Kuziba riziki ya mtu

Sasa anayeziba anafaidika badala ya yule aliyezibwa, ile riziki itarudi ama ndo hivyo imetoka hiyo?
In short.., anayeziba huishia katika Mikosi na kupoteza nguvu zake hatimaye kubaki muflisi kama siyo kuchananyikiwa!! (mifano ona washirika/partnerships, hiana,wanaoghushi)MN !!
 
Mimi imani yangu uwa inanituma kuamini kwamba hakuna mwanadamu au chochote kinachoweza KUZIBA au KUCHELEWESHA riziki ya mtu. Kama Mungu kanipangia riziki yangu kupatikana kwa mfano tarehe 1 Julai 2017, kama kutakuwa na yeyote hapo katikati kabla ya tarehe hiyo anaeweza kuhesabiwa na wengine kuwa ananizibia au kunicheleweshea riziki yangu mimi sitaamini hivyo. Mtu wa hivyo nitamchukulia kama sehemu ya miiba ya kawaida ninayotakiwa kukutana na kupishana nayo njiani nikiwa katika safari yangu kuelekea siku ya riziki yangu ambayo ni tarehe 1 Julai, 2017. Hivyo tarehe yangu ya riziki iliyopangwa na Mungu iko palepale haizibwi wala kucheleweshwa na mtu. Hivyo vikwazo ni sehemu tu ya process ya kunifikisha tarehe yangu ya riziki.
 
Hizi ndio dhana potofu za waafrika, uwezi kuziba riziki ya mtu labda mtu ajizibie mwenyewe riziki zake. Kikubwa kwa mtu kufanikiwa ni reasoning ability kitu ambacho uwezi kumnyan'ganya ata ufanyaje.

Katika life span ya binadamu anaweza kukutana na changamoto kwa sababu maisha ayaji na manual on how to leave with people, kuna watu wanajiamini, wengine awajiamini, kuna wenye tamaa, wivu wa maendeleo you name it to do with the mix.

Inategemea umezungukwa na akina nani wengi kama ni wale negative utakutana na changamoto hizi za kutaka kukuaribia lakini inatakiwa iwe kama experience tu zinazoleta setback za maisha na ujifunze binafsi naita mafunzo kutoka kwa mungu mwenyewe kama sehemu ya kukuonyesha mbeleni na kujua danger zilipo.

Mzungu ndio mtu pekee kagundua njia ya kuweza kuziba risks, kwa uelewa wa kuwa uwezi kuzuia reason ability ya binadamu anachofanya sasa ni kukutoa kwenye kufikiria na kukuchanganya kwa sababu anajua wote awafikirii sawa anaweza kuingiza mdudu wa dini, au kukuwekea matatizo ya drugs kwenye jamii yako chochote kile kinachoweza kukufanya utoke kwenye mstari hapo sasa na ujikite kufikiria kile ambacho akijengi creativity.

Na hapa ndio waafrika wengi walipo tunashindwa kujua chanzo cha kukwama wewe unakaa na watu ambao saa zote ni usumbufu, majungu, maneno na negative zingine; halafu ujifunzi utaishia kulalama kuna mtu anakuzibia risk za maisha, wakati unaona wazi kunaweza kuwa na kundi fulani liko positive na wote wakafanikiwa.
 
Hivi ukijaribu kuziba riziki ya mtu, nini kitatokea baada ya hapo?

Maana wengi wanasema ni vigumu kuziba riziki ya mtu.
Kwenye ulimwengu wa nguvu za giza haya mambo yapo japo huisha muda baada ya muda ndio maana kwenye post zangu nyingi zinazozungumzia ushirikina nimetahadharisha sana kuhusu kutupa hovyo manii kinyesi nywele za aina zote kucha nk nk na hata nguo za ndani pia hivyo vitu ni muhimu sana kwenye kutumika kichawi kukufanyia lolote baya
 
Mimi imani yangu uwa inanituma kuamini kwamba hakuna mwanadamu au chochote kinachoweza KUZIBA au KUCHELEWESHA riziki ya mtu. Kama Mungu kanipangia riziki yangu kupatikana kwa mfano tarehe 1 Julai 2017, kama kutakuwa na yeyote hapo katikati kabla ya tarehe hiyo anaeweza kuhesabiwa na wengine kuwa ananizibia au kunicheleweshea riziki yangu mimi sitaamini hivyo. Mtu wa hivyo nitamchukulia kama sehemu ya miiba ya kawaida ninayotakiwa kukutana na kupishana nayo njiani nikiwa katika safari yangu kuelekea siku ya riziki yangu ambayo ni tarehe 1 Julai, 2017. Hivyo tarehe yangu ya riziki iliyopangwa na Mungu iko palepale haizibwi wala kucheleweshwa na mtu. Hivyo vikwazo ni sehemu tu ya process ya kunifikisha tarehe yangu ya riziki.
Yaah ukiona ulitaka kupata kazi au pesa kisha ikaishia hewani hiyo haikuwa yako na pengine ungeipata kuna mengi yangekutokea rizq yako haichelweshwi wala nini siku ulopangiwa na mungu kuipata ndio hiyo kutakuwa hakuna figisufigisu wala nini.
 
Bure mtameza sumu, mfe huku mnaona
Alopewa muheshimu, riziki yake ni pana
Kuipora kwake ni vigumu, mtahangaika sana....
 
Sasa hapo hasara si imepatikana, maana kama ulitakiwa ujenge nyumba mfano ukiwa na miaka 25 ukaja kujenga ukiwa na miaka 45 au 55, si hasara hiyo?
Ww sio mzima una matatizo sio bure.... Kwahiyo kujenga at 45 and above ni hasara?
 
Back
Top Bottom