Kuweni makini, utapeli mpya umeibuka Dar

Kuweni makini, utapeli mpya umeibuka Dar

Hamuyu

Senior Member
Joined
Mar 29, 2010
Posts
118
Reaction score
21
Nilikua njiani naelekea ofisini kwangu, nikiwa mitaa ya Darajani Zanzibar simu yangu iliita aliyenipigia alijitambulisha na nilikua simjui, alisema yupo Mkoani Kigoma anafanya kazi shirika moja la kimataifa, alinieleza anahitaji mtu wa kushirikiana naye katika mambo ya kibiashara anayetoka Zanzibar, alidai alipatiwa namba yangu na moja kati ya rafiki zangu wanao ishi Uk, na hakutaka nimuulize niliendelea kumsikiliza.

Akaanza kunielekeza anafanya Biashara ya kununua Product ambayo inahifadhi vyakula visiharibike na akanipatia namba ya mtu anayehusika katika utengenezaji wa production na jina lake akadai anaitwa Ibrahim na anapatikana Mahonda Zanzibar, akaniambianimpigie Ibra kumuuliza kama hiyo Production ipo na inapatikana kwa bei gani, nilimpata Ibrahim na akanieleza wanazo bidhaa kutoka ncho tofauti lakini best zinatoka Sweeden na bei yake kwa chupa 2 ni T shs 1,200,000/= nikamjibu yule jamaa aliyenitambulisha kwa Ibra kwamba bei yake ndio hiyo, baada ya hapo akaniambia kwamba pia wapo mabosi wake wa kizungu wamefikia Zamani Kenpisky Hotel Pwani Mchangani wananunua hiyo bidhaa kwa bei ya juu sana mara 2 ya bei ya kununulia, wakati nawasiliana na hawa jamaa tokea dakika ya kwanza niligundua kwamba hawa ni matapeli na nilichukua hatua za kuripoti tukio hili kituo cha Polisi na walifika kwa wakati nikawa nawashirikisha katika mawasiliano na hawa matapeli.

Polisi niliwapatia namba za simu za hawa jamaa wakaweza kuzifanyia utafiti na wakagungua wenye kuzimiliki, na sasa baada ya muda mfupi nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwamba anaitwa Fred yupo Kenpsky na ameelekezwa kwangu kuja kununua Product mimi sikujivunga nikamwambia zitapatikana ndio hapo akaniambia kabla sijapeleka mzigo nimpelekee sample 1 pair ili akiridhika nao ndio tunaondoka pamoja na kwenda kuchukua mzigo wote.

Nikamweleza yule jamaa aliyenipigia simu mwanzoni kwamba wanunuzi wanahitaji sample wakiridhika ndio wanunue mzigo wote, hivyo akaniambia niwasiliane na Ibra kuhusu sample nikampigia akaniambia beio yake ndio hiyo aliyoniambia hapo juu Milioni moja na laki mbili, nikamjulisha jamaa akaniambia nifanye maarifa nipeleke hizo pesa.

Nikawaeleza Polisi tukaweka mtego baada ya muda kidogo nikawaambia kwamba fedha tayari waniletee mzigo, wakanielekeza walipo wakaniambia wapo Kibweni tukaenda mimi nilitangulia na polisi wakiwa nyumba yangu kwa umbali kidogo, nikapiga simu akaja kijana mmoja akaniuliza ni wewe niliyeagizwa kuhusu mzigo nikamwambia ni mimi na mzigo uko wapi nikupatioe hizo fedha? akaniambia nimsubiri kidogo akaufuate niliendelea kusubiri pale na kupiga simu hakutokea baadae alizima simu kabisa.

Nikawaarifu polisi kwamba jamaa wameshtuka nikarudi ofisini kwangu. nilichoamua kufanya baada ya hapo niliwapigia simu wale jamaa wote tuliokuwa tunawasiliana kwamba nawashukuru sana mzigo nimeupata na tumeshafanya biashara nimemkabidhi jamaa Milioni moja na Laki mbili ispokuwa jamaa aliyepokea pesa alitaka wale jamaa wote wasijue kama tayari ameshapokea fedha.

na nikawashukuru sana sikujua kilichoendelea baada ya hapo, hii ni tahadhari natoa kwa wenzangu wa JF na watanzania tuwe makini na tujiepushe na tamaa za kijinga tutaingizwa mjini.

nawasilisha.
Wana JF, mchana huu nimepigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama Mr Makombe wa WFP Kigoma na akanieleza kwamba kuna opportunity ya kupata pesa kwa ku-supply madawa ya kunyunyizia nafaka huko WFP Kigoma. Akasema kama niko tayari aniunganishe na bosi wake mzungu, kwa upande mmoja na muuzaji wa hayo madawa. Akazidi kuniambia kwamba yeye hataki kuwasiliana na muuzajio kwani walikorofisha mara ya mwisho - yeye Makombe hakupata mgao wake.

Nikamwambia sawa. Akanipa namba 0717289138 ya muuzaji dr Peter na nilipompigia huyu dr akadai anayo madawa aina ya damoline iliyotengenezwa sweden na anayauza kwa dola 3600 kwa pair moja. Mara nikapigiwa na huyo mzungu aliyesema kafikia Golden Tulip akitaka pair 50 na nimpelekee sample kwanza na akiridhika na ubora wake tutaandikiana mkataba ndipo nimletee pair hamsini kwa bei ya dola 4400 kwa pair (hii ndo bei ambayo mr makombe alisema nimtajie huyo bosi wake mzungu wa wfp!

Kwa kuwa nilikwisha soma katika magazeti fulani juu ya utapeli wa aina hiyo niliamua kuwapigia na kuwambia waache utapeli na wizi utawafikisha pabay. Kusikia hivyo wakakata simu. Kwa tahadhari simu wanazotumia kwa leo ni: 0752565642 na hiyo hapo juu.

Wanachofanya ni kwamba ukikubali dili ukaenda kwa dr ambaye ni mwenzao ukalipa dola 3600 ndo umeliwa hapo - wanazima simu na hutosikia cha mzungu wala nini.

Chukueni tahadhari
Ndugu wapendwa,

Story ifuatayo ni ya kweli maana imenitokea mimi binafsi jana tarehe 10/18/2011. Najua kwa kiasi fulani itakuwa inaninizalilisha kwa kutokuwa makini lakini naona ni vyema niwashirikishe rafiki zangu ili msije mkatapeliwa kama mimi na wengine wengi wameshatapeliwa kama vile ndugu yake Galeba, laiti Galeba angeweza kutuelezea yaliyomsibu ndugu yake labda na mimi ningeweza kuepuka utapeli huu. Kinchosikitisha matapeli wenyewe ni watu wanaotufahamu vizuri.

Mnamo muda wa saa tano asubuhi nikiwa nyumbani (nipo likizo) nikapokea simu nisiyoifahamu kutoka kwa mtu ambaye alijitambulisha ananifahamu, na kwa jinsi alivyonitaja kwa jina na career background details zangu sikuwa na shaka kwamba hanifahamu. Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:

TAPELI: Mr. Alex Matovu habari za siku nyingi.
Mimi: Nzuri
Tapeli: Vipi bado unafanya kazi Blue Financial Services?
Mimi: Hapana, nani mwenzangu?
Tapeli: John, nilikuwa nafanya kazi Wizara ya elimu, na uliwahi kunisaidia nikapata mkopo, ila kwa sasa nipo World food programme, Kigoma kama Chief supplies officer.
Mimi: okay sasa nikusaidie nini John (ukweli nikwamba sikumkumbuka ila kwa kuwa tulikuwa tunatoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali, siku jiuliza sana, after all alikuwa hajasema anachotaka)

Tapeli: Sasa nina issue naomba unisikilize kwa makini, kama unavyofahamu WFP tunatoamisaada ya vyakula hivyo tuna maghala makubwa ya kuhifaadhi chakula, hivyo ili kuhakikisha vyakula haviharibiki huwa tuna weka presavative inayoitwa Damoline Liquid solution made in Sweeden, hii inapatikana MSD na kwa licensed dealers kama Mohamedi Enterprises. Kwahiyo tuli float tender mwaka jana na supplier aliyeshinda tulikubaliana anipe 10% lakini baada ya ku supply hayo madawa akanidhulumu na kunitisha kuwa iwapo nitamdai hiyo 10% angeniripoti kwa mabosi wangu. Kwa hiyo sikuwa na cha kumfanya bali kusubiri contract yake iishe alafu nimtafute supplier mwingine. Sasa ndio nikaona nikupigie ndugu yangu maana nakujua wewe hii kazi utaweza kuifanya ukizingatia unalipwa cash on delivery!

NOTE: nimeshawahi ku deal na supplies officer wengi hivyo sikuwa na doubt yeyote, bali nikaona hii is just another deal kama ambazo nimeshawahi kufanya successfully.

Mimi: Okay sasa unataka nifanye je?

Tapeli: Unachotakiwa kufanya ni kwenda MSD umuone Dr. Shija, huyu ndiye mkuu wa hapo na ndiye aliyekuwa supplier wetu wa zamani aliye ni dhulumu, sasa kwa kuwa sitaki kumpa kazi tena, wewe uende ujifanye unaulizia hiyo liquid solution, na u negotiate ujue atakuuzia shillingi ngapi. Kwahiyo nakutumia simu yake mpigie muongee akupe quotation, alafu akisha kupa bei nipigie ili nikuelekeze cha kufanya.

Basi wandugu nikampigia dr. shija, mwanzoni shija ana hesitate kuzungumza na mimi aki pretend kuwa hapendi kuongea na strangers na akataka kujua namba yake nimeipataje, sasa kwa kuwa siwezi kumwambia ukweli kuhusu aliyenipa namba yake, ikabidi na mimi niwe muongo kwa muda, nika pretend kuwa mimi ni mkulima na nahitaji hiyo presavative kwa ajili ya maghala yangu yaliyopo arusha. Basi akawa na imani na kukiri kuwa anayo stock yakutosha, na hiyo liquid inauzwa kwa pair ya chupa mbili zenye ujazo wa 1000mls, kila pair ni 1.2m. Sasa angalia nilivyoingia katika mtego, baada ya kunipa bei ni kaomba punguzo na akasema atauza kwa 1million.

Nikafanya kama nilivyoelekezwa na John wa WFP kuwa baada ya kupata bei nimjulishe nilivyomjulisha akasema kinachofuata ni kuwa mimi nitauza kwa USD. 1700, na tofauti kwa maana ya faida tutagawana, hivyo nisubiri aniunganishe kwa bosi wake for further final details.

Basi wandugu kama mnavyonijua katika issue za fwedha, nikachukua calculator ya simu ili nijue deal ina shillingi ngapi, hela zilivyokuwa nyingi hata calculator iligoma, maana WFP wanahitaji 50 pairs @ usd 1700, mimi nanunua kila pair kwa 1million ambayo ni kama usd 770 hivyo difference usd 930 x 50 pairs = USD 46500, ALAFU tunagawana pasu pasu. Guys you can imagine what was going on in my head!

Basi kweli muda si mrefu nikapigiwa simu na huyo bosi wake ambaye ni mzungu na mazungumzo yalikua kama ifuatavyo:

MZUNGU: This is Mr. Scheinder from WFP, are you the new supplier?
MIMI: YES
MZUNGU: Do you have enough stock of Damoline Liquid solution, we are looking for 50 pairs?
MIMI: Yes I have sufficeint stock
Mzungu: what is your price per pair?
Mimi:$1700
Mzungu: ahaaaaaaaa thats a very good price, do you want to be paid in dollars or TZS
MIMI: Dollar of course, you how how unstable the local currency is ( Hapo tena na mimi nataka kuonyesha kuwa ni International businessman)
Mzungu: No problem, we have enough dollars, you want to be paid cash or by cheque?
Mimi:Cash
Mzungu: Okay no problem, now listen very carefully mr. new supplier we need this liquid urgently possibly today, and since you have said you have enough
stock we are taking off this morning from Kigoma coming to Dar, please arrange for the transport to take us to Movenpick, we will pay usd. 200 for your fuel, but most importantly make sure you bring one pair of the sample with you.
Mimi: No problem at all I have been in this business for quite sometime now you can be sure everthing will be fine.

Masikini bila kujua nimeingizwa kingi, nikachukua cheque book, nikaandika cash withdraw 1million ili nikanunue sample yakwenda kuwaonyesha wateja wangu. Baada ya kutoka bank nikampigia dr. shija ili aniuzie hiyo sample, akasema kwa sasa ametoka ofisini ila sample anazo katika gari na alikuwa anaelekea Mwananyamala hosp, then Magomeni alafu Muhimbili, hivyo tukutane Magomeni hosp. Yaani jinsi nilivykuwa naendesha gari basi hata kama ni mashindano ningeweza kushinda, basi mimi mbio mpaka magomeni hosp namsubiri dr. shija. Nikampigia akasema yupo ndani hospitalini na yupo na mabosi wake asingeweza kutoka ila anamtuma kijana wake nimpe hizo fedha na yeye anipe hizo dawa, kweli ikawa hivyo kijana akaja akaingia kwenye gari nikamwambie anipe hizo sample kwanza nikazisoma ziko exactly kama WFP wanavyotaka! NIKAKABIDHI HELA 1 MILLION. Bila hata aibu yule kijana akaniomba 50,000/= nikamwambie asijali maana deal kubwa itakamilishwa saa nane.

Kwa kuwa wageni wangu walishaniambia niwaaandalie usafiri, nikampigia dreva tax wangu aje airport saa nane, nikamuuliza bei kutoka airport mpaka movenpick ni ngapi akasema 25,000 nikamwambia usijali ntakupa 50,000/=!!!!!!!!!!!!! (kumbuka mimi ntalipwa usd 200 ya usafiri).

Basi mimi mbio nikaenda airport terminal one kusubiri ndege ya WFP ili tumalize biashara, nilipofika kuulizia reception nikaambiwa hakuna kitu cha namna hiyo na mimi ni mtu wa 10 kutapeliwa, basi tena nikajirudia kimya kimya. Nikaenda kula chefs pride nikamsimulia jamaa mmoja yaliyonisibu, kabla sijamaliza akasema hata ndugu yake ametapeliwa wiki iliyopita, nikampigia Galeba akasema yeye jamaa yake alipigwa 3.5m last week.

Taarifa nilizonazo mpaka nikuwa hii ni network ya wahaya na mpaka sasa ni wahaya wengi wameishaibiwa ukilinganisha na makabila mengine.

So guys thats my story for yesterday!
 
Mjini shule ami, pole sana. Namshukuru Mungu hukuingia kwenye mtego wao....
 
Mjini shule ami, pole sana. Namshukuru Mungu hukuingia kwenye mtego wao....

Mkuu nilipofika ofisini niliwashirikisha wenzangu tukawa tunashauriana cha kufanya, haya mambo nikuepuka tamaa zisizo na msingi hakuna short cut ya kihivyo kwenye maisha tunahitaji kupambana Ahsante
 
ami pole sana hizo dili wameandika wengi kweli humu zingine wameumizwa ndio wakaja wengine ka wewew wamewah..pole ami
 
ami pole sana hizo dili wameandika wengi kweli humu zingine wameumizwa ndio wakaja wengine ka wewew wamewah..pole ami

Ok, niliona kwenye moja ya magazeti ya udaku kuna Miss Tz mmoja na yeye yalimkuta tena niliposona walitumia nyia za mana hii hii, Ahsante tuwe makini kwa pamoja
 
Wengi wamelizwa na huuutapeli, lakini mimi nadhani ni wajinga kwa sababu mtiririko wooote wa hao matapeli unaacha maswali mengi kwa mtu anayejiuliza mara mbili mbili.

Kuna jamaa mmoja walimwingiza mjini kikwelikweli.... Unajua walifanyaje?

Walipoleta ile sampo akaichukua kwa shilingi milioni moja.... halafu kule alokoagiziwa apeleke akakuta ni 'wateja wa ukweli'.... na wakamlipa fedha nzuri tu..... mara mbili ya ile aliyotoa, na wakamwambia wanataka mzigo zaidi. Si jamaa alikimbia mbio mbio dukani kwake akamwambia kijana wake kusanya mauzo yooote unipe kwani nimepata dili la nguvu...
akapitia benki akakomba ka-akiba alikokuwa nako kooote, akaona haitoshi akaenda kwenye duka la rafiki yake akakopa fedha... akaenda kuchukua 'mzigo' wake. Sasa kazi ilikuwa 'kuuza' kwani jamaa wale wanunuzi waliyeyuka wooote.

Sisi tukamwambia yale 'madawa' si madawa kweli, lakini hakuamini alikaa na yale mafurushi kwa mda mrefu .... sijajua kama aliyatupa lini, ila jamaa alikonda sana, japo sasa amejitahidi hali yake kifedha imeanza kuwa nzuri....
 
Tuache tamaa ya kutaka utajiri wa haraka haraka ndipo tutapona kwenye utapeli huu. Kwenye mazingira ya kawaida mtu usiyemfahamu hawezi akakuunganisha na dili zenye faida kwani yeye hana ndugu zake! Hongera sana umepona kuibiwa.
 
Haya yote yanatokana na kuwa na tamaa ya utajiri wa haraka!
 
Hii taadhari ilitolewa humu mara nyiiiiiiiiiingi mpaka! Wewe hukuwepo naona pole sana
 
Pole sana hata mimi last year ili nitokea, lakini nilikua nimeshasoma malalamiko kama haya humuhumu nadhani so walivonieleza baada ya hapo sikupokea cm ya huyo mtu. Pole sana.
 
Wadau kuna utapeli mpya ambao unafanana na blackmailing kwa wafanyakazi wa Serikali, wafanyabiashara na watu wengine.

Matapeli wanawapigia simu za kuwatisha wafanyakazi wa Serikali kwamba wao ni maofisa usalama wa taifa na wameona mafaili yao ni machafu hivyo wanashawishi wawasaidie ili wayasafishe kwa kuwahonga.

Wafanyabiashara wanatishwa kwamba wanakwepa kulipa kodi na wakigundua una fedha wanaweza kukuteka.
 
Utapeli huu umeshika kasi sana siku hizi.
Ugumu wa maisha unapoongezea huenda sambamba na kuongezeka kwa uhalifu
 
Hii nzuri sana.
Sasa kama wewe ni mfanyakazi wa serikali mtu akakupigia simu akakwambia ana faili lako chafu na wewe ni msafi unaogopa nini?

kama wewe ni mfanyabiashara mtu anakupigia simu anakwambia unakwepa kodi wakati wewe ni msafi unaogopa nini?

Mimi naona hao matapeli waaendelee kuwepo tu.
 
kama we ni msafi sioni watakutapeli vip... uwe mfanyakazi au mfanyabiashara kama ni muadilifu huna haja ya kuwaogopa hao watu
 
Back
Top Bottom