Kuweka watu ndani masaa 48, Mkuchika awataka wakuu wa Wilaya na Mikoa wasimharibie kazi

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Waziri Mkuchika:” Wakuu wa Wilaya/ Mikoa wanaojimwambafai msiniharibie kazi yangu ”

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora wakati akijibu hoja za Wabunge amewataka wakuu wa Mikoa na Wilaya kuzingatia Sheria inayowapa madaraka ya masaa ya kuwaweka watu ndani ili wasimuharibie kazi yake kwani yeye ni Waziri wa Utawala Bora na bado anaipenda nafasi yake.

wengi wa viongozi hao wamekuwa wakikiuka sheria kwa kufanya kinyume na sheria inavyotaka ambapo pia ametumia muda huo kuwaonya.

“Mkuu wa mkoa amepewa saa 48 za kumuweka mtu ndani lakini nachotaka kusema sio lazima wewe umuweke ndani, tuache kujifanya mwamba na naomba msiniharibie mambo mimi ndio Waziri wa Utawala bora”.
 
Janja tu ya Kumsafisha Rais ili aonekane haungi Mkono yanayofanywa na Wakuu wa Mikoa &Wilaya..
Dunia inajua.. Lissu Kawashika sawasawa..
Lisu hausiki hapo, hata hajui bunge linaendeleaje, yupo anakunywa Champagne na mabwana zake wazungu...

Wakuu wa wilaya na mikoa washazoea kuweka watu ndani bila sababu kubwa ya kiusalama. Ndomana waziri amekuja juu kutoa muongozo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani yameanza leo haya ya kuweka Watu ndani?
Tangu 2016 haya yamepigiwa Kelele na Upinzani, Akiwemo Lissu Kabla ya shambulio..
 
Lisu hausiki hapo, hata hajui bunge linaendeleaje, yupo anakunywa Champagne na mabwana zake wazungu...

Wakuu wa wilaya na mikoa washazoea kuweka watu ndani bila sababu kubwa ya kiusalama. Ndomana waziri amekuja juu kutoa muongozo

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uzuzu, kwani wameanza juzi? Jafo katoa matamko, Mkuchika si Mara ya kwanza, Magufuli kasema lakini kesho yake Malima kamuweka ndani diwani kwa kosa la kukunja nne!!!! Hao wakuu wa Wilaya wanejiteua hadi wawe na kiburi kiasi hicho kama hakuna nguvu toka kwa mteuzi jeuri hiyo wanaipata wapi? Uteuzi wa kwanza Magufuli aliwaambia wana mamlaka ya kuweka watu ndani wakayatumie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom