanajustify tusipewe chochote lakini pia inatoa mwanya wa kupigwa.

Nani anayeshehudia kinachoendekea Japan
 
unafiki huo , unazuia mchanga wakati huo huo
1. unajenga airport chato nje ya bajeti.
2. Unamlipa lipumba mshahara wakati hakuna kazi anayofanya
3. unamlipa bashite mshahara wakati anatumia vyeti vya kuazima
4. unametea bashite na kumlipa mshahara wakati ni jambazi wa kuvamia vituo vya TV na kuwatishia watu.

Hizi ndio akili za mgabe, kuwakomoa wazungu wakati mwenyewe unafanya madudu .
 
Wanabodi
Kwenye mazuri tupongeze, mabaya tukosoe na panapostahili ushauri au angalizo tutoe.

Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule!. Hili la mchanga nawaomba wenye kumbukumbu wekeni kumbukumbu sahihi ya bandiko hili kuwa tutabana wee lakini mwisho wa siku tutaachia tena tukiwa tumeumizwa katokana na kubana. Ili tusiumizwe, Tanzania lazima haya makontena 277 tuliyoyakamata, lazima tuyasimamie wenyewe, yachenjuliwe ili tujue kilichomo, hivyo kuweza ku calculate kiasi walichokuwa wanatuibia. Majadiliano yoyote bila udhibitisho wa kilichomo, tutapigwa tena, na mchanga utaendelea kuchenjuliwa kule kule unakochenjuliwa!. ili tusijue kilichomo kwenye mchanga huu, wanyonyaji hawa, watakuwa tayari kufanya lolote, hata ikibidi kutulambisha asali, watatulambisha, lakini mchanga uondoke!.

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nia ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji sio tuu nia ya dhati, bali pia uwezo. the capacity na ruhusa ya wakubwa wa dunia hii, ndipo uvifanye.

Wachumi wa sekta ya madini humu jf, hebu tusaidieni kwenye hili, jee kwa umeme huu, wa gridi ya taifa na gold kiduchu hii kwa hizo smelter za uwezo huo jee Tanzania tunaweza?, unless tununue vile vi smelter vidogo tuuchenjue wenyewe mchanga wetu kidogo kidogo na vi smelter vidogo, huwezi kuchenjua kila kitu. Ukichenjua mchanga kidogo, the economics of scales inaingilia kati kwa the cost of extraction kuwa ni kubwa kuliko the byproducts za kitakachopatikana!. Piga ua galagaza, tumezua mchanga kwa mbwembwe nyingi, lakini tukilambishwa tuu asali, mtashuhudia tutaendelea kusafirisha mchanga na tutaendelea kuibiwa unless tuvunje mikataba!.
Paskali
Hizi dola milioni 300 tunazopewa sio tunalambishwa asali, kisha turuhusu mchanga uendelee kusafirishwa, ama tunajenga smelter, tuuchenjue, tujue kilichomo, ndipo tupigiane mahesabu na mwizi wetu!.

Ila pia wajemeni, moja shika sii kumi nenda rudi, tupokee tuu hiki kidogo kilichotolewa, wakati tukiendelea kukifuatlia kikubwa. Rais Magufuli na Prof. Kabudi, tuwapongeze kwa hili japo ni kidogo, lakini ni something, na something is better than nothing!, tuwe na shukrani katika madogo, ili tujaaliwe makubwa!.

Paskali
 
Wanabodi
Nimekiita ni kitendo cha kizalendo na kishujaa kwa sababu kinagusa maslahi ya wakubwa, hivyo tutatikiswa na kupewa misukusuko na wakubwa hawa!. Inahitaji uzalendo wa kweli kuingilia kati utekelezaji wa mikataba ya kinyonyaji iliongiwa na watangulizi wake au kwa ujinga wa kutojua tunaibiwa, au kwa maslahi ya matumbo yao!.

Irani ilipotaka kutengeneza reactor iliipata, Sadam Husein wa Iraq nae aliipata na kwa nchi za Afrika, Muamar Gaddafi alishungulikiwa, hivyo wakubwa hawa wakisikia Tanzania tuna mpango wa kununua smelter ili angalau mchanga wa Afrika uchenjuliwe Africa, wakubwa hawa hawatakubali, hivyo kwa uamuzi huu, Magufuli anahitaji sala zaidi ya pongezi tuu ili aweze kuyaweza yote katika YEYE amtiaye nguvu.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, .

Paskali
Nafanya tuu rejea, usikute zile demokrasia na haki za binaadamu katika nyaraka zile ni bangusilo tuu, the real issue ya kumtikisa Magufuli ni hii ya vita vya kiuchumi.

Lets wait and see.

P,
 
It is simple,atekeleze yale maazimio 14 aache la ushoga mambo yatakwenda sawa.Shida ni kuwaachia wapinzani hapo anaona kama crime
 
Wanabodi
Kwenye mazuri tupongeze, mabaya tukosoe na panapostahili ushauri au angalizo tutoe..

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe tuu mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kabisa kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo wa ndani wa kuyachimba, bahati mbaya Nyerere alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata just a peanut huku wenye migodi wakikomba kila kitu na kuishia na faida yote huku wakituachia mashimo! .

Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania kwa hivi tulivyo sasa, bado hatuna uwezo huo rais wetu Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo nchi kama za Ghana na África Kusini ambazo ziko kwenye top 10 bora za uzalishaji wa dhahabu, bado hazijawa na uwezo wa kuwa na smelter hizo, what are the chances kwa Tanzania kujenga smelter kwa sio kwa uwezo gani bali kwa mchanga gani wa kuutengenezea smelter?!.

Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule!. Hili la mchanga nawaomba wenye kumbukumbu wekeni kumbukumbu sahihi ya bandiko hili kuwa tutabana wee lakini mwisho wa siku tutaachia tena tukiwa tumeumizwa katokana na kubana. Ili tusiumizwe, Tanzania lazima haya makontena 277 tuliyoyakamata, lazima tuyasimamie wenyewe, yachenjuliwe ili tujue kilichomo, hivyo kuweza ku calculate kiasi walichokuwa wanatuibia. Majadiliano yoyote bila udhibitisho wa kilichomo, tutapigwa tena, na mchanga utaendelea kuchenjuliwa kule kule unakochenjuliwa!. ili tusijue kilichomo kwenye mchanga huu, wanyonyaji hawa, watakuwa tayari kufanya lolote, hata ikibidi kutulambisha asali, watatulambisha, lakini mchanga uondoke!.

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nia ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji sio tuu nia ya dhati, bali pia uwezo. the capacity na ruhusa ya wakubwa wa dunia hii, ndipo uvifanye.
Paskali
Wanabodi
Katika bandiko hili, kuna kitu nilikisema kuhusu huu mchanga wa dhahabu.

Mazungumzo yamemalizika rasmi na makubaliano yamefikiwa, hivyo subirini tutangaziwe rasmi kisha tukumbushane vizuri kuhusu viapo vya watu kujiapiza kwa nguvu kweli kweli, halafu, wakiishwa labishwa tuu asali...
Mchanga huo unaondoka.

Huu mchanga ukiondoka bila sisi kujua kilichomo, kiukweli kabisa sitashangaa kwa sababu naelewa the games people plays.

Tusubiri, tukumbushane.
P
 
Hizi dola milioni 300 tunazopewa sio tunalambishwa asali, kisha turuhusu mchanga uendelee kusafirishwa, ama tunajenga smelter, tuuchenjue, tujue kilichomo, ndipo tupigiane mahesabu na mwizi wetu!.

Ila pia wajemeni, moja shika sii kumi nenda rudi, tupokee tuu hiki kidogo kilichotolewa, wakati tukiendelea kukifuatlia kikubwa. Rais Magufuli na Prof. Kabudi, tuwapongeze kwa hili japo ni kidogo, lakini ni something, na something is better than nothing!, tuwe na shukrani katika madogo, ili tujaaliwe makubwa!.

Paskali
Ahadi ya fedha hizi dola milioni 300 ilikuwa ni goodwill kuonyeshea nia njema ya kuzungumzia deni letu lote la dola bilioni 191.

Sasa mazungumzo yamemalizika wamefikia makubaliano ya mwisho, fedha hizo sasa ndio kifuta machozi chetu na kusamehe deni letu lote.

Kwa vile mimi sio authority, tusubiri taarifa rasmi.

P.
 
Wanabodi

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe tuu mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kabisa kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo wa ndani wa kuyachimba, bahati mbaya Nyerere alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata just a peanut huku wenye migodi wakikomba kila kitu na kuishia na faida yote huku wakituachia mashimo! .

Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania kwa hivi tulivyo sasa, bado hatuna uwezo huo rais wetu Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo nchi kama za Ghana na África Kusini ambazo ziko kwenye top 10 bora za uzalishaji wa dhahabu, bado hazijawa na uwezo wa kuwa na smelter hizo, what are the chances kwa Tanzania kujenga smelter kwa sio kwa uwezo gani bali kwa mchanga gani wa kuutengenezea smelter?!.

Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule!. Hili la mchanga nawaomba wenye kumbukumbu wekeni kumbukumbu sahihi ya bandiko hili kuwa tutabana wee lakini mwisho wa siku tutaachia tena tukiwa tumeumizwa katokana na kubana. Ili tusiumizwe, Tanzania lazima haya makontena 277 tuliyoyakamata, lazima tuyasimamie wenyewe, yachenjuliwe ili tujue kilichomo, hivyo kuweza ku calculate kiasi walichokuwa wanatuibia. Majadiliano yoyote bila udhibitisho wa kilichomo, tutapigwa tena, na mchanga utaendelea kuchenjuliwa kule kule unakochenjuliwa!. ili tusijue kilichomo kwenye mchanga huu, wanyonyaji hawa, watakuwa tayari kufanya lolote, hata ikibidi kutulambisha asali, watatulambisha, lakini mchanga uondoke!.

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nia ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji sio tuu nia ya dhati, bali pia uwezo. the capacity na ruhusa ya wakubwa wa dunia hii, ndipo uvifanye.

Paskali
Wanabodi nimeiona draft agreement ya mazungumzo ya serikali na Barrick, hakuna lolote kuhusu kuchenjuliwa kwa mchanga!.

Tuliuzuia mchanga kwa sababu tulihisi tunaibiwa kwa kutokujua kilichomo. Tume mbili za rais ile ya Prof. Mruma na Prof. Osoro zikathibitisha ni kweli tunaibiwa. TRA wakapiga hesabu deni likaja dola billions 193.
Kwenye mazungumzo tumekubali kufuta deni hilo kwa kulipwa kufuta machozi cha dola million 300 ambazo zitalipwa ndani ya miaka 7.

Sherti la kwanza ni tukubali kulipwa down payment ya dola million 100 mchanga uondoke na zuio liondoewe.

Kama tuliuzuia mchanga usiondoke kwa sababu hatujui kilichomo ndio maana tunaibiwa, leo tunambiwa mchanga utaondoka bila sisi kujua kilichomo, then tuliuzuia wa nini?!.

Kina kitu nilikisema humu kuhusu mchanga huu na mambo ya kulambisha asali!.

Kama kwenye sakata la Acacia, the bone of contention ni ule mchanga, kwa sababu hatujui kilichomo, mgogoro huu utaishaje bila kujua kilichomo?.
Kiukweli kabisa mchanga ukiondoka sitashangaa tuu bali nitaamini nilicho kisema humu kuhusu mchanga ni kweli.
P
 
Pongezi za nini wewe kikaragosi!?😳

Wanabodi
Kwenye mazuri tupongeze, mabaya tukosoe na panapostahili ushauri au angalizo tutoe.

Hatua ya rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa kinachoitwa mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa, ni kitendo cha kizalendo na kishujaa cha hali ya juu sana kinachostahili pongezi za dhati kwa sababu kiukweli Tanzania lilikuwa ni shamba la bibi, tumekuwa tunaibiwa sana mchana kweupe kwa sababu hiki kinachoitwa mchanga wa dhahabu, kiukweli sio mchanga wa dhahabu bali ni makinikia ya dhahabu, ni gold concentrate yenye shaba na fedha, na madini mengine mengi kwa kiwango kidogo ila yana thamani kubwa.

Nimekiita ni kitendo cha kizalendo na kishujaa kwa sababu kinagusa maslahi ya wakubwa, hivyo tutatikiswa na kupewa misukusuko na wakubwa hawa!. Inahitaji uzalendo wa kweli kuingilia kati utekelezaji wa mikataba ya kinyonyaji iliongiwa na watangulizi wake au kwa ujinga wa kutojua tunaibiwa, au kwa maslahi ya matumbo yao!.

Kisingizio cha kuibiwa huku ni hoja kuwa Tanzania hatuna uwezo wa kutenganisha dhahabu, shaba, fedha, na madini mengine toka katika mchanga huo!.

Tena sio tuu ni Tanzania pekee ndio tumeelezwa kuwa hatuna, uwezo huo, bali wakoloni mamboleo hawa na mabeberu, wametengeza mfumk kuhakikisha mitambo hiyo haipo bara zima la África lenye dhahabu, kisha kwenda kusimika mitambo hiyo nchini Japan ambako hawana hata tone la dhahabu!.

Wenye smelter za uwezo huo ni wale wale mataifa makubwa kiuchumi, the big 5!. Marekani, Japan, China Urusi na Ujerumani ambao wanatumia umeme wa nuclear reactor. Mfano kuna kanchi kadogo sana kanaitwa Uswiss hakana hata tone la dhahabu lakini kanazo smelter 5!.

Irani ilipotaka kutengeneza reactor iliipata, Sadam Husein wa Iraq nae aliipata na kwa nchi za Afrika, Muamar Gaddafi alishungulikiwa, hivyo wakubwa hawa wakisikia Tanzania tuna mpango wa kununua smelter ili angalau mchanga wa Afrika uchenjuliwe Africa, wakubwa hawa hawatakubali, hivyo kwa uamuzi huu, Magufuli anahitaji sala zaidi ya pongezi tuu ili aweze kuyaweza yote katika YEYE amtiaye nguvu.

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe tuu mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kabisa kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo wa ndani wa kuyachimba, bahati mbaya Nyerere alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata just a peanut huku wenye migodi wakikomba kila kitu na kuishia na faida yote huku wakituachia mashimo! .

Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania kwa hivi tulivyo sasa, bado hatuna uwezo huo rais wetu Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo nchi kama za Ghana na África Kusini ambazo ziko kwenye top 10 bora za uzalishaji wa dhahabu, bado hazijawa na uwezo wa kuwa na smelter hizo, what are the chances kwa Tanzania kujenga smelter kwa sio kwa uwezo gani bali kwa mchanga gani wa kuutengenezea smelter?!.

Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule!. Hili la mchanga nawaomba wenye kumbukumbu wekeni kumbukumbu sahihi ya bandiko hili kuwa tutabana wee lakini mwisho wa siku tutaachia tena tukiwa tumeumizwa katokana na kubana. Ili tusiumizwe, Tanzania lazima haya makontena 277 tuliyoyakamata, lazima tuyasimamie wenyewe, yachenjuliwe ili tujue kilichomo, hivyo kuweza ku calculate kiasi walichokuwa wanatuibia. Majadiliano yoyote bila udhibitisho wa kilichomo, tutapigwa tena, na mchanga utaendelea kuchenjuliwa kule kule unakochenjuliwa!. ili tusijue kilichomo kwenye mchanga huu, wanyonyaji hawa, watakuwa tayari kufanya lolote, hata ikibidi kutulambisha asali, watatulambisha, lakini mchanga uondoke!.

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nia ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji sio tuu nia ya dhati, bali pia uwezo. the capacity na ruhusa ya wakubwa wa dunia hii, ndipo uvifanye.

Wachumi wa sekta ya madini humu jf, hebu tusaidieni kwenye hili, jee kwa umeme huu, wa gridi ya taifa na gold kiduchu hii kwa hizo smelter za uwezo huo jee Tanzania tunaweza?, unless tununue vile vi smelter vidogo tuuchenjue wenyewe mchanga wetu kidogo kidogo na vi smelter vidogo, huwezi kuchenjua kila kitu. Ukichenjua mchanga kidogo, the economics of scales inaingilia kati kwa the cost of extraction kuwa ni kubwa kuliko the byproducts za kitakachopatikana!. Piga ua galagaza, tumezua mchanga kwa mbwembwe nyingi, lakini tukilambishwa tuu asali, mtashuhudia tutaendelea kusafirisha mchanga na tutaendelea kuibiwa unless tuvunje mikataba!.

Kama mikataba ya migodi hiyo huo ndio uliokuwa utaratibu wao, maamuzi kama haya yanamaana gani kwenye investment climate yetu? .

Kwa vile rais wetu ameonyesha nia kulinda rasilimali zetu, Tanzania tusiendelee kufanywa shamba la bibi, nashauri tusiishie kwenye mchanga tuu wa dhahabu, tende kabisa kwenye mikataba yenyewe ya madini, ni mikataba ya kinyonyaji, na tusiishie kwenye madini tuu, kwanini tusiende hadi kwenye gesi asili maana huko nako nako tunaibiwa kweli kweli kwa vile hatuna hili wala lile!.
Gesi asili: Is it "day light robbery?!" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Hakuna hata kitalu kimoja cha gesi kinachomilikiwa na Watanzania, kwa kisingizio hatuna uwezo wa kumiliki hata kitalu kimoja tuu cha gesi!, what are the chances ya kumiliki smelter.

Sasa kama tumeshindwa hata kuchangishana mifuko yetu yote ya hifadhi za jamii na mabenki yote kumiliki angalau kitalu kimoja tuu cha gesi, what are the chances ya kumiliki gold smelter la kiwango cha nuclear power reactor?!.

Niliwahi kushauri
Japo Beggars Can Not Be Choosers, Tuache Siasa Kwenye Uchumi. We Have to Choose Or. ..

Ili hizi zisije kuwa ni siasa tuu, Tanzania tunahitaji uniform standard formula na rules za kulinda rasilimali zetu zote kwa manufaa ya Watanzania na sio double standards kwa kuzuia tuu mchanga wa dhahabu tuu, huku tunaendelea kuibiwa kwenye dhahabu zenyewe!. Watanzania tunaibiwa kwenye Tanzanites, tunaibiwa kwenye gesi, tunaibiwa kwenye vitalu vya uwindaji, light aircrafts zinatua na kupaa migodini huku no body cares zinabeba nini huku tembo wetu wakizidi kuyeyuka!.

To hell with mikataba ya kinyonyaji, to hell with wawekezaji majambazi wanaotuibia kwa kisingizio cha umasikini wetu, to hell with FDI dependence kwenye uwekezaji, tujenge uwezo wa ndani kwa Watanzania kukopa na kuijenga nchi yetu, kwa kutumia mitaji na rasilimali zetu za ndani kumiliki uchumi wetu, swali linabaki ni moja tuu "kwa kutumia nini from where and how? .

Paskali
 
Wanabodi nimeiona draft agreement ya mazungumzo ya serikali na Barrick, hakuna lolote kuhusu kuchenjuliwa kwa mchanga!.

Tuliuzuia mchanga kwa sababu tulihisi tunaibiwa kwa kutokujua kilichomo. Tume mbili za rais ile ya Prof. Mruma na Prof. Osoro zikathibitisha ni kweli tunaibiwa. TRA wakapiga hesabu deni likaja dola billions 193.
Kwenye mazungumzo tumekubali kufuta deni hilo kwa kulipwa kufuta machozi cha dola million 300 ambazo zitalipwa ndani ya miaka 7.

Sherti la kwanza ni tukubali kulipwa down payment ya dola million 100 mchanga uondoke na zuio liondoewe.

Kama tuliuzuia mchanga usiondoke kwa sababu hatujui kilichomo ndio maana tunaibiwa, leo tunambiwa mchanga utaondoka bila sisi kujua kilichomo, then tuliuzuia wa nini?!.

Kina kitu nilikisema humu kuhusu mchanga huu na mambo ya kulambisha asali!.

Kama kwenye sakata la Acacia, the bone of contention ni ule mchanga, kwa sababu hatujui kilichomo, mgogoro huu utaishaje bila kujua kilichomo?.
Kiukweli kabisa mchanga ukiondoka sitashangaa tuu bali nitaamini nilicho kisema humu kuhusu mchanga ni kweli.
P
mkuu una maana kuna kitu uliandika ambacho wewe mweneyewe hukiamini lakini unataka sisi tukiamini? tutake radhi sisi tuliokujanjarusha mapemaaa!!!

walambishwe kina Ngeleja pekeyao!!!? aa wapi, "wanaume" wamekata kitu kidogo.

sisi tusiopambania uteuzi haturembirembi kama Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom